Wabunge acheni hizo!

Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,523
653
Jana kwenye kikao cha bunge wakati mbunge wa CHADEMA- Leticia Nyerere alipokuwa anazungumza alikuwa akichanganya kiingereza na kiswahili, kuna mbunge mwingine simkumbuki jina wala chama chake akaomba mwongozo wa mwenyekiti kwa kutoa taarifa kwamba ni kinyume na kanuni za bunge (akaisoma) kuchanganya lugha na kuwa inaruhusiwa pale unaponukuu, mwenyekiti George Simbachawene aliafiki na kuwataka wabunge wazingatie kanuni hiyo, ajabu ni kwamba huyo bi leticia nyerere akaibuka na kusema anaikataa taarifa hiyo, je huo ni uungwana? sina tatizo na mbunge kuchanganya lugha najua inaweza tokea bila kudhamiria kwa bahati mbaya pia wabunge wengine huwatokea hivyo na hata watu uraiani huwatokea, lakini kinachonikera pale mbunge anapopewa taarifa yenye mantiki na ukweli na mbunge mwenzie halafu anasema taarifa haipokei au haikubali, huko ni kuendekeza ligi bila sababu za msingi, na tatizo hili lipo kwa wabunge wa vyama vyote, kama taarifa haina msingi au ukweli au ni tata, hapo ipo haki ya kuikataa lakini sio kukataa hata taarifa ya kikanuni,ni kujidhalilisha na kukosa hekima, kwani kukubali taarifa ya kweli ni uhalifu? tena kwa suala la leticia nyerere alionywa na mwenyekiti kuwa kukataa mwongozo uliotolewa na kiti ni ukosefu wa nidhamu na anaweza kuchukuliwa hatua siku nyingine.Maoni yangu ni kuwa wabunge waache ligi zisizo na msingi, wadau wenzangu mna maoni gani?
 
Back
Top Bottom