Wabongo si wa kuamini

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Kupitia stori na hata kushuhudia mwenyewe toka kwa watu wa karibu kweli na conclude wabongo walio wengi si waaminifu na wengi wanastahili kubakia na hali zao mbaya za kiuchumi
Stori iko hivi, kuna dada mmoja ni rafiki yangu, ile alipokuja tu hapa marekani ndugu zake nyumbani walianza kumpigia simu kulia shida, hawakujua dada wa watu ana pesa au hana wao walichojua anazo, so huyu dada akafanya kazi huku akijitahidi kuwasaidia ndugu kwa kile kidogo alichofanikiwa, miezi kama minne nyuma dada yake mkubwa akampigia kumpa dili la kiwanja hapo nje ya dar kidogo na bei aliyomwambia ni 4ml. So huyu dada akanipigia kuniomba ushauri, tukajadili kidogo na kwakuwa pesa yenyewe si nyingi nikamshauri akichukue so badala ya kutuma hiyo 4ml ya tz akatuma $4000. ambayo ni kama 7440000.Tsh so kilichotokea ni kwamba dada mkubwa kanunua kiwanja then kaandika jina lake na mume wake, mdogo mtu alipotaka ufafanuzi dada mkubwa anajibu kwa jeuri huku akidai atamlipa pesa zake.

Kiukweli ndugu zetu wengi walio bongo huwa hawathamini makubaliano hasa yanayohusu mambo ya pesa, hususani wachagga wenzangu, wengi wanapenda mambo ya kiujanja ujanja, huwezi mwamini mtu, hujui mtu anahustle kiasi gani, wakati wote jamaa wanataka kujifanya mabingwa na kukuingiza cha kike.
 
huo mtindo wa kutuma pesa jamaa mmoja alishakuta kibanda badala ya ghorofa. ...
 
Mwana tabia hii ya kutokuwa na uaminifu, inakatisha sana tamaa, naamini wengi wetu tunatamani tufanye miradi ya maendeleo bongo lakini utamwamini nani sasa, maana jamaa wajanja wajanja, wanafikiria kukuliza wakati wote
 
Aisee. ,
Alafu huyo ni ndugu mtu.Atakua alishindwa kumkopa akaona amdanganye kwamba ni kizuri anunue yeye.

Still sidhani kama hili ni swala la kikabila bali tabia ya mtu. Wapo kibao wasio waChagga na wanawafanyia watu wao hivyo. . . pia ambao ni waChagga na wanafanya mambo kuendana na makubaliano.
 
Wadanganyika wengi ni kama walking venomous vultures ready to pounce on the next victim.

Sku hizi hamna cha ndugu wala nini
 
Tatizo linakuja haohao walia njaa ndo wakwanza wasio waaminifu, kuna jamaa yupo toronto alimtumia mama yake pesa ya mradi akampa mdogo wake maana yeye ndo anajua jinsi ya kuzifuatilia western union, dogo alipozipata nusu tuu ndo ilifika kwa mam yao
 
Umeongea too general. Utapeli wa huyo mtu mmoja usifanye ndio tabia za wabongo wote hasa Wachaga.
 
Umeongea too general. Utapeli wa huyo mtu mmoja usifanye ndio tabia za wabongo wote hasa Wachaga.

hakuna cha too general....wabongo wengi siku hizi ni matapeli maskini kwa matajiri,wadogo kwa wakubwa,wanawake kwa wanaume wote matapeli period..na ndugu ndio zaidi ..
 
ni kweli waswahili walio wengi pengine >75% si wa kuwaamini...si mzee, si mbaba, si mmama, si mdada, hao vijana ndo hawafai kabsaaa....ni wasanii, wababaishaji...ni wizi na ujanjaujanja tu wa kupata pesa (mshiko). km huamini fanya deal na mswahili utakuja kutuambia hapa!
 
Ni kweli kabisa nakubaliana na dhana hii wabongo siyo waaminifu kabisa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom