Waandishi wa habari waaswa kuwaibua wakwepa kodi, wakumbushwa nafasi yao kuchochea ufikiwaji wa malengo ya Bajeti

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
135
227
Katika kuhakikisha Serikali inafikia malengo ya bajeti kama zinavyopitishwa waandishi wa habari nchini wamehaswa kutumia vyema uwezo na nafasi zao kitaaluma kuchochea ufikiwaji huo ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
IMG-20240514-WA0011.jpg

Kauli hiyo imetolewa Mei 12, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro katika mafunzo ya siku mbili.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, amesema kuwa waandishi wa habari wanaweza kutumia taaluma zao na vyombo vyao kuhamasisha ulipaji Kodi, utoaji wa risiti sambamba na kufanya habari za uchunguzi kufichua wakwepa kodi.

"Serikali inapitisha bajeti lakini namna ya kupata hizi fedha tunahitaji mchango wenu kama wanahabari kuhamasisha Watu kwamba wana wajibu wa kufanya na sisi kama Serikali tuna wajibu wa kufanya ili kuweza kuzipata hizi fedha"amesema Benny Mwaipaja

Akitataja miongoni mwa mambo ambayo wanaweza kusaidia amesema "Mtusaidie kufichua watu wanaokwepa kodi, nyinyi mnafanya Habari za uchunguzi (investigative journalism), fanyeni uchunguzi mkiona watu wanakwepa penyezeeni hata kama sio kuripoti lakini tuambieni kwamba Mtu fulani anakwepa kulipa kodi ya Serikali"

Aidha kufuatia kongamano hilo ambalo limejikita kutoa elimu kwa baadhi ya ya waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini, Benny Mwaipaja amesema kuwa mitandao ya kijamii kwa siku za hivi karibuni imekuwa na tija kubwa kwa kueneza taarifa kwa uharaka pamoja na kutoa fursa za moja kwa moja kwa wananchi kutoa maoni (comment) ambayo wao wadau uyafanyia kazi.

"Citizen Journalism inafanya habari kuenea kwa kasi kulingana na teknolojia inavyoimalika na kuongezeka, kwahiyo sisi hapa jukumu letu ni kuhakikisha kwamba tunapeleka ujumbe ambao ni sahihi zaidi kwa wananchi kuliko hao ambao sio wanataaluma." amesema Benny Mwaipaja

Ameongeza "Tunapata 'Feedback' nyingi sana kutoka kwa wale ambao wanatoa maoni yao tukishaposti habari zetu, nasisi tunafanyia kazi maoni ambayo yanatolewa, mkishaposti tunapitia tunasoma"

Akiwasilisha mada katika kongamano hilo kuhusu Pensheni na Mirathi, CPA Jenipha Josephat Ntangeki kutoka Wizara ya Fedha, amesema kuwa Serikali ipo kwenye mpango kuandaa mpango wa 'Mstaafu Portal' ambao unalenga kuwasaidia watumishi wanaostaafu kupata mafao yao kwa uharaka bila kupata changamoto.

Pia amewahasa wastaafu wanaofuatilia mafao yao kuwa makini na matapeli ambao wamekuwa wakipiga simu na kutaka kuwatapeli wastaafu hao kwa kuwaadaa kuwapatia mafao yao kiurahisi, amesisitiza kuzingatia taratibu zilizopo wazi katika kufuatilia masuala hayo.

Lakini amesema kuwa Serikali hipo kwenye mpango wa kutumia mifumo kidigtali utakaosomana na LITA ili kutambua kuwa urahisi na uharaka wastaafu waliofariki waliokuwa wanaopokea mafao ili kuepusha mazingira ambayo yamekuwa yakidaiwa kutokea kwa Watu waliofariki kuendelea kudaiwa kuonesha kupokea mshahara licha ya kutowafikia wahusika.

Hoja hiyo ameieleza kufuatia swali la mshiriki wa kongamano hilo kuhoji jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali kutambua wastaafu waliofariki ili kusaidia familia kunufaika na stahiki ambazo wanastahili kisheria.

Hata hivyo baadhi ya washiriki wametoa ushauri kwa Wizara ya Fedha pamoja na taasisi zinazotoa mafao kuzingatia zaidi ulinzi wa taarifa binafsi za watu wanaowahudumia ili kuepusha taarifa kufika kwa matapeli ambao uzitumia kwa utapeli.

Mshiriki alidai kuwa matapeli wanaweza kupata taarifa kwenye daftari la 'wageni' na kuzitumia tofauti hivyo amesisitiza umakini unaolinda taarifa hususani kuzingatia Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Mada nyingine kwenye kongamano hilo ni pamoja na kuwaongezea ujuzi na uelewa juu ya namna namna bora ya kuripoti taarifa za Bajeti. Mada hiyo inafundishwa ikiwa imabakia siku chache kusomwa kwa bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2024/ 2025.

Sanjari na hayo wawasilisha mada kutoka Wizara ya Fedha wamesisitiza kwamba huduma kwa wastaafu zinatolewa bure, kwamba mstaafu anapatiwa mafao yake bila kulazimika kutoa fedha.

Ambapo imesisitizwa juu ya umuhimu wa wanahabari kuwaeleza wastaafu namna ya kupata taarifa sahihi kwenye vyanzo vya kuaminika ili kuepuka utapeli ambao unadaiwa kuwakumba, hususani kupigiwa simu na watu wanaojitambulisha kutoka kwenye vitengo vinavyotoa huduma hizo, kuwa wawatumie pesa kiasi fulani ili kuwawezesha kupata mafao kwa uharaka bila usumbufu.

Ili kuendelea kukabiliana na changamoto hiyo pamoja na nyingine ambazo zimekuwa zikitajwa kuwakumba wastaafu nchini wadau hao kutoka wizarani wamedai kuwa tayari jitahada mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwemo kutoa elimu kupitia vyombo vya habari, makongamano na kwenye nyumba za ibada.

Vilevile Salome Kingdom ambaye ni Mchumi kutokea Wizara ya Fedha, akiwasilisha mada siku ya pili, kuhusu namna bora ya kuripoti taarifa za bajeti, amesema wamekuwa wakifanya jitahada za kufanya Bajeti kusomeka kutokana na kuwepo kwa maneno yenye ugumu kutambuliwa na Watu wengi kirahisi.

Amedai kuwa pia waandishi wamekuwa wakikumbana na changamoto katika kuripoti viwango mbalimbali vya fedha ambavyo utajwa kwenye bajeti hizo na kupelekea ugumu wa namba kusomeka na kueleweka kirahisi.

Akiwasilisha mada amesema zipo mbinu mbalimbali ambazo waandishi wanaweza kuzitumia na wakaeleweka zaidi kwa jamii, lakini amegusia namna mchakato wa bajeti unavyoazia ngazi ya chini, kupitishwa kwake hadi kutekelezwa.

IMG-20240514-WA0012.jpg
Ambapo amesema kuwa Wizara ya Fedha inatambua umuhimu wa waandishi wa habari katika michakato hiyo yote hususani kuhabarisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayoweza kuwa yanaibua maswali.

Kongamano hilo limehitimishwa kwa washiriki wa kongamano hilo kuhaswa kuendelea kushirikiana na Wizara katika mambo yanayohitajika kupatiwa majawabu kwa manufaa ya umma.
 
Nawasihi wanaokwepa kodi waongeze bidii zaidi ili kuepuka upuuzi wa matumizi ya hovyo ya fedha za umma
 
Back
Top Bottom