Katika watu wanaotoa mada za kijinga humu unaongoza!
Huwa una fikra hafifu sana!
Labda ndo job description yako pale Lumumba! Ama ndio uwezo wako ulipoishia!
Huna lolote wewe unabwata tu hata hujui nchi inakwenda wapi.
Mbunge wa Cadema mmoja sawa na wabunge wa magamba 50, mbunge wa Chadema akihudhuria kikao kimoja mchango wake ni sawa na michango 50 ya wabunge wa magamba
Sisi wananchi msidhani tumekufa au tumelala usingizi, pumba tunaziona hapo Bungeni hatuna haja kuwa na wabunge wenye kuhudhuria kipindi chote cha Bunge na hawana cha zaidi ni kufikiria posho , kuchapa usingizi , kushangilia kwa kila jambo kama hayawani na kufikiria ufisadi. Jamani kwa nini ukweli usisemwe kuwa CCM tumewachoka ?
Huna jipya mtoa mada! Mara ngapi tumesikia Rais yupo Dodoma na kuitisha mkutano na wabunge wa CCM wakati bunge likiendelea? Hii si kutumikia chama cha mapinduzi? Kama ingekuwa kutumikia taifa Rais angeitisha mkutano wa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri na si wale wa CCM tu! Acha propaganda isiyoeleweka.
Wana-JF;
Suala la wabunge wa CHADEMA kuendekeza chama chao kuliko utaifa (bungeni) kwa sasa limedhihiri.
Wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakikosa vipindi vingi vya bunge, tena kwa ujumla wao, huku wakizijua athari zitokanazo na mahudhurio mabovu.
Wamekuwa wakifanya 'chokochoko' makusudi kabisa, ili wamlazimishe spika kutumia kanuni awatoe, ili waende majukwaani na kukitumikia chama chao.
Tukio la Arusha nalo limefanywa kisiasa, kwani wabunge wote wa CHADEMA wamepanga kutohudhuria bungeni, ili wapate fursa za kukaa majukwaani na kukitumikia chama.
Wito wangu kwa CHADEMA, ifike wakati sasa taifa mlipe kipaumbele kuliko chama chenu, bunge la bajeti ni bora zaidi kuliko mnayo angaika nayo huko Arusha.
Nyie Waliberali si mmesema sasa mnapumua bungeni na vurugu zimeisha...
Kwenu nyie kuulizwa kuhusu wizi na ufisadi mnaofanya ni vurugu. Sasa mmeachiwa bunge mnalialia, hamna wema, sijui mnataka CHADEMA iwashike masaburi ndio mridhike