Waasisi, viongozi wajiengua CUF Tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waasisi, viongozi wajiengua CUF Tarime

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 10, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, akisisitiza hatua ya kuendelea kuwatimua viongozi na wanachama wanaodaiwa kukiuka maadili na katiba ya chama, viongozi wengine watano ambao pia ni waasisi wa CUF Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, wamejiengua katika chama hicho.

  Kujiuzulu kwa viongozi hao kumekuja ikiwa ni wiki moja tu tangu viongozi wengine wa Wilaya ya Musoma Mjini watangaze kujiuzulu nyadhifa zao na kukihama chama hicho.

  Akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Musoma Mjini juzi, Mtatiro alisema kamwe CUF haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi yoyote atakayebainika kwenda kinyume cha maadili ya chama hicho.

  Alisema CUF inatarajia kuchukua nchi, hivyo haiwezi kufumbia macho viongozi wanaokiuka maadili na katiba ya chama kwa kuogopa nyadhifa za watu au uasisi wake ndani ya chama.

  Hata hivyo, wakati Mtatiro akitoa tamko hilo, viongozi wakuu wanne wa CUF wilayani Tarime na waasisi watatu wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao kisha kukihama chama hicho jana.

  Hao ni pamoja na aliyekuwa Katibu wa CUF Wilaya ya Tarime, Thomas Magero, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tarime, Dotto Chacha Wangwe ambaye ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (Chadema), marehemu Chacha Wangwe.

  Wengine ni Mwenyekiti wa Vijana Wilaya hiyo, Salma Salumu, Mwenyekiti wa Wazee Wilaya, Raurent Johanes, na muasisi wa kwanza wa CUF Wilaya ya Tarime, Idd Mohamed, pamoja na kada maarufu na mfadhili wa chama hicho Wilaya na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya, Jumanne Patroba.

  Akizungumza baada ya kutangaza kuchukua hatua hiyo mjini Tarime, Magero alisema hivi sasa CUF imekuwa ikiendeshwa kisultani kwa kuwafukuza watu hovyo kwa kuzuia wanachama kuhoji kuhusu mwenendo mzima wa chama.

  “Tumesikia Mtatiro yuko hapa mkoani eti kwa ziara za kuimarisha chama. Tumempelekea ujumbe asikanyage Tarime. Na kama akilazimisha, atakiona kama kichompata Mchungaji Mtikila alipokuja huku kwa kuwatukana akina mzee Mengi na Mbowe…Hapa tunataka siasa, si matusi kwa watu ama kuonyesha umwamba. Ukileta umwamba kwetu hapa Tarime, lazima pia uandae nyuzi za kutosha za kushonewa,” alisema Magero.

  Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wanawake, Wangwe alisema CUF hivi sasa imepoteza mwelekeo na kuwa chama cha viongozi badala ya wanachama.

  “Viongozi wa juu wa CUF sasa ni sawa ni miungu watu. Hawathamini wanachama na viongozi wa chini. Sasa wamefanya makao makuu kuwa sehemu ya genge la watu wachache ambao kamwe hawataki kuhojiwa hata kama wanatenda makosa…Ukithubutu kufanya hivyo tu kitakachokukumba ni kuhojiwa na kufukuzwa bila kufuata katiba,” alisema Wangwe.

  Muasisi wa CUF, Idd Juma, alisema kuanzia jana amejivua uanachama wa chama hicho.

  Aliifananisha CUF sawa na kijiwe cha kahawa kinachohusisha watu wasio na kazi.

  Wiki iliyopita, viongozi zaidi ya watano na waasisi zaidi ya nane wa CUF katika Wilaya za Musoma Mjini na Vijijini, walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiondoa ndani ya chama hicho na kufanya ofisi za Musoma Mjini kufungwa kwa kukosa uongozi.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  CUF ipo katika grave condition.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Ni kweli lakini kila chama cha Siasa hakikosi matatizo ndani yake katika kila chama cha Siasa kuna Mafisadi ndani yake ndio maana kuna tokea mgawanyiko ndani ya chama sisi binadamu hatuko sawa kimawazo ndio maana kuna tokea kila wakati migogoro ya Siasa kila sehemu ya hii dunia nakukubalia Mkuu unavyosema CUF inachungulia Kaburi.
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa kila chama kina matatizo yake, ila tatizo hili la CUF ni pigo takatifu lililowakumba baada ya kuonekana wanashirikiana na CCM kukandamiza wapinzani wengine.
  In short Cuf ni ADUI WA MAENDELEO.
  Die in peace CUF.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kwa ushauri wangu vyama vya Upinzani vingelikuwa na umoja haya matatizo yanayoletwa na chama kinachotawala yangelikwisha siku nyingi na haki ingeliweza kupatikana lakini bila ya kuwa na vyama vya upinzani kuwa na msimamo mmoja basi hata wakati wa uchaguzi unaokuja chama kinachotawala kitashinda tu kwa hali na mali. Kwa sababu zipo nyingi tu kwani kwenye vyama vya upinzani kuna mapungufu mengi tu ndio maana kila kunapotokea uchaguzi chama tawala lazima kishinde, vyama vya upinzani viwe na umoja na ukweli katika kuongoza upinzani sio kubabishwa na Vijipesa hakutakuwa na maendeleo yoyote katika nchi yetu namalizia hapo Mkuu.
   
