Waandishi washambuliwa Ngorongoro huku Mbunge akihusishwa katika tukio hilo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
431
626
Mkurugenzi wa Gazeti la Jamvi la Habari Habibu Mchange na waandishi wa habari wapatao sita wamevamiwa na kundi la Vijana wa kimasai na kujeruhiwa vibaya walipokuwa wakifanya mahojiano na wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Baadhi ya waandishi wa habari waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo katika kijiji cha Endureni wilayani Ngorongoro ni Denis Msacky, Ferdinand Shayo. Akizungumza na Jambo TV ndugu Habib Mchange amemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Mhe. Emanuel Oleshangai kuratibu mashambulizi hayo ambapo.

Jambo TV imefanikiwa kuzungumza na Mbunge Oleshangai kuhusiana na tuhuma za kuratibu mashambulizi hayo kwa wanahabari ambapo amekanusha vikali kuhusika na uhalifu huo huku akisema hana sababu ya kuratibu mashambulizi kwa wanahabari hao.

Oleshangai amesema Endureni ni kijijini kwake na aliwaona hao waandishi wa habari wakiwa mnadani wakiwakusanya watu kwa ajili ya kuzungumza nao huku yeye na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa CCM wakila nyama na baadae akaondoka kurejea nyumbani kwake.

Oleshangai amesema alipofika nyumbani kwake ndio alipata taarifa ya kutokea kwa fujo hizo hivyo hahusiki nazo.


============

Ngorongoro.JPG
 
Mkurugenzi wa Gazeti la Jamvi la Habari Habibu Mchange na waandishi wa habari wapatao sita wamevamiwa na kundi la Vijana wa kimasai na kujeruhiwa vibaya walipokuwa ...
Habari Yako ni nzuri ila weka paragraphs
 
Ee Mungu turehemu waja wako tunakusihi, yote haya ni matokeo ya kukuasi wewe kwa tamaa za kitambo tu za kuwaza anasa na mali za dunia hii na kupelekea mafarakano miongoni mwetu.
 
Zaidi ya vijana 200 wa jamii ya kimasai (morani) eneo la Enduleni, Wilaya ya Ngorongoro, Mkoani Arusha wamewavamia na kuwajeruhi waandishi wa habari na mkalimani aliyeambatana nao.

Waandishi hao wamekuwa wilayani humo wakipata uelewa wa kwa nini Serikali inashauri wahame kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi hiyo kwenda Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Waandishi waliojeruhiwa ni pamoja na Ferdinand Shayo wa ITV, Denis Msacky (mwandishi wa kujitegemea), Habib Mchange (Jamvi la Habari), mkazi mwingine wa Ngorongoro, Lengai Ngoishie pamoja na mwandishi wa habari hizi.

Vijana hao walikuwa wamebeba mapanga, mikuki, sime na mishale.

Wakati tukio hili linatokea Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Oleshangai, alikuwepo eneo la tukio na baada ya vijana hao kuvamia na kujeruji alioondoka eneo hilo.

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala amesema anatuma askari kufika eneo hilo

Source Mwananchi
 
Waandishi wa gazeti mwananchi lilipoteza uadilifu na kuungana na mafisadi wamevamiwa na kujeruhiwa na Wananchi wenye hasira kali ngorongoro

Haijulikani walikuwa wanawahoji vitu gani

Ikumbukwe wananchi wa ngorongoro wapo kwenye mateso makubwa baada ya kufukuzwa kwenye nchi yao ya asili na ardhi kukabidhiwa waarabu

Tunapoenda wananchi wataacha kulalamika watakuwa wanajilinda wenyewe
 
Zamani waandishi wa habari walikuwa marafiki wa umma. Watu wakiwa na matatizo, wakija waandishi wa habari, waathirika walijua kuwa matatizo yao yatafahamika.

Siku hizi ni tofauti. Hakuna wanahabari, badala yake kuna waganga njaa kupitia habari. Hao wanaojiita wanahabari, wanaweza kwenda kwenye tukio, wanawahoji wahusika, lakini kitakachotoka kwenye vyombo vya habari ni tofauti kabisa na kile walichonena waliohojiwa. Hali hiyo, nadhani inachangia pia wanahabari kuonekana ni maadui wa umma.
 
Back
Top Bottom