Wabongo hatarini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabongo hatarini

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by VISIONEER, May 19, 2011.

 1. VISIONEER

  VISIONEER Senior Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HILI TATIZO LA MGAO HADI LINI WAJAMENI? BIASHARA ZETU ZINAKUFA MNATURUDISHA NYUMA KWENYE UMASIKINI TULIOUAGA.


  KUANZIA leo nchi itaanza mgawo wa umeme ambao utachukua siku nne kutokana na matengenezo makubwa ya mitambo ya gesi ambayo imekuwa ikizalisha umeme na kuingizwa
  kwenye Gridi ya Taifa.

  Hatua ya matengenezo hayo inalenga kupunguza kama si kumaliza tatizo la umeme, ambalo limekuwa likiigubika nchi hata kusababisha uzalishaji katika sekta mbalimbali nchini kudorora na hivyo kuathiri uchumi.

  Kipindi hiki cha mgawo huu wa nchi nzima ambao umegawanywa kwa makundi mawili, yale yanayoanza saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni na wa saa 12 jioni hadi saa 5 usiku, kitakuwa kigumu kwa kila Mtanzania anayetumia umeme.

  Nishati hiyo imekuwa ikitumika kuendeshea mitambo, kumulikia, kuongoza magari, kuhifadhi chakula na vitu vingine vinavyoharibika haraka na hata kupikia majumbani.

  Huu unaonekana kuwa mgawo mkubwa ambao athari zake pia ni kubwa, ingawa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilitoa hadhari mapema kwa taarifa na matangazo kwenye vyombo vya habari na kutoa mwanya kwa wananchi kujiandaa.

  Kitakuwa ni kipindi ambacho jenereta zitatumika sana na mazingira kuathirika kwa moshi lakini pia kelele mitaani, ili tu kunusuru uzalishaji angalau mdogo unaokuwapo na hivyo wananchi kujipatia riziki.


  Ni kipindi kibaya kwa wasio na uwezo wa kumiliki jenereta ambao watalazimika kufunga biashara zao kwa siku zote hizo mgawo utakapokuwa unaendelea na hivyo kuathirika kiuchumi.

  Kwa kuzingatia hali hiyo, tunapenda kuishauri Tanesco na hasa mafundi wake watakaokuwa wakijishughulisha na matengenezo hayo kufanya juhudi za usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba matengenezo hayo yanakamilika kwa muda uliopangwa.

  Tunasema ni vyema hilo likazingatiwa, kwani adha kama hii haitakiwi kuchukua muda mrefu, kwani ina athari kubwa kwa mtu mmoja mmoja na hata Taifa kwa jumla.

  Lakini pia wakati huu wa mgawo ni wa hatari kwa baadhi ya watu wenye nia mbaya kutumia kiza kufanya uhalifu, hivyo tunatoa mwito kwa Jeshi la Polisi pia kuwa makini na kuimarisha ulinzi katika maeneo ya makazi ya watu ili kukabiliana na uhalifu.

  Kwa kuwa matatizo haya ni ya kiufundi, ni vyema tukawaachia mafundi na wataalamu kulimaliza hilo, na hivyo wanasiasa waache kulibeba kisiasa na kupotosha wananchi na kuwaongezea machungu.
   
 2. VISIONEER

  VISIONEER Senior Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :a s 103: :a s 103: :a s 103: :a s 103: :a s 103: :a s 103: :a s 103: :a s 103:


   
Loading...