Waandishi Wa Habari Nchi Hii Mjitafakari

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Tasnia hii kwa miaka ya karibuni imekuwa chaka la waliokosa sifa za kuendelea na masomo ama kazi nyingine. Ndiyo likaja jina la makanjanja. Ni tasnia iliyojaa wenye njaa na elimu ya kuunga unga.

Nchi waandishi wa habari hawana msimamo wa kile wanacho kipigania. Lkn pia kwa njaa zao wamekuwa wakitumiwa na wamiliki wa vyombo vya habari na wanasiasa pia. Natoa mifano michache hapa chini:-
1. Kabla ya wahariri kuongea na rais pale ikulu kulikuwa na kelele zikipigwa juu ya ubovu wa muswada wa habari uliokuwa bungeni wakati huo. Lkn walipouliza suala hilo kwa rais aliwapa makavu laivu kuwa hawajui wanacho pigania, muswada ni mzuri, una maslahi yao mengi na atausaini bila kupoteza hata sekunde utakapo mfikia.
Tangu hapo kimyaaa! kimya kabisa. Hata silaha zenu (kalamu) mmeziweka sandukuni.

2. Mwangosi alifariki, A. Kibanda na Kubenea walipewa kashkash kubwa, wengi wamewahi kupigwa na sasa Halfan Lihundi akaswekwa ndani lkn tunaishia kusikia matamko mepesi.

Acheni Kujipendekeza Ili Mpewe Vyeo. Fanyeni Kazi.
 
Polycarp Isaya Urio

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
2,008

Kipengele cha kwanza ukimya wao ulimaanisha walimuelewa Rais na kukubaliana naye.
Kipengele cha pili hayo ni mambo ya kisheria na Kuna baadhi ya hatua zimechukuliwa ambapo mhusika kafungwa miaka 15.
Hilo la elimu linahitaji kuangaliwa ili kua na waandishi weledi tofauti na siku za nyuma.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom