Wabunge aina ya Aden Rage hawatatufikisha popote kimaendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge aina ya Aden Rage hawatatufikisha popote kimaendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mo-TOWN, Jun 25, 2011.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Sikieni alichokisema jana; kuwa anawashukuru sana watu wa manicipal ya Tabora kwa kumchagua kuwa mbunge... nafasi ambayo amekuwa akitafuta kwa muda mrefu...Kwamba Tabora hawadanganyiki kwa kuwa hakuna jimbo hata moja lilochukuliwa na upinzani. Kauli ya Rage kwamba amekuwa akitafuta ubunge kwa muda mrefu inaonyesha kuwa lengo ni personal zaidi ya jamii iliyomchahua... amethibitisha tu kuwa alitaka kuwa mbungeSwala la kusema Tabora hawandanyiki ni dharau kwa watanzania. Nimuulize Rage vipi kuhusu ahadi mbalimbali ambazo zinatolewa na CCM zingine over 20 yrs old mpaka leo hazijatekelezwa je si kuwadanganya wananchi? Vp swala la umeme? Ubora wa elimu? Matatizo ya malipo ya walimu ni ahadi ya mwaka gani? Maisha bora six years later social services zinakuwa worse je si kuwadanya wananchi?Nimalize kwa kusema kama ni track record ya kudanganya basi CCM itakuwa inaongoza... after all upinzani haujawi kushika madaraka.Wabunge wasifanye bunge kuwa kijiwe cha majigambo juu ya vyama vyao na nani ni nani kamwe hawatasaidia kuleta maendeleo nchini TZ.
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  RAGE sio raia wa nchi hiindio maana anajipendekeza kwa magamba
   
 3. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wapo wengi wameingia bungeni kwa mgongo wa chama cha MAGAMBA ambao kwa hakika ni mzigo mkubwa.Yupo Juma Nkamia, Komba,Majimarefu,Koka na wengine wengi ambao kimsingi hata iwe vipi hawawezi kujenga hoja za kuwaletea maendeleo wananchi wao tofauti na ahadi zilezile za miaka 47.Yaani mwaka unaokuja tusipoangali tutaingiza bungeni hadi kina Gerad Hando, Kibonde na Shigongo kupitia chama chama cha MAGAMBA.Solution ni CHADEMA, kama huamini angalia mjadala wa bunge utagundua tofauti kubwa kati ya wabunge wa CHADEMA na MAGAMBA.
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama mtu anadiriki kuiba vitu vidogo vidogo kama mipira iliyotolewa na FIFA kwa FAT enzi hizo kwa manufaa ya maendeleo ya soka nchini, unategemea itakuwaje akipata cheo kikubwa kama ubunge? Pesa zote za maendeleo ya jimbo lake lazima zitafanyiwa kitu mbaya na zisijulikane zimepotelea wapi! Tabora maendeleo msahau, subirini maembe yakomae muangue mpoze njaa!

  Rage ni raia wa kule kwenye nchi isiyo kuwa na serikali kwa zaidi ya miaka 20, hawezi kisema vibaya CCM.
   
 5. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amejikuta amesema ukweli wake. Ameutafuta ubunge kwa muda mrefu na kwa mbinu mbali mbali. Ameanzia kujitangaza kwenye FAT, TFF mkoa wa Tabora, na sasa Simba. Hiyo yote alikua anafanya marketing. Ni vyema ajue kwamba jimbo analoliongoza halina utaratibu wa kumrejesha mbunge kipindi cha pili tangu enzi za mwalimu. Waulize akina Prof. Mgombelo, Kaboyonga, nk. Ajiandae kupisha, na safari hii atakabidhi jimbo kwa CDM, atake asitake.
   
 6. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jamani, kauli hii sio nzuri, siipendi ina element za kibaguzi.
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  rage raia wa nchi gani? maana anavosema katafuta kwa siku nyingi ubunge inaonekana amaedhamiria pia kulinda maslahi ya huko anakotokea. ni wa nchi gani tafadhali
   
 8. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwanza rage alishawahi kupatikana na makosa alipokuwa FAT na kupelekwa jela.Sheria hairusu mtu ambaye aliyepatikana na makosa ya jinai kuwa mbunge.Niambie rage amewezaje kugombea kama si kubebwa na magamba yake.Ok tuje kwenye hoja yake.TABORA hatudanganyiki! kama ndio hvyo basi watu wa tbr leo wangekuwa barabarani wakiandamana kwa ahadi feki za chama cha magamba walizodanganya sana.Kifupi anajikosha kwa magamba yake asiulizwe asili yake
   
 9. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nchi ambayo Hussein bashe anatokea
   
 10. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwanza rage alishawahi kupatikana na makosa alipokuwa FAT na kupelekwa jela.Sheria hairusu mtu ambaye aliyepatikana na makosa ya jinai kuwa mbunge.Niambie rage amewezaje kugombea kama si kubebwa na magamba yake.Ok tuje kwenye hoja yake.TABORA hatudanganyiki! kama ndio hvyo basi watu wa tbr leo wangekuwa barabarani wakiandamana kwa ahadi feki za chama cha magamba walizodanganya sana.Kifupi anajikosha kwa magamba yake asiulizwe asili yake
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,128
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  Hizi ndio hasara ya kuwapa wafungwa kama rage madaraka..angalia mambo anayofanya simba, anaconduct mambo ki criminal zaidi.. Jela imemuathiri huyo.
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!kumbe ukweli ukitamkwa huwa unauma sana!!
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ukweli utabaki palepale kuwa Rage ni mgeni(Si raia) na ni mbabaishaji wa kutupwa!!
   
