Waandishi wawili wa habari waachiwa huru Italia


Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
5,624
Likes
6,192
Points
280
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
5,624 6,192 280
Mahakama moja nchini Italia imewaachia huru waandishi wawili wa habari za uchunguzi waliokuwa wakishitakiwa kwa kuchapisha nyaraka za siri zilizoibwa zinazohusiana na kashfa ya rushwa katika makao makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican.

Waandishi hao wawili Emiliano Fittipaldi na Gianluigi Nuzzi, walikuwa wakikabiliwa na kifungo cha hadi miaka minane gerezani kwa kuchapisha vitabu viwili vinavyohusiana na nyaraka hizo za siri.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo walitiwa hatiani kwa kuhusika na kuvuja kwa nyaraka hizo za siri ambao ni pamoja na Padri mmoja mhispania Lucio Vallejo Balda aliyehukumiwa kwenda jela miezi 18 na afisa mmoja wa masuala ya mahusiano ya umma nchini Italia Francesca Chaouqui ambaye amehukumiwa kifungo cha nje kwa kipindi cha miezi kumi.

Chanzo: DW
 

Forum statistics

Threads 1,235,344
Members 474,524
Posts 29,219,430