Wabakwa hadi kufa!

babelwa1971

Member
Jun 27, 2007
11
7
Watoto wabakwa hadi kufa, mtuhumiwa mmoja mbaroni

Na Andrew Gasper, Singida

KIJIJI cha Ilongero kilichopo Wilaya ya Singida Vijijini, kimekumbwa na simanzi baada ya watoto wawili wa kike wa familia moja kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile hadi kufa.

Watoto hao, Twaiba (13) alikuwa anasoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Mrama iliyoko tarafa ya Ilongero, wilayani Singida na mdogo wake Zulfa(7) aliyekuwa akisoma wa shule ya chekechea, walikutwa na mkasa huo Jumapili iliyopita wakati wanamwagilia bustani yao ya mboga.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilongero, Issa Swedi, alisema tukio hilo lilitokea Jumapili kati ya saa 12:00 jioni na saa 2:00 usiku kwenye korogo la mto uliopo jirani na Shule ya Msingi ya Ilongero.

Swedi alisema kabla ya mauaji hayo, majira ya 10:00 jioni siku hiyo, watoto hao walitumwa na wazazi wao kwenda kumwagilia bustani hiyo lakini hawakurudu na kisha miili yao kukutwa kesho yale asubuhi ikiwa imetupwa kwenye shamba la viazi lililopo karibu na korongo hilo.

Alisema baada ya watoto hao kuchelewa kurudi nyumbani hadi saa moja jioni, wazazi wao walipata hofu wakatoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji, ambaye aliongozana nao hadi Kituo cha Polisi cha Ilongero kutoa taarifa juu ya kutoweka kwao.

Polisi waliwashauri warudi nyumbani na kwamba wasipoonekana warudi kituoni kesho yake asubuhi ili waanze kuwatafuta.

Asubuhi, wazazi pamoja na majirani zao walianza kuwatafuta na walipofika kwenye bustani ya baba yao mzee Athumani Jumanne walikokuwa wakimwagilia bustani, waliona alama za viatu aina ya kata mbuga na zingine za buti katika eneo hilo.

"Inaelekea watu hao waliwakamata watoto hao kwa nguvu na kuwabeba huku wakiwa wamewakaba koo na kwenda nao kwenye korogo refu la mto uliopo katribu na bustani hiyo," alisema Swedi.

Walipofuatilia nyayo za watu hao hadi kwenye korogo, waligundua kuwa watoto hao walifanyiwa unyama huo kutokana na kukuta viatu (kata mbuga) na suruali ambazo zilibainika kuwa ni mali ya mtu mmoja (jina tunalo) katika eneo hilo vikiwa vimetapakaa kinyesi na damu.

Wakiwa kwenye eneo, walipelekewa taarifa na wenzao kuwa miili ya watoto hao imeonekana kwenye shamba la viazi hatua kama 300 kutoka kwenye korongo hilo.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Dk Joyce Kishindo, alisema uchunguzi wao umebaini kuwa watoto hao ambao baba yao ni mlemavu wa miguu, wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri.

Mtoto mkubwa walipochunguzwa alibainika kuwa ameharibiwa vibaya sehemu zake zote mbili za siri na viganja vyake vya mikono pamoja na nguo zake zilikuwa na damu nyingi na kinyesi.

Kwa upande wa mdogo wake, alisema kuwa kutokana na udogo wa sehemu zake za siri walimwingia nyuma na kusababisha sehemu yake ya haja kubwa kutoa nje.

Dk Nicolaus Mabula kutoka Singiza mjini aliyeifanyia uchunguzi miili hiyo, alisema kifo Twaiba pia kilichangiwa na kukabwa koo, wakati mdogo inaonyesha kuwa aliinamishwa kichwa chini kwa muda mrefu hadi alipokuta kutokana na kukosa pumuzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Celina Kuluba alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba hadi juzi jioni walikuwa wanamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 33 (jina tunalo), mkazi wa Kijiji cha Mrama kuhusiana na mauji ya watoto hao.

Kamanda Kaluba, alisema jeshi hilo limeanzisha msako wa kumtafuta mtuhumiwa mwingine aliyetajwa kwa jina moja anayedaiwa kukimbia baada ya kufanya unyama huyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mama mmoja wa Kizungu anayefanya kazi za kujitolea katika Kituo cha Afya cha Ilongero akilia baada ya kushuhudia miili ya watoto hao, huku akilaani kitendo hicho kuwa ni cha kinyama.

Kutokana na tukio hilo, wakazi wa kijiji hicho walijazana kwenye chumba cha maiti katika kituo hicho, kufuatilia tukio hilo na kusababisha huduma kituoni hapo kusimama siku nzima.

Baadaye wanakijiji hao walikwenda kwenye Kituo Kidogo cha Polisi kwa lengo la kumuuua mtuhumiwa aliyekamatwa kwa kulishambulia gari ambalo lilikuwa limembeba kumpeleka kituoni hapo, lakini wote walitawanyika baada ya kutokea askari wa kituo hicho wakiwa na bunduki.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, suruali ya mtuhumiwa huyo ambayo ilikutwa katika eneo la tukio ikihusishwa na tukio hilo, ilitoweka na haijajulikana nani aliyeichukua.

Suruali hiyo ambayo inadaiwa kwamba ilikuwa imetapakaa kinyesi na damu haikuonekana baada ya mganga kutoka mjini Singida kuagiza ichukuliwe ili kuoainisha na vipimo vilivyochukuliwa kwa marehemu hao.
 
Watoto wabakwa hadi kufa, mtuhumiwa mmoja mbaroni [/B]

Mkuu karibu JF. Nadhani hii post ingewekwa kwenye habari na tuendelee na hii mada ya mkataba kwenye hii thread. Thanks na karibu tena JF.
 
Back
Top Bottom