 14. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mahakama kuu ilimsafisha baadaye
   
 15. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rage anajichanganya mara ubunge mara mwenyekiti huko simba, hawezi kufanikisha hata moja ni bora akaamua kuwa na moja
   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mshika Mbili Moja Humponyoka.
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  huyo RAGE NI KIONGOZI WA HOVYO KATIKA MAANA YA KIONGOZI WA HOVYO
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Amesababisha Ndimbo ajiuuzuru U-Afisa habari simba kwa kumwingilia madaraka yake.Anadai eti wameshamwambia ndimbo aache utangazaji ch 10.Mbona yeye ni mbunge halafu mwenyekiti wa simba.Yeye anaifanya simba kama ya kwake vile yeye ndio kila kitu. Matokeo yake simba ilpoenda kongo kucheza na motema pembe,walikaa walizuiwa kiwanja cha ndege kwa muda mrefu kwa sababu timu ilikuwa haijafanya mawasiliano na wenyeji wao kazi ambayo inapaswa kufanywa na afsa habari.
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kutaka ubunge kwa muda mrefu siyo hoja, hoja inakuja sasa umeupata je baada ya miaka mitano wana-Tabora wategemee nini zaidi ambacho leo hii hawana?. Tabora siyo kwamba wananchi hawadanganyiki ila uswahili umezidi, kwa wakazi wake wengi kukosa elimu na kutokutilia maanani suala la elimu kwa watoto wao na wengi wao wakiisha piga kura hawajli what next whether kura zinzchakachuliwa au la, ndiyo maana ninawashawishi CDM Tabora waitembelee sana katika kutoa elimu ya uraia. Rage anatakiwa kutumia muda mwingi sana katika kuwashawishi viongozi wa CCM wanaopitisha majina ili aweze pata nafasi ya kupitishwa tena.

  Mbunge wa Tabora mjini aliye-serve muda mrefu alikuwa Misigalo, kuanzia hapo ninakumbuka tokea hapo wabunge waliopita kama mvua ni Kisanji, Mgumia, Busongo, Mgombelo, Kaboyonga na sasa Rage, hii ni ndani ya miaka si zaidi ya 30, inaonesha kuwa kupata term zaidi ya moja kuongoza jimbo la Tabora mjini ni big deal. Sababu kubwa ni kwamba Tabora imesahaulika na wakuu wa CCM wanajua fika kuwa njia pekee ya kuendelea kulishika jimbo ni kuwawekea mgombea mpya kila uchaguzi ili wananchi wadhanie kuwa labla huyu atawasaidia.

  Rage anachotakiwa kufanya kwa sasa si kuwasifia wana-Tabora ambao kwa uelewa wangu wa kuishi mkoa huo wengi ni watu masikini sana. Anatakiwa kutumia muda huu kuishinikiza serikali ihakikishe kuwa 2015 wanatabora wa miaka hamsini iliyopita wamepiga hatua, kulikuwa na viwanda kama cha nyuzi, cha nyama n.k vyote ni historia. Tabora wanalima Tumbaku ila inakuwa processed Morogoro, haya ni mambo ambayo anatakiwa kuyafuatilia kama kweli anahitaji kuliongoza jimbo kwa vipindi zaidi ya kimoja. Vinginevyo atakuwa ni one term kama wenzake wanne au watano waliomtangulia.

  Mitaa ya Tabora mjini yote miaka ya 70 kurudi nyuma ilikuwa ina rami, taa za barabarani zilikuwa zinawaka mitaa yote usiku, leo hii hakuna hata mtaa mmoja wenye taa za barabarani, barabara zote zimekuwa na vumbi hata ushaidi wa rami hakuna, watu wanakula mlo mmoja wa kesho hawajui watakula vipi, mtu akikuona unakunywa soda anaenda kutangaza kuwa una matumizi mabovu ya pesa, uwanja wa Ali Hassan mwinyi tuliochangia pesa zetu kwenye bidhaa kama sukari, mafuta ya taa yaani kila kitu tulichonunua kilikuwa kinaongezewa shs 1 mchango wa uwanja enzi hizo dola moja ilikuwa shs 50. Uwanja huo tokea alipohamishwa Dr Lawrence M Gama (RIP) ukuu wa mkoa mpaka leo hakuna la maana, timu yao ya Milambo imekufa na Dr Gama.

  Hebu Rage tueleze mambo haya utafanyaje kuhakikisha yanatengemaa?, badala ya kusifia wanatabora tu?, sifa haziondoi njaa, sifa haziondoi dhiki na umasikini. Ninatarajia Rage utakuwa makini sana kuiwajisha serikali yako ya CCM, vinginevyo watakuwajibisha wewe 2015 kwa kumuweka msanii mpya ili waendelee kulishikilia jimbo. Sooner or later wanatabora wanajua kuwa with CCM there is no future na ikifikia hapo basi ujue hakuna wa gwnda la kijani atakaye weza kuwashawishi tena. Maana watakuwa hawadanganyiki kweli. Mimi ningekuwa Rage ningejiuzulu uenyekiti wa clab ya simba ili niweze kuwatumikia wanatabora vizuri!
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatiza sio uraia tatizo ni anafanyia nini madaraka aliyopewa kwa faida ya waliomchagua. Tatizo Ni Uzalendo

  Yule mama claire short wa UK aliyepinga Tanzania kuuizwa raia sio raia wa Tanzania . Chenge n i raia tena mzawa lakini nani mwenye faida kwa Tanzania na watanzania.

  Kuna watu ni raiahalali laikini si wazelendo na kuna ambao si wazawa lakini ni wazalendo.

  Viongozi wengi pamoja na uraia na uzawa wao sio wazalendo. wich diqsqualify them to lead.
   
Loading...