Hawa watu wanachekesha sana, huku wameambiwa wasihukumu wenzao na yule asiye na dhambi ndiye awe wa kwanza kurusha jiwe, huku hawaishi kutupa mawe.
Mimi atheist, siamini dini wala Mungu.
Kuna mama mmoja mlokole alikuwa karibu sana nami, siku moja aliniambia, mwanangu, najua wewe si mtu wa dini na wala huamini Mungu, lakini maisha yako unavyoishi, unawafanya hao wanaosema wanaamini Mungu waonekane kama wanafiki, halafu wewe usiyeamini Mungu ndiye unaishi kama unaamini Mungu.
Nikaukiza, kwa nini? Akasema nimekuona wewe ni mtu wa msaada sana, una moyo wa upendo sana, na hao wanaojiita walokole ukiwaomba msaada hawakusaidii, wanakwambia tu "tutakuombea kwa Mungu".
Nikamtania nikamwambia "Mama mimi siwezi kukuombea kwa Mungu kwa sababu siamini Mungu yupo, hivyo inabidi niifanye kqzi ya Mungu mimi mwenyewe, nikusaidie mwenyewe tu".
Mara nyingine hao walokole wanakuwa wakatili sana katikankutojali feelings za watu, wanajiona wao wanamjua zaidi Mungu.