Waathirika wa anguko la RA, EL, et al

Waathirika wa anguko la RA, EL, et al

Gurudumu

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2008
Posts
2,349
Reaction score
264
Yawezekana ama kweli wameanguka kisiasa au ni mchezo wa kuigiza. Vyovyote ilivyo, kuna mabadiliko katika maisha yao ya kisiasa na kiuchumi na uwezo wao wa kuwezesha mawakala wao wa kisiasa na kiuchumi.

Ni wazi, kuna wapambe wao wengi ndani ya chama tawala, upinzani na serikalini. Baadhi yao naamini walikuwa kipato chao pekee kinatokana na ukuwadi wao, uvuvuzela, kunusa taarifa na pengine kushulikia adui.

Baada ya mabadiliko yaliyofanywa ngazi ya juu ya ccm, naamini kwamba maisha na kipato cha hawa wapambe vitafifia. Baadhi wanaweza kuwa jobless (mfano, kuna watu tayari wameaga hapa janvini na wengine wanaonekana kubadili falsafa zao)

Je tunaweza kukisia ni watu wangapi wameathirika na mabadiliko haya na ni kwa kiwango gani? Je sasa nchi itatawalika?
 
iweke vizuri mbona hujamalizia kaka/dada?

Tayari mkuu, hii ilinitoroka nilikuwa naandika kwenye simu unajua tena vingine unabonyeza kwa bahati mbaya kabla hujamaliza. Ndiyo maana utaona zimetokea mbili, hiyo ya kwanza ilikuwa premature. Nadhani sasa iko sawa asante
 
Funika kombe mwanaharamu ajinafasi,ni namna ya tu ya kurudisha imani kwa wananchi,yes hao ni gamba lakini kuna magamba yaliyobaki mwili mzima ,gamba la usoni tu limejaribiwa kutolewa
 
Hawajaanguka. Wanajipanga kujibu mapigo. Subiri.
 
Yawezekana ama kweli wameanguka kisiasa au ni mchezo wa kuigiza. Vyovyote ilivyo, kuna mabadiliko katika maisha yao ya kisiasa na kiuchumi na uwezo wao wa kuwezesha mawakala wao wa kisiasa na kiuchumi.

Ni wazi, kuna wapambe wao wengi ndani ya chama tawala, upinzani na serikalini. Baadhi yao naamini walikuwa kipato chao pekee kinatokana na ukuwadi wao, uvuvuzela, kunusa taarifa na pengine kushulikia adui.

Baada ya mabadiliko yaliyofanywa ngazi ya juu ya ccm, naamini kwamba maisha na kipato cha hawa wapambe vitafifia. Baadhi wanaweza kuwa jobless (mfano, kuna watu tayari wameaga hapa janvini na wengine wanaonekana kubadili falsafa zao)

Je tunaweza kukisia ni watu wangapi wameathirika na mabadiliko haya na ni kwa kiwango gani? Je sasa nchi itatawalika?
Nadhani ungeuliza kama chama hicho kitatawalika bila michango yao haramu, kwani nchi ni kubwa mno na inaweza survive bila wao!
 
Ngoja nikuweke sawa kidogo kwani naona unavyosema wameanguka kumbe wamepanda chati zaidi kwani wengi waliowekwa pale ni kwa matakwa yao ilikutimiza kila jambo ambalo wao wanalihitaji mfano mzuri tu ni mtoto wa mzee aliyeanguka nafikiri mpaka hapo umenipata kumbuka wao ndio waliompa millioni mia nne amtoe william shelukindo na ili kumkomo zaid shelukindo dogo kapewe ile ile kamati ambayo shelukindo alikuwa anaongoza .badala ya kujivua gamba wamevaa gumu zaid tusubiri minyukano zaid kwani kauli ya professa mark mandosya kwa mwenyekiti kuwa anaomba wale wote wanotuhumiwa waziteuliwe tena kushika wadhifa wowote ndani ya CCM inaelekea ilawaudhi sana RA na rafiki yake mkubwa na je ccm bila RA na EL itaenda? kumbuka kauli ya sophia simba aliyowahi kutowa siku za nyuma akiwa anashika wadhifa moja ikulu kuwa mwanaume wa shoka anayeogopeka ndani ya CCM ni EL tu
 
napenda sana kuona mabadiliko na kama ni sanaa wala haitadumu kwani kuna walioongea wakimaanisha na kama ujuavyo hawatakaa meza moja na mafisadi kamwe! Bado mapema tusubili mwisho wa sanaa ccm unakaribia! Cha muhimu chadema washa moto zaidi hayo ni matunda yako
 
Nadhani ungeuliza kama chama hicho kitatawalika bila michango yao haramu, kwani nchi ni kubwa mno na inaweza survive bila wao!

Ukumbuke lakini kwamba mtu kama EL alikuwa anahonga in anticipation of political office. Uwezekano wake kupata madaraka umefutika therefore motivation ya kuhonga imekufa
 
Ilimradi wawe na pesa tu,mengine yatajipa.Japo hatuombei yatokee.

Mi nadhani pesa walikuwa wanapata kwa sababu walikuwa na madaraka waliyokuwa wanayatumia kujilimbikizia na kupata tenda. Pengine kitakachotokea ni waliopo kwenye hizo nafasi sasa nao kufanya ufisadi uleule lakini siyo hao waliotoka
 
Yawezekana ama kweli wameanguka kisiasa au ni mchezo wa kuigiza. Vyovyote ilivyo, kuna mabadiliko katika maisha yao ya kisiasa na kiuchumi na uwezo wao wa kuwezesha mawakala wao wa kisiasa na kiuchumi.
QUOTE]

... mchezo ule ule wa kuigiza. Walioenguliwa washitakiwe mahakamani kwa tuhuma zinazowakabili. Vinginevyo ni USANII ule ule, kama zilivyo tuhuma zile na kesi katika mambo ya EPA n.k.
Tuhuma za jinai zishughulikiwe kisheria. Vinginevyo, narudia, USDANII mtupu!
 
Mkuu hapo juu nakupa senksi! Kama hawana ushahidi basi hao watakaovuliwa nafasi zao washtaki pia.
 
Back
Top Bottom