Waandishi wa habari TZ waonjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari TZ waonjwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Barubaru, May 20, 2011.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  MCT yakerwa uandishi usiozingatia maadili
  Na Mwandishi wetu  20th May 2011


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni


  Baraza la Habari Tanzania (MCT), limesema limebaini kwa masikitiko mwenendo mbaya wa baadhi ya waandishi kuandika habari bila kuzingatia maadili.
  Taarifa ya Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Kajubi Mukajanga, ilisema jana kuwa masuala ya imani yana unyeti mkubwa unaopaswa kuzingatiwa katika uandishi ili kuepuka upotoshaji unaoweza kuleta uchochezi na chuki katika jamii.
  Ilisema kumekuwa na uandishi usiozingatia uhalisia, ulinganifu na umahsusi na badala yake kuchukua mfumo wa kuegemea upande mmoja hivyo kufanya majumuisho yasiyokuwa na ukweli wowote.
  Alisema mapungufu hayo ya kiweledi yamesababisha habari nyingi kuwa potofu na za kuchonganisha kwa jamii.
  Ilisema weledi hautaki kwa mfano gazeti kumhoji sheikh mmoja au kadhaa au askofu mmoja na kutoka na vichwa vya habari vinavyosema “Waislamu wataka…au Wakristu wataka” ikiwa ni mawazo ya kiongozi fulani wa kidini.
  Ilisema madhehebu yanaweza kuhusishwa tu ikiwa anayehojiwa ni msemaji rasmi na anazungumza kwa niaba ya madhehebu hayo.
  “Vichwa vya habari kama ‘Maaskofu wamng’oa Naibu Meya Arusha,’ huku kukiwa hakuna ushahidi wowote ndani ya habari yenyewe unaoashiria kuwa kujiuzulu kwa huyo naibu meya kulitokana na shinikizo la maaskofu ni upotoshaji unaoweza kusababisha chuki,” ilisema sehemu ya taarifa.
  “Mbaya zaidi ni pale kesho yake gazeti lingine linapofuata masheikh na kuwaomba kauli yao kuhusu kung’olewa kwa naibu meya kulikofanywa na maaskofu,” ilisema.
  Ilisema ni wazi kwa kufanya hivyo wanahabari watageuka wachonganishi.  CHANZO: NIPASHE


  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli waandishi wengi huko Tanzania wametanguliza maslahi binafsi mbele na kuvunja maadili ya kiuandishi.

  Bora baraza la habari tanzania mmeliona hilo na sasa kulisema hadharani. lazima mtengeneze adhabu kwa waandishi wanao kiuka maadili ya kazi zao
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Kuna wale wanaojulikana kama makanjanja,ndo tatizo.
   
Loading...