Waandishi wa Mwananchi wafukuzwa msafara wa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa Mwananchi wafukuzwa msafara wa JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 26, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na Kizitto Noya, Mwananchi

  WAANDISHI wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) wamefukuzwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete.

  Ray Naluyaga, ambaye anaandikia gazeti la The Citizen, na Frederick Katulanda wa Mwananchi, walifukuzwa kwa nyakati tofauti kwenye kampeni zilizofanywa katika mikoa ya Geita na Kagera.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alikanusha chama hicho kutimua waandishi kwenye msafara wa Kikwete akisema anaamini waandishi hao wamefukuzwa na mtu aliyemwita kuwa ni mhuni na si CCM kama chama.

  Waandishi hao walifukuzwa kutokana na chama hicho kueleza kutofurahishwa na habari iliyoripotiwa na gazeti hili juzi ikiwa na kichwa kisemacho "JK ahaha kunusuru mpasuko CCM".

  Akielezea mkasa huo, Naluyaga alisema alifukuzwa Ikulu saa 1:30 asubuhi jana mjini Bukoba ambako msafara wa mgombea huyo ulipokuwa ukijiandaa kwa safari ya kuelekea Wilaya ya Misenyi.

  "Mimi nilifika Ikulu leo (jana) saa1:30 na kukuta waandishi wenzangu wakiwa wamevalia jaketi zilizoandikwa 'Kikwete Press 2010," alisema Naluyaga na kuongeza:

  "Nikaenda kuripoti kwa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais) Salva Rweyemamu, lakini yeye akaniambia nimsubiri (mratibu wa habari wa timu ya Kikwete) Muhingo (Rweyemamu) kwa kuwa yeye (Salva) ni mshauri tu wa masuala ya habari."

  Naluyaga alisema baada ya Muhingo, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya New Habari Corporation ambaye sasa anafanya uratibu wa kampeni za urais za CCM, kuwasili alimtaka aendelee kusubiri kwa kuwa jina lake limepelekwa Ikulu kujadiliwa kwanza.

  Muhingo, ambaye kampuni yake huzalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na The African, pia alikuwepo kwenye timu ya kampeni ya Kikwete mwaka 2005 wakati mwenyekiti huyo wa CCM akiwania kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza.

  Katika kampeni za mwaka 2005, Muhingo alimfukuza mwandishi wa Mwananchi baada ya kutofurahishwa na habari alizokuwa akiandika.

  "Msafara unaanza na yeye (Muhingo) akaendelea kuniambia subiri; subiri; subiri. Baadaye akasema suala langu ni gumu hivyo siwezi kwenda na msafara wao," alisema Naluyaga na kubainisha kuwa ndani ya Ikulu hiyo kulikuwa na makada kadhaa wa CCM, akiwamo mwenyekiti Kikwete, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Kagasheki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Deodorous Kamala.

  Alisema ingawa Muhingo hakumweleza sababu za jina lake kupelekwa Ikulu kujadiliwa, makada mbalimbali wa CCM walimwambia kuwa tatizo ilikuwa habari iliyoripotiwa na gazeti hili juzi.

  "Wengine walisema kampuni ya Mwananchi ni hatari sana kwa sababu ni kampuni binafsi inafanya kazi zake bila upendeleo. Lakini kama issue (suala) ni kampuni binafsi, mbona kulikuwa na waandishi wengi wa kampuni binafsi," alihoji Naluyaga.

  Lakini jana Muhingo alikanusha kumfukuza Naluyaga akisema "Atakuwa amekwambia uongo. Kwa nini nimfukuze mwandishi? After all (zaidi ya yote) tunahitaji coverage (taarifa zitoke)".

  Muhingo alieleza kuwa ni kweli alimwacha Naluyaga Ikulu ndogo ya mjini Bukoba, lakini si kwa sababu hakutaka aripoti matukio ya kampeni za CCM bali ni kwa sababu ya uhaba wa magari ya kusafiria.

  "Tulitegemea tuwe na magari mawili ya waandishi, lakini tukapata moja tu na mimi nilikuwa na waandishi kumi niliotoka nao Dar es Salaam sasa katika mazingira hayo, unamchukua aliyeanzia Bukoba ama, unaendelea na wale ulioanza nao Dar es Salaam,"alihoji Muhingo.

  Awali Katulanda alisema alidokezwa suala la kufukuzwa kwa waandishi wa Mwananchi juzi na Muhingo majira ya saa 4:00 asubuhi wakati Kikwete alipokuwa anahutubia kwenye Uwanja wa Katoro mjini Geita.

  Alisema siku hiyo mara baada ya Kikwete kupanda jukwaani na kuanza kuhutubia, aliitwa na Muhingo, anayeshughulikia mambo ya habari.

  "Akaniambia twende huku. Nikamuuliza wapi? Akasema twende. Akanipeleka mahala ambako nisingeweza kumsikiliza Kikwete anavyozungumza na kuniuliza:
  "Kwa nini umeandika habari hiyo? Wewe huoni unatuharibia? Kuna vitu vingi vya kuandika ikiwamo wilaya mpya kuanzishwa mwezi Januari, lakini bado uliona hiyo ndio habari. Mimi ni mtu muhimu hata huko Mwananchi; jina langu limo kwenye usajili wa gazeti lenu na nitakufukuza kwenye msafara wetu," alieleza Katulanda akimnukuu Muhingo.

  Katulanda alisema maswali hayo yaliibua mvutano kati yake na Muhingo hasa pale aliposisitiza kuwa anaamini alichoandika ndicho wananchi wanachopaswa kujua.

