Waanguka na ungo katika kituo cha polisi manyoni

Waanguka na ungo katika kituo cha polisi manyoni

Jidu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
1,232
Reaction score
757
uchawi 1.jpg
wizard 2.jpg

Jeshi la polisi wilaya ya Monyoni mkoani Singida
linawashikilia vijana watatu waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ungo kutoka katika
kijiji cha
Kinika kata ya Mkwese wilayani Manyoni kuelekea mkoani Mbeya na kuanguka karibu na kituo hicho.

hii kwa hisani ya Kapinga blog
 
Wameanguka au wameenda wenyewe na miguu yao?
 
Huyo mwenye kitumbo cha unyafuzi nae ni kijana?
Hii biashara ingerasimishwa fast jet wangedoda!
 
Si wanasemaga kuwa huwa wanasafiri wakiwa naked? mbona hao wamejisitiri?
 
Kumbe ndege zao nao huwa zinapata hitilafu kama hizi nyingine.Inaonekana rubani alifanya kutua kwa dharula!
 
View attachment 81710
View attachment 81711

Jeshi la polisi wilaya ya Monyoni mkoani Singida
linawashikilia vijana watatu waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ungo kutoka katika
kijiji cha
Kinika kata ya Mkwese wilayani Manyoni kuelekea mkoani Mbeya na kuanguka karibu na kituo hicho.

hii kwa hisani ya Kapinga blog

Spaceship yao ilikuwa inaenda 300km per hour kama sijasahau na kajamaa kalipoangalia nyuma tu wakala mweleka. Hizo vyombo siziamini kiusalama, Naamini chombo kimoja tu ambacho ni Yesu Kristo, yaani hapo hata akikwambia panda kwenye chombo kizee utafika bila shida hata uangalie nyuma, mbele, juu au chini yaani no problem kabisa na speed ni hakuna spea.
 
Damu ya Yesu inanena mema lazima itakuw kuna watu walifanya maombi usiku maeneo hayo wakapita ndo matokeo ya kuanguaka
 
Pumba pumba urongo urongo urongo ad infinitum. Mbona hii picha ilishawekwa jamvini zaidi ya mara kumi! Ina maana watu hawana cha kutundika bali ujinga ujinga mtupu? Shame on you!
 
Hivi mbona picha za nyungo zenyewe wanazotumia huwa hatuzioni? Ni ungo huu huu tunaoujua au wenyewe ni spesheli?
 
Unidentified object hahaha. Camera huwa haiinasi ila subiri tu camera ya Mungu siku hiyo tutaonyeshwa
 
Hizi ni dalili za taifa lililokosa hofu ya mungu.
 
mmmh,.walikuta hapo kituoni ni noma kwa nguvu iliyopo hapo, ila huu usafiri wangeuweka wazi yaan mtu ukitaka kwenda uk, tandahimba, yaan popote pale ni chap.. mi nlijuaga wanakua uchi kumbe wanavaa kabisaa,.waziri anayehusika na usafiri alichek na hili...
 
Back
Top Bottom