Waasi watatu wa ADF wanaodaiwa kuwa raia wa Tanzania wakamatwa Congo

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Jeshi la taifa la Kongo FARDC limetangaza kuwakamata raia watatu wa Tanzania ambao ni waasi wa ADF waliosajiriwa wilayani Beni mashariki mwa Kongo.

Raia hao wa Tanzania, walikamatwa Jumapili hii, Februari 6, 2022 wakati wa doria zilizofanywa na askari wa Kongo katika bonde la Mwalika, katika eneo la Beni Kivu Kaskazini.

Kulingana na taarifa ya msemaji wa secteur (tarafa) ya Sokola 1 Kivu Kaskazini, Kapteni Athony Mwalushayi ; waasi hao wamekiri kuwa walisajiriwa kwa nia mbaya na raia wa Kongo ambaye aliwadanganya kwamba watafanya kazi katika migodi ya dhahabu, lakini wakajikuta katika kikundi cha waasi wa ADF.

Akizungumza na BBC, Kapteni Athony Mwalushayi amesema, waasi hao raia wa Tanzania wako sasa mikononi mwa idara husika ili waandelee kuchunguzwa.

Mnamo Januari 28, katika eneo hilo hilo la Beni, FARDC pia lilimkamata muasi wa ADF, raia wa Kenya, Salim Muhammad, ambaye alikuwa anasambaza video za ukatili.

Januari 9, 2022, Benjamin Kisokeranio, mkuu wa tawi la ADF la muasi Jamil Mukulu, alikamatwa Uvira katika jimbo la Kivu Kusini.

NAIOMBA SERIKALI KUZICHUNGUZA KAMPUNI ZA ULINZI BINAFSI MAANA NANUSA UHUSIKA WAO WA KUWAPELEKA VIJANA HAWA NJE KWA USHAWISHI WA KAZI ZA ULINZI KUMBE KUJIUNGA MAKUNDI HARAMU
 
Kiongozi mkuu wa waasi wa ADF alikamatwa Gongolamboto Dar es salaam ambako alikuwa akiishi kificho akijifanya mtu wa kigoma akimiliki nyumba na biashara

JWTZ walimdaka baada ya waasi wa ADF kuua askari wa JWTZ walioko kongo

Akakabidhiwa kwa serikali ya Uganda sababu alikuwa akitumia majeshi yake ya waasi kusumbua Hakuuawa uganda?
 
Wanakuja kupigana na nani?
Amewakosea nini?
Maana hawa wengi watakuja kuonea raia wasio na hatia tu.
Halafu umejuaje kuwa wameenda kote huko kufanya mafunzo?Au una taarifa na wanaofanya hizo connections?Kama unazo inteligensia yetu inakwama wapi?Au nawe ni mmoja wao?Kama wewe ni mmoja wa intelligentsia yetu,basi umeonesha udhaifu kufichua siri hiyo kwenye media.
Labad walienda mafunzo, wengne wapo Msumbiji, wengne Somalia, Afghanistan nk siku wakirudi bongo kitawaka!
 
Back
Top Bottom