  Katulanda alisema kuwa Muhingo alidai habari iliyoripotiwa na gazeti hili juzi kwamba Kikwete alitumia mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la Buchosa kutuliza wimbi la mpasuko unaoonekana kukikumba chama hicho tawala baada ya kumalizika kwa kura za maoni za kuteua wagombea ubunge na udiwani zilizosababisha wanachama wengi kukimbilia upinzani.

  Akizungumza na Mwananchi, Makamba alisema: "Ili uamuzi uwe wa chama lazima ufikiwe na Kamati Kuu, Nec au uamuzi afanye katibu mkuu. Vikao hivi havikufanyika kokote na mimi (katibu mkuu) sijaagiza mtu awafukuze waandishi. Fuatilia vizuri habari yako, utagundua tu kwamba yupo mhuni amekosana nao akaamua kuwafukuza."

  Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MCL, Theophil Makunga alieleza kusikitishwa na kitendo cha mratibu wa habari wa kampeni za CCM kuwafukuza waandishi wake, akisema kuwa kampuni haikutegemea kitendo hicho kufanywa na CCM.

  "Sishangai sana kwani hata mwaka 2005 walimfukuza mwandishi wetu maeneo ya Ngara. Lakini nasikitika na sikutegemea hilo kufanywa na chama makini kama CCM," alisema Makunga na kuongeza.

  "Hata hivyo bado ninawahakikishia wasomaji wa magazeti yetu kwamba tutafanya kila liwezekanalo kuwaletea habari zote zinazohusu kampeni zote, zikiwemo kampeni za CCM," alisema. MCL inachapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

  Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, John Chiligati alisema hana taarifa ya tukio hilo na akalitaka gazeti hili liwasiliane na mratibu wa kampeni za chama hicho, Abdurhaman Kinana au Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kwa maelezo zaidi.

  Jana kutwa nzima, Kinana hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

  Habari inayoelezwa kulalamikiwa na CCM iliripotiwa na gazeti hili juzi kwamba Kikwete alitumia jukwaa la kampeni kunusuru mpasuko wa wanachama wanaohamia vyama vya upinzani kupinga matokeo ya kura za maoni za kupata wagombea ubunge na udiwani, akiwataka waige mfano wake wa uvumilivu.

  Kikwete alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Tarafa ya Nyehunge.

  Alisema wanachama walioshindwa hawana budi kutulia na kuwapigia kampeni wagombea waliopita kupeperusha bendera ya chama hicho ili kishinde uchaguzi.

  Alikuwa ameshtushwa na kitendo cha mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni kutoonekana katika msafara ulioenda kumlaki alipowasili na pia kutoonekana kwenye mkutano wa hadhara kwenye jimbo hilo ambalo makada wanne wa CCM wamefungua kesi kumpinga mgombea wa CCM, Dk Charles Tizeba.

  Kikwete alisema kuwa walioshindwa hawana budi kuiga mfano wake kwa kuwa baada ya kushindwa na Benjamin Mkapa mwaka 1995 kuwania tiketi ya CCM ya kugombea urais, alivumilia na mwaka 2005 akapata nafasi hiyo kwa ushindi wa kishindo.

  Kikwete aliongoza awamu ya kwanza ya kura za maoni za kutafuta mgombea urais wa CCM mwaka 1995, lakini katika awamu ya pili aliangushwa na Benjamin Mkapa ambaye baadaye alishinda uchaguzi na kuwa rais wa serikali ya awamu ya tatu.

  Kikwete aliingia tena kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta urais kwa tiketi ya CCM na kushinda kwa kishindo kwenye kura za maoni za chama hicho mwaka 2005.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  tatizo hakuwa na jaket limeandikwa ''kikwete pres 2010''

  hii ndo tanzania yaani basi tu halafu kuna waandish wengine wa habari wanavaa hadi zile tisheti za kijani

  pole mwanadishi wa mwananchi
   
 3. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Nawapongeza waandishi wote waliofukuzwa wameonyesha umakini wao kazini, nimeona na leo ameandika magari ya serikali kutumika. Safi sana Mwananchi na waandishi wako.
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hayo yaliwahi kumkuta Mwandishi wa Gazeti la Rai na Mtanzania (Kabla ya kuchukuliwa na RA) ambapo mwandishi Keny Manara alitimuliwa katika msafara
   
 5. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapo patamu....
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,393
  Likes Received: 3,143
  Trophy Points: 280
  WENZAKE WALIPATA POSHO ILI WAMTANGAZE KJ MGONGONI MWAO LAKINI WAO MWANANCHI WALIKAIDI NA HIYO NDIYO ADHABU YA KJ...........Jamani nasita kumwita jk kwani hafikii hata robo ya nyerere
   
 7. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,185
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Wanadhani kuandika kwenu ndo kulisababisha kishindo cha mweleka nini?
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,955
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Nijuwavyo mimi KJ maanake Kubwa Jinga!!!
   
 9. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilidhani waandishi wa habari wameukuzwa,kumbe ni waripoti wa vijarida vya udaku!Hata hivyo hao jamaa ni wakenya katika uchaguzi wetu inawagusa nini?Mbona wao kule wamechinjana wala hatukuwaingilia!Na bado tutawafukuza nchini!
   
 10. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,559
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Waandishi waliopo kwenye msafara wa JK,WAMEVAA FULANA,KOFIA zenye Chata ya "Press Kikiwete 2010" huku wakiwa na note book,pen zenye nembo hizo.

  Baadhi yao niliowaona ni
  1.Vedasto Msungu,ITV
  2.Mcharo Mrutu, Channel ten
  3.Gabriery Zakaria,TBC
  4.Irene Mark,Tanzania Daima.
  5.John Daniel ,Majira
  6.Mgaya Kingomba,Habari Leo
  7.
  Wengine siwajui kwa majina
   
Loading...