Waasi wanapatikanaje?

Mamzalendo

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,670
558
Ndugu zangu nimekaa sana nikawaza yote haya natafakari tu eti waasi kama wa libya na kwingine wanatengenezwa au wanatokeaje? au ni watu wa aina gani au ni kina nani?na je hili huwa ni jambo la ghafula au kukurupuka? na je ni muda gani unahitajika kuwapata? na je Serikali ya Tanzania inaweza kuwa inaandaa waasi bila kujua? embu nisaidieni mawazo ya hawa wanatokeaje?
 
Uvumilivu ukiisha waasi wanpatikana kikubwa ni Tolerance ikiisha mambo huwa mengine!

naweza kukubaliana na wewe lakini je ni uvumilivu upi ukiisha wa kuibiwa rasilimali? maisha magumu kwa kukosa basic need? kutukanwa na kudhalilishwa? ukiukaji wa sheria? au ni uvumilivu wa nini ukiisha? na inamaana mpaka uvumilivu wa wananchi uishe viongozi wanakuwa hawaoni au n vipofu?
 
Kungekuwa na wahasi wakukodishwa tungechanga hata humu JF tuwakodishe ili magamba tuwaonyeshe cha moto
 
Kumbe TZ uvumilivu bado haujaisha

Ni uvumilivu haujaisha au hajatokea mtu wa kulianzisha?mi najiuliza ni nini kitafanya uvumilivu uishe?halafu hapa kuna jambo lingine ni uvumilivu haujaisha au ni woga?
 
Kungekuwa na wahasi wakukodishwa tungechanga hata humu JF tuwakodishe ili magamba tuwaonyeshe cha moto

unajua inawezekana kabisa wapo wa kukodi lakini je hao unaohitaji kuwakomboa wanaona umuhimu wa kukombolewa?hivi jf kuna waasi au hamna?unajua huwezi kumpa uhuru mtu ambaye haelewi kama anahitaji uhuru?
 
Ningekwambia lakini nawaogopa
Tunasimamia
Isipite
Serikali
Safi
 
Serikali inapowakusanya kodi halafu haileti maendeleo. Inapowadhulumu wananchi haki zao bila huruma. Inapowavamia, kuwapiga, kuwaweka ndani na kuwabambika kesi wakati wakihoji haki zao. Wananchi wanafika mahali wanachoka, wanakuwa sugu na wanaamua kupambana! Hapo ndipo wanaitwa waasi!
 
Aha kumbe sasa ni nani wanawapa wananchi silaha kama wakihitaji au msaada wa kiufundi kwa ajili ya mapambano je? je wananchi ambao wanaasi wanaweza pia kuwepo katika hiyo hiyo serikali inayohitaji kubadilishwa?
 
Viongozi wa vyama vya siasa, wanaharakati na wanamageuzi huwa wana"take advantage" ya kuwaongoza wananchi! Wananchi wanakuwa individual na hao watu wanawa organise na kuwaongoza hadi kufikia malengo. Lazima kuwe na waongozaji, jambo ambalo nadhan sisi hatujalipata. Wanatakiwa kuwa jasiri na wako tayari kujitoa. Hapa kwetu nadhani wamekosa ujasiri na utayari wa kujitoa mhanga. Kwa kiwango ambacho wananchi wamechoshwa na uvumilivu, akitokea tu, na uasi unaanza!
 
NI sawa kabisa lakini kwa nini tumekosa viongozi kwani mkuu ni kwa sababu wamekosa ujasiri au wanahongeka kirahisi na hizi shida za dunia zinawazonga sana kiasi kwamba wakitafakari kujitoa mhanga wanashindwa mfano mimi ni mama wa watoto wawili tena wadogo na hela za matunzo sina kivile je nikijitoa mhanga kweli watoto wangu wataishia wapi?kitu cha kwanza nafikiri waasi wanachofanya nikujiwekea ulinzi wa kutosha kwa sababu unapoanzisha vuguvugu siku zote kutakuwa na majibu je umejiandaaje kwa majibu iwapo itashindikana in first attempt? mi nafikiri walibya this was not their first trial?
 
hivi kuwa na waasi katika nchi kuna ubaya? nini faida zao na hasara kwa nchi hapa naulizia long term and short term advantage and disadvantages. tukizijua zitatusaidia either kutokomeza dalili zote za uasi au kuzisupport na pia is it real worthy the risk?
 
Umetumwa kwamba tafuta kama kuna watu wanamawazo ya kuiasi nchi na serikali na mkuu wakitengo.Nimesikia ofisini wakati mmapanga mchakato,dah na mimi pia am a muasi tangia zamani.
 
Umetumwa kwamba tafuta kama kuna watu wanamawazo ya kuiasi nchi na serikali na mkuu wakitengo.Nimesikia ofisini wakati mmapanga mchakato,dah na mimi pia am a muasi tangia zamani.

ha ha ha ha,is that all u can think eh?ndio nimetumwa na mkuu wa kitengo unajua ni nani ni akili yangu?maana limwili lote linaongozwa na akili!
 
Mamzalendo! We kuwa kimya kidogo hapa Tanzania tunayosema kisiwa cha AMANI siku moja utasikia waasi unaowaulizia wamechafukwa na Mioyo na wanataka kukomboa NCHI kwenye mikono ya mafisadi na hao utasikia WAASI WA TANZANIA wamechafukwa na mioyo na wanataka uhuru kamili ama katiba mpya. Na hapo ndiyo utajua Waasi wametokea wapi na faida yake ni nini. Tuombe MUNGU a2pe uzima tu.
 
kwa mawazo ya haraka haraka na kwa kufikirika uasi unawezekana lakini kwa tz hii labda baadae sana maana wananchi wake ni waoga kupita maelezo haki zao hawazi fahamu
 
ahsante mkuu ngoja nisubirie lakini kwani wanadalili yakutokea cku za karibu nisijekaa sana nikisubr,
 
kwa mawazo ya haraka haraka na kwa kufikirika uasi unawezekana lakini kwa tz hii labda baadae sana maana wananchi wake ni waoga kupita maelezo haki zao hawazi fahamu

nakubaliana na wewe hatujui haki ze2 kabisa na hapa ndio serikali inapo take a good advantage bt pole pole ndio mwendo,
 
Back
Top Bottom