Wabunge ana kwa ana na zimwi lao


Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
38,994
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 38,994 280
Limewakaa kooni miaka miwili
Safari hii ni ama wao au serikali
Wabunge wakiwa kwenye kikao chao mjini Dodoma (Picha kutoka makataba)Wiki hii inaanza kwa kamati za Bunge kujadili miswada mbalimbali, lakini macho na masikio ya wananchi yanaelekezwa kwenye hatima ya Richmond, sakata lililochukua muda na rasilimali za taifa kwa muda wa miaka miwili bila kufikia ukingoni.
Hii itakuwa ni mara ya nne kwa wabunge kujaribu kujadili ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond, lakini kila wakati kikiibuka kisingizio hivyo kukwepesha mjadala huo. Kwa mujibu wa taarifa ya Bunge iliyotolewa wiki iliyopita, kamati za Bunge zinaanza vikao vyake kuanzia leo hadi Januari 22, pamoja na mambo mengine suala la utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu Richmond litawasilishwa kwa Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo.
Nipashe jana iliwasiliana na Shellukindo kujua kama taarifa hiyo imekwisha kuwafikia, lakini alisema kamati yake inatarajia kukutana kwa faragha wiki hii ili kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Richmond.
Kujipanga kwa kamati hiyo ni mkakati wa kupata msimamo wa pamoja kabla ya kuanza kujadiliwa rasmi kwa hoja hizo ndani ya kikao. Shellukindo alisema kwa kuwa hoja hiyo ni nzito itabidi wajumbe wote wakutane kwa faragha na kuweka mikakati ya namna ya kuishughulikia.
Hata hivyo, Shellukindo hakusema ni siku gani hoja hiyo itajadiliwa, lakini alisema itajulikana watakapopata ratiba ya shughuli za vikao hivyo. "Mimi nilikuwa jimboni kwangu na taarifa za kuwepo vikao hivyo nimeisoma kwenye magazeti ila kesho (leo) nitakwenda kumuona Katibu wa Bunge ili anipe ratiba hiyo," alisema
Shellukindo alisema kuna mambo mengi yatakayojadiliwa na kamati yake katika vikao vitakavyoanza leo hadi Januari 22 mwaka huu.
Hoja ya Richmond imekuwa ikiahirishwa kujadiliwa mara kadhaa katika vikao vya Bunge. Kashfa ya Richmond imekuwa donda ndugu katika siasa za Tanzania kiasi cha kujenga picha ya msuguano wa moja kwa moja baina ya mihimili miwili ya dola yaani Serikali na Bunge.
Serikali bado inaendelea kusuasua katika utekelezaji wa maazimio 23 yaliyopitishwa na Bunge Februari mwaka 2008, hususani kipengele kinachoitaka kuwachukulia hatua watendaji wake kadhaa waliozembea na kusababisha serikali kuingia katika hasara kwa kuipatia zabuni ya kufua umeme wa dharura Kampuni ya Richmond LLC ya Marekani wakati haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme huo wa megawati 100.
Kampuni hiyo ilipewa mkataba huo Juni 23, 2006 baada ya nchi kukumbwa na ukame mwaka huo uliyosababisha kukauka kwa mabwawa ya kuzalisha umeme. Mkataba huo wenye gharama za Dola za Marekani milioni 179 (Sh. bilioni 200) uliiwezesha Richmond na mrithi wake Dowans kulipwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Sh. milioni 152 kwa siku hata kama haikuzalisha umeme. Baada ya malalamiko yaliyotolewa na wabunge kadhaa, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Septemba 2007 aliunda Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba huo iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe. Wajumbe wengine walikuwa Herbert Mtangi, Stella Manyanya, Lucas Selelii na Mohamed Habib Mnyaa.
Taarifa iliyowasilishwa na kamati hiyo bungeni Februari 6, 2008 ilibainisha kuwa Richmond ilikuwa kampuni ya mfukoni na kwamba ilipewa mkataba huo kwa upendeleo, hali iliyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mawaziri wawili waliowahi kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi Februari 7, 2008.
Hatua hiyo ililifanya baraza la mawaziri livunjike na kumlazimisha Rais Jakaya Kikwete kuunda jipya baada ya kumteua Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu.
Pamoja na Pinda kuwahakikisha wabunge wakati akiahirisha mkutano wa Februari, 2008 kuwa maazimio yote yatatekelezwa na serikali, hadi sasa miaka miwili hakuna mtendaji wa serikali aliyewajibika wala kuwajibishwa kutokana na kashfa hiyo.
Wakati wa mkutano wa 16 wabunge waliibana Serikali iwawajibishe waliohusika na Richmond, lakini serikali ilishindwa kutoa maelezo ya kina, hali iliyomlazimisha Sitta kuipa muda zaidi hadi katika mkutano wa 17 kwa ajili ya kujibu hoja za Richmond na Kiwira. Hata hivyo, pamoja na Bunge kusema kuwa ajenda za Richmond na Kiwira zingejadiliwa katika mkutano huo, lakini ulimalizika bila kujadiliwa wala kutolewa maelezo ya kina.
Baadhi ya watendaji waliokuwa wakitakiwa na wabunge kuwajibishwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, aliyekuwa Mwanasheria Mkuuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi na Mkurugenzi wa Nishati, Bashir Mlindoko. Kuhusu suala la Kiwira, Serikali ilitangaza wakati wa mkutano wa 16 wa Bunge kuwa imeurejesha mgodi huo katika umiliki wa Tanesco na Shirika la Madini la Taifa (Stamico), lakini bado wabunge wanataka kujua kama waliokuwa wamiliki wake, wakiwemo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona watalipwa fidia.
CHANZO: NIPASHE
 

Forum statistics

Threads 1,250,866
Members 481,514
Posts 29,748,754