Tanzaniaist
Senior Member
- Nov 29, 2011
- 161
- 156
Habari zenu wana JF..,leo hii kwenye mada yangu napenda kugusia wabunge wa CHADEMA ambao wamekuwa Nguzo mhimili wa Chama pamoja kama sehemu ya serikali (Bunge)
Niwapongeze sana kwa kuweza kuhimili mikiki na mizengwe ya CCM tangia uchaguzi paka sasa hivi kwani kumekuwa na suala la hawa wabunge kufungiliwa kesi na kubambikiziwa makosa yasiyokuwa na msingi baada ya jeshi la polisi kushindwa kutimiza wajibu wao wa kusimamia haki na kushurutushwa na Siasa
Katika kampeni za Uchaguzi, wabunge wengi wa Chadema waliahidi mambo makubwa ili waweze kuchaguliwa na vile vile waweze kuzidi hoja wapinzani wao..,na kuna baadhi waliamua kufunguka kwa kuwaambia wananchi ukweli kama John Mnyika na Tundu Lissu kuhusu majukumu na wajibu wa mbunge..!
Na hili suala limekuwa tatizo sana kwa wananchi, wengi hawajui kazi ya Mbunge ni nini..? wamekuwa wakitoa tu malalamiko bila sababu za msingi hasa hapa Jamvini..
Mimi ninaamini Kazi ya Mbunge, Sio KUJENGA BARABARA, KUCHIMBA VISIMA, KUNUNUA MADAWATI, KUJENGA MADARASA, KULIPIA ADA WANAFUNZI, KUNUNUA DAWA NA VITANDA MAHOSPITALINI, KUCHIMBA MITARO, KUTOA MIKOPO, na N.K
Bali mimi naamini Kazi ya Mbunge ni kuisimamia serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi, kwa kuwa serikali INAKUSANYA KODI, MBUNGE KWA MSHAHARA WAKE WA MILIONI MBILI ukizingatiwa anakatwa kodi na mkopo wa gari.,na posho za bungeni hata kama wakipewa hizo 250,000 tshs Mbunge HAWEZI kujenga barabara,..au kufanya mambo makubwa hapo juu niliyoyataja ukizingatiwa wengi wana familia au wengine ndio wanaanza maisha au hata wengine walikuwa Mafukara..,TUWALAUMU wabunge ili wafanye kazi lakini TUSIWAHUKUMU..,
Serikali ndio imekuwa chanzo cha matatizo kwani inakusanya kodi na kupokea misaada toka nnje lakini pesa zinaishia kuliwa na wachache ama kutokuwa na matumizi mazuri ya pesa..,na kushindwa kujenga na kuboresha huduma muhimu za kijamii...!
Na ninawaonea sana HURUMA wabunge wa CHADEMA, wanapata sana wakati mgumu kutimiza ahadi zao kwakuwa Halmashauri nyingi wanazotoka madiwani wengi ni wa CCM, na hata watendaji wa serikali wengi wanafuata matakwa ya CCM, na saa nyingine hata shughuli zao za kibunge kuvurugwa tu kwa makusudi na jeshi la polisi ama mizengwe ya watendaji ili mbunge aonekane tu hafai mfano,.Godbless Lema, huyu mheshimiwa tangia awe mbunge kila siku ni kufunguliwa kesi,kudhalilishwa na polisi bila sababu za msingi.,na kujikuta muda mwingi akipoteza muda na kushindwa kusimamia ahadi zake pamoja na shughuli za kibunge! na ningependa kuhoji kama Godbless Lema ni mkorofi kama watu wanavyosema mbona kabla hajawa mbunge hakuwa na kesi mahakamani...!
Na ikumbukwe kwamba hawa wabunge wa CHADEMA inakuwa ngumu kutekeleza ahadi zao kwakuwa hata serikali inaongozwa na CCM kwanzia Raisi na Mawaziri..,na ili matatizo yao yasikilizwe kwa urahisi itabidi wawe mawakala wa CCM kama LYATONGA MREMA wa TLP au JOHN CHEYO wa UDP,la sivyo itakuwa ngumu kutimiza ahadi zao na hata mambo kuwa magumu zaidi jimboni kwa kubaniwa huduma muhimu za kijamii..!
Sasa imefika wakati.,,Wabunge wa CHADEMA kutumia UMMA kuchangia shughuli zao za Kimaendeleo mfano.Alivyofanya Hezekiah Wenje alivyoandaa harambee kwa ajili ya madawati..,au Hata wabunge hawa wa CHADEMA kutumia wafadhili kutoka nje kufadihili miradi yao ya kimaendeleo jimboni kwani kuitegemea tu serikali itakuwa ni sawa na kujivika kitanzi..,Kwani Serikali chini ya CCM kila siku wanatafuta njia ya kurudisha hayo majimbo mliyoyapata kwa CCM..,nimpongeze sana MH.PHILEMONE NDESAMBURO kwa kupigana kiume hadi sasa hivi lakini sidhani kama asingekuwa tajiri asingeweza kuwa mbunge hadi sasa kwani amekuwa akitumia uwezo wake kifedha kuisadia serikali kuboresha huduma za kijamii lkn kama asingekuwa na uwezo huo mambo yangekuwa tofauti na hata kutimiza ahadi zake..! sasa kwa wabunge wengine ambao sio wafanya biashara hali itakuwa vp?
Napenda kuwasilisha..!