Waandishi Wa Habari Za Michezo Kuweni Wazalendo

motonkafu

JF-Expert Member
Dec 2, 2015
1,019
703
Nimesikiliza na kusoma habari nyingi za michezo hasa baada ya Taifa Stars kuikosakosa Algeria kule kaskazini, kilichonikera ni jinsi watu wanavoandika na kukomenti vibaya kuhusu timu yetu ya taifa azi ifu wao ni waarabu wa Algeria.

Nikajiuliza kama wabongo wenye timu wanakomenti pumba izi, je Waalgeria waliojikwamua na kipigo cha Stars kwa wao kushinda waseme nini, maana yake dharau zote tumemaliza sisi wenye timu.

Mtangazaji mmoja ametangaza bila ya aibu;
"Na huu ni mwendelezo wa ubabe wa Algeria kwa Taifa Stars......"
Akakumbushia matokeo ya ile mechi ya mwaka 2015, nikaujiuliza kama kuna haja ya kuunganisha matokeo ya 2015 na ya sasa, hasa ukizingatia matokeo yale hayakua mazuri sana. Nikajisemea rohoni kwamba kama huyu ni Mtanzania na shabiki wa mpira kwanini asiripoti hivi;
"Na huu ni mwendelezo wa Algeria kujiokoa na kichapo cha taifa stars, kwa kushinda wao vinginevyo Taifa Stars isingesita kuwaadhibu wakiwa nyumbani kwao"
Nafikiri hii ingekaa kiTanzania zaidi kwani "mwenda kwao si mtoro bali aisifuye mvua imemnyea"

Hapa jf mdau mmoja aliandika; "Taifa stars ni kichwa cha wendawazimu". Nikastuka na kutikisa mashavu, nikashamshangaa huyu kama mTanzania na hii timu ya taifa la Tanzania, maana yake yeye ndo anaimiliki, kwa iyo kusema 'ni kichwa cha wendawazimu' na yeye akiwa ni mmoja wa wamiliki basi hakuna shaka na yeye ni mwendawazimu pia.

Kwa uchambuzi wa kisoka sasa kumbukeni tunacheza na timu kubwa Afrika ambayo inashika nafasi za juu kuliko sisi kwenye viwango vya FIFA wanatuzidi karibia mara tatu wao wako nafasi ya 60 sisi tukiwa nafasi ya 147 kwa mujibu wa FiFa Rakings March 2018,
(http://googleweblight.com/i?u=http://www.fifa.com/fifa-world-ranking/ranking-table/men)

Pili nyinyi mnaolaumu timu, kocha na wachezaji ni mashahidi wa ukweli kuwa mnakaaga kwenye luninga mkiwashuhudia Mahrez anavowasumbua kina Kante EPL, Baghdad, Islam wanavotisha Ulaya, sasa leo ndo tumewapangia Gadiel na Kapombe, ebu kuweni fair basi, hamuoni kama CAF kutupanga na Algeria wanataka tukajifunze mpira sio kushindana, ndo maana kila karenda ikitoka Tanzania Vs Algeria wana lao jambo na bahati nzuri vijana wameanza kuimpruvu juzi wamepunguza wiki mpaka siku nne, kwa nini tusiwashangilie.

Mwisho naona wote mnaolaumu sio mashabiki wa mpira, mmevamia fani, ini aza wedzi; 'stresi zenu za maisha mmeamshia kwenye mpira, ndo nyie mnaopiga marefa viwanjani' kwa sababu nimesikiliza maoni ya makocha hakuna alielaumu ata mmoja wote wametaja sababu za kiufundi ikiwemo maandalizi ya timu.
 
mkuu hivi unajisikiaje umekaa na mwanao huku unakula bisi kwenye li sikilini likubwaa, unashangilia timu yako inashindiliwa goli saba..unadhani baada ya dakika tisini, utakuwa ni mzima kweli? yaani kila Timu mkikutana nayo ni kichapo tu..
 
umetumia nguvu nyingi kuandika utumbo, timu inafungwa kwa uzembe halafu unatetea hata wewe sio mzalendo kwa kutetea upuuzi

  • TFF migogoro ya viongozi haishi
  • kocha hana mkataba timu ya taifa kumbuka hii ni professional yake
  • wachezaji hawalipwi posho zao kwa wakati
  • hakuna mpango wa kuandaa wachezaji kwa future

uzalendo utatokea wapi?
 
Back
Top Bottom