Wabunge 27 hawajawahi kuuliza swali miaka mitatu,yumo Prof Sarungi wa Rorya

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Wakati mijadala kuhusu malipo makubwa ya wabunge ukiendelea imebahinika kuwa kundi la wabunge 27 hawajawahi kushiriki kikamilifu shughuli za bunge ,ikiwa ni pamoja na kutouliza maswali ya msingi na hata kuchangia mijadala muhimu kitaifa
Mshaara wa wabunge ni shi milioni sita kwa mwezi na kwa miezi 39 ambayo wamelitumikia Bunge hadi sasa wamelipwa sh Bilioni 6.318 mpaka sasa kwa kuwa tu wabuge,hii maana yake ni kwamba kila mbunge amelamba 234 (sawa na mshhara wa watumishi 2000 wa serikali
Ni hawa wafuatao
Prof PHIELIMON SARUNGI ,EDWARD LOWASA ,ROSTAM AZIZ ,WILIAM LUKUVI ,SADIQ MURAD ,BAKARI MWAPACHU ,JOSEPH MUNGAI ,ABDALAH SALUUM ,THOMAS MWANGONDA , CHRISTINE ISHENGOMA ,na ZAKIA MEGHJI
wengine, ALLI Haji ali, ANNA ABDALA HASAN ,RAJABU KHATIB,OMAR SHEA MUSA, EUSTACE KATAGIRA ,NAZIR KARAMAGI
 
Nadhani unaweza usiulize maswali lakini ukawa na michango ya msingi ( substantive contribution) Tom Mwang'onda kwamfano nakumbuka alichangia mjadala wa budget ya wizara ya ajira na maendeleo ya vijana na alitoa mchango mzuri sana ikimaanisha alijitayarisha vema.Wengine kama akina Karamagi na Lowasa hawa walikuwa wasemaji wa serikali kabla yakupatwa na ajali za kisiasa na kwa sasa nadhani itakuwa ngumu kwao kuanza kuuliza maswali.Rostam inaeleweka kwanini yuko bungeni na hakuna haja hata kujaribu kujadili.Wengine kama Lukuvi ni mkuu wa mkoa sijui atamuuliza nani swali na yeye ni sehemu ya serikali.Zakia Meghi aliteuliwa ili apewe uwaziri hivyo hawakilishi jimbo lolote.
 
hii inamaana hata kuchangia kwa maandishi? au kuitikia "ndiyooo" pale spika anapouliza waliokubali hoja za kifisadi fisadi?
 
Hapo wakulaumiwa ni mwananchi anaye chagua mtu goigoi aende kumwakilisha alafu akifika bungeni anaweka mdomo plasta....mwananchi aliye mleta huyu mbunge bungeni ndo wa kwanza kulaumiwa ndiye aliye mchagua kwa kumpigia kura halali.
 
Kweli lkn usiwalaumu wananchi pengine wamewauzia kura zao je? mm mbunge wangu mh. O.S .Mussa wala sisemi asiponiwakilisha, karamiu ya wali wa biriani na pilau na kisimu cha nokia alichohonga kuwania uteuzi kwa wajumbe vinamlipa hizo 234m.
 
Kweli lkn usiwalaumu wananchi pengine wamewauzia kura zao je? mm mbunge wangu mh. O.S .Mussa wala sisemi asiponiwakilisha, karamiu ya wali wa biriani na pilau na kisimu cha nokia alichohonga kuwania uteuzi kwa wajumbe vinamlipa hizo 234m.

Mkuu mwananchi ndiye aliyeletewa mgombea ubunge na akampigia kura lakini kumbuka kuna wagombea kibao na sifa mbali mbali wao ndo huyo wamemchagua walaumiwe wao.
 
Kwani kama mambo yanaenda vizuri kwako, kwa anajimbo wako na chama chako kuna haja ya kuuliza?
 
Kwani kama mambo yanaenda vizuri kwako, kwa anajimbo wako na chama chako kuna haja ya kuuliza?

Mkuu tutajie jimbo moja tu ambalo mambo yanakwenda vizuri hapa Tanzania.
Ili liwe mfano kwa majimbo mengine.
 
HE!!:mad::mad:!! Na mbunge wangu yumo?!?!? Mbona anakujaga mitaa yetu na kusema anaipeleka puta serikali!!
 
List ina majina ya wengi waliokuwa mawaziri recently, labda ndo maana michango yao imekuwa hafifu.

Lakini as long as mambo yao yapo supa majimboni kwao, hawaoni haja ya kushiriki kwenye midaharo. Na hivi wegine ndo wametemeshwa ulaji (uwaziri) naona sasa watasusa jumla na kuuchuna tu. Sitarajii kuona mtu kama EL aanze kupigia kelele maendeleo ya jimbo lake!
 
HE!!:mad::mad:!! Na mbunge wangu yumo?!?!? Mbona anakujaga mitaa yetu na kusema anaipeleka puta serikali!!

Mkuu Mwazange.Lakini kumbuka Mzee Mwapachu anasema wazi kuwa hatumpi kura kwa sababu tunampenda...ni yale anayotufanyia kule Kisosora..sijaona kitu kule labda ni ile mikeka anayogawa bure Misikitini!!Lakini nakuthibitishia safari hii amesema anapumzika,hataki tena Ubunge....Naona Mwamvita na Mzee Juma Mwapachu wanajipanga....kazi kweli kweli!!
 