 6. F

  Falconer JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Mutasema mengi kuhusu CUF lakini ukweli hamuujui. CUF ndio chama kilicho na sifa kamili za kichama katika nchi ya Tanzania. Cuf hatokufa kwani wao wameanza mapema kusafisha uchafu, uzembe na maadui ndani ya chama. Chadema munachelewa. MaCCM wamejaa ndani ya chadema. Sisi tumewajua na kabla kampeni za kura zinazokuja tutakuwa tunachama tayari kabisa kuchukua mamlaka endapo wananchi watakikabidhi. Tunaona maendeleo yanayoendelea zanzibar.It's just a matter of time. Haki sawa kwa kwote.
   
 7. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye red hawajakosea.. Katika matawi mengi ya CUF uswahilini lazima kuwe na kijiwe cha kahawa..! wanashinda hapo asubuhi mpaka ucku wanapoenda kulala.. tayari kwa kukutana kesho tena asubuhi..
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Hatusemi sisi kwa ushabiki wa chama cha chadema tunachosema ni ukweli mtupu ikiwa CUF kila kukicha Viongozi wake wanajiuzulu Je kwenye uchaguzi

  unaokuja hicho chama cha CUF kitaweza kupata ushindi Mkubwa katika nchi yetu hii? wewe umeona wapi chama cha upinzani katika hii dunia yetu kila kukicha magazeti yanaandika viongozi wake wa CUF wanajiuzulu eti kisha uchaguzi ujao

  Kishinde na kuongoza nchi? Labda huko Visiwa vya Pemba na Unguja tu lakini si kwa Tanzania nzima CUF haijawa na uwezo wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu na kuongoza nchi sio kitu rahisi Mkuu namalizia hivyo..
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280

  Samahani kidogo , how old are you my friend?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona Mkuu Falconer kakukimbia kashindwa kukujibu labda umemuuliza kwa lugha ya kiingereza ungelimuuliza hivi mkuu Falconer una umri gani? ninafikiri angelikujibu haraka.
   
 11. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #11
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wanaojitangaza wamejitoa CUF wanahangaika bure,alafu mbona wote wanapojitangaza kwenye media sentesi zao ni zile zile tatu ikiwemo chama kinendeshwa kisultani.Hizi ndo sentesi alizitamka hamad rashid kwa mara ya kwanaza inaonekana wazi ni watu wanaolishwa maneno na hamad rashidi na kupewa pesa za ccm ili kuivuruga CUF.Hawa jamaa wanahangaika bure kwa kutunga habari za uongo kila siku na kuwanunua watz na kuwaahid vyeo kwenye chama cha hamad rshid kiitwacho ALLIENCE FOR DESTABILIZING CUF-ADC.Nawataadhaharisha kwamba CCM weshaanza kukata tamaa kumfadhili hamad rshid ili kuivuruga cuf hivyo hizo pes mnazoongwa ili kuuza utu wenu muda si mrefu zitaisha,hta pesa ya chai mnayopewa kilasiku hamtaiona tena na CUF mtaiona ikiendelea kushamir.NJAA MBAYA SANA AISEE.MTAKUFA KISIASA NA KUIACHA CUF IMARA.
   
 12. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #12
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we mzizi mkavu uliooza hamad rshid kakuhonga shs ngapi ama ndo amekuahid kuwa mwandish wa kudumu kwa magazeti yake yanyoelekea kufa ya ANIKA UKWELI na MWANA AFRIKA
   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Mkuu, huyu mtu ilikua ni lazima akimbie.
  CUF ni maiti iliyooza, 'eh Lipumba pokea mzoga huu kauzike mbali huko ':whoo:
   
 14. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #14
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waliojiondoa ndo wako kwenye grave coz hamd rshid kawaburuza kama mazuzu anwapeleka wasikokujua ila anajua yeye na ccm tu.wao wanafuata pesa ila lazima pesa hizo za kuhongwa ziwatokee puani,pesa za ccm haziendi bure lazima uwe mtumwa wao kupitia ALLIENCE FOR DESTABILING CUF-ADC
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mangi Masta mbona unakuja juu kama mawimbi ya bahari? Huutaki ukweli wa mambo? Yakhe? Waswahil husema ukitaka kuung'owa Mti kata mizizi yake Mkuu Mzee

  Maalim Seif kafanya haraka au makosa kumfukuza Mzee Hamadi Rashid na wenzake angelimuonya tu sio kumfukuza Kazi Muanzilishi mwenzake wa chama cha CUf hayo ni makosa ya Maalim Seif kafanya atakuja juta baadae kwanini alifanya hayo makosa ninaishia hapo kwa leo nakusikilza wewe unasemaje Mangi Masta Mchaga wa CUF.
   
 16. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Cuf ife mara ngapi??? Punde CUF ilipoanza kulala under the same roof in the same bed na CCM tena bila nguo ndo imezikwa pale numbwi tena kwa kutoswa kwenye kina kirefu baada ya kufungiwa jiwe la kusagia.
  Maendeleo ya Zenji ni hizo biashara za bidhaa used mnazofanya??
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hata maiti daudi mchambuzi inaongea rip..daudi
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Yani kuanzia hamad rashid mpaka wewe wote ni sehemu ya mzoga huu uliokufa kwa sumu iliyotegeshwa kwenye kipande cha nyama.
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Rip daudi mchambuzi msalamie HR
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Kesho Lipumba akifika kuhani msiba huu wa marehemu CUF huenda maiti ikachana sanda, ombeni sana wafiwa.
   
Loading...