Wakati mijadala kuhusu malipo makubwa ya wabunge ukiendelea imebahinika kuwa kundi la wabunge 27 hawajawahi kushiriki kikamilifu shughuli za bunge ,ikiwa ni pamoja na kutouliza maswali ya msingi na hata kuchangia mijadala muhimu kitaifa...
Ni hawa wafuatao
Prof PHIELIMON SARUNGI ,EDWARD LOWASA ,ROSTAM AZIZ ,WILIAM LUKUVI ,SADIQ MURAD ,BAKARI MWAPACHU ,JOSEPH MUNGAI ,ABDALAH SALUUM ,THOMAS MWANGONDA , CHRISTINE ISHENGOMA ,na ZAKIA MEGHJI
wengine, ALLI Haji ali, ANNA ABDALA HASAN ,RAJABU KHATIB,OMAR SHEA MUSA, EUSTACE KATAGIRA ,NAZIR KARAMAGI

...wahoji nini ilhali wengine waliwahi shikilia nyadhifa muhimu kwenye serikali zilizopita? ushasahau ya kunyoosha kidole wakati vitatu vinakuelekea mwenyewe? au aliyemsafi aanze kutupa jiwe?, Kinywa huponza kichwa ati!
 
Kuchangia/kuuliza maswali si hoja sana. Kwa wapigakura wengi nadhani cha msingi ni jinsi mbunge anavyo'lobby' na kupeleka maendeleo jimboni kwake.
 
Watu wengine waacheni wajifie salama. Wamekwishagundua wakati wao bungeni umekwisha. Lakini utashangaa mtu kama Mungai bado anagombea ubunge na kushinda!
 
Mbunge wangu aligombea kwa mbwembwe, lakini alipoukosa uwaziri akazira na kuzirai. Wapiga debe wake nasikia kutwa wanahaha wakitafuta wanachoita "stimulus package" aweze kuzinduka mapema awahi kinyang'anyiro cha mwakani !! Tumlaumu Obama kwa kuongoza jopo la madaktari;)
 
Nadhani unaweza usiulize maswali lakini Wengine kama Lukuvi ni mkuu wa mkoa sijui atamuuliza nani swali na yeye ni sehemu ya serikali.Zakia Meghi aliteuliwa ili apewe uwaziri hivyo hawakilishi jimbo lolote.


WoS mchango wako mzuri sana. Hapa ndiyo kuna haja ya kutowateua Wabunge kutokuwa Mawaziri au Wakuu wa Mikoa maana badala ya kuwawakilisha wananchi kutoka majimbo yao basi huegemea 100% upande wa serikali kitu ambacho kinawaacha wananchi wa majimbo yao kama vile hawana wawakilishi bungeni.
 
WoS mchango wako mzuri sana. Hapa ndiyo kuna haja ya kutowateua Wabunge kutokuwa Mawaziri au Wakuu wa Mikoa maana badala ya kuwawakilisha wananchi kutoka majimbo yao basi huegemea 100% upande wa serikali kitu ambacho kinawaacha wananchi wa majimbo yao kama vile hawana wawakilishi bungeni.

Im with you 100%
 

Wengine kama Lukuvi ni mkuu wa mkoa sijui atamuuliza nani swali na yeye ni sehemu ya serikali.

Mheshimiwa huyu kwa mujibu wa rekodi za Bunge, alikwenda Washington International University kupata shahada ya kwanza mwaka 2001 akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni wapi, kivipi na wakati gani alipata muda wa kufanya homework za chuo huyu mdau hata sielewi. Anadai alifuzu. Lini? Hasemi.

Amekusanya vyeti vya "EDUCATIONS" za "leadership course," ana cheti cha "political course," "Defence and Security" bila kutaja majina ya vyuo zaidi ya kusema tu LINDI. IRINGA. MOSCOW. Moscow shule gani, wapi Mkuu?
Iringa chuo cha kikachero ni kipi hicho we jasusi-looking CCM aparatchik?

2797.png


Name: William Vangimembe Lukuvi

Constituent:
Isman

POSITIONS

1975 1980 Primary School Teacher

1980 - 1993 CCM Youth League District Secretary, CCM Head Office Deputy Secretary General, Youth

1994 - 1995 Bukoba District Commissioner

1995 - 2000 Ministry of Labour and Youth Development Deputy Minister

2000 - 2005 State, Prime Minister's Office (Policy) Minister

Date of Birth 15 August 1955

EDUCATIONS


School Name/Location
Lindi
Course/Degree/Award: Political Course
Start Date: 1976
End Date: -
Level: CERTIFICATE

School Name/Location Iringa
Course/Degree/Award: Training in Defence and Security
Start Date: -
End Date: 1980
Level: CERTIFICATE

School Name/Location Moscow - USSR
Course/Degree/Award: Leadership Course
Start Date: 1985
End Date: -
Level:CERTIFICATE

School Name/Location Washington International University
Course/Degree/Award: USA BA (Inter. Studies &Diplomacy)
Start Date: 2001
End Date: -
Level: GRADUATE


 
Back
Top Bottom