Waandishi vihiyo na kubeba wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi vihiyo na kubeba wanasiasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fiksiman, Apr 8, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ni kawaida kabisa kukuta kichwa cha habari kikubwaa cha kuvutia tena kwenye gazeti lenye heshima la kitaifa KURASA YA MBELE kuashiria habri muhimu na jamii yote ipepesa macho na hata kuingia mifuko wanunue ili wajue kuna nani. Maajabu utasikia kinasema "Bwana Fulani anatabia ya kujisaida kitandani" au amelala nyumba ndogo!

  Sio siri inakera sana hasa ukijua kuwa aliyeandika habari hiyo hakuwa na hakika pengine alipata dokezo toka mtu wa karibu wa mtu huyo basi atasema chanzo chetu cha kuaminika. Mhusika cha kushangaza zaidi mhusika akijitokeza kukanusha ama kutaka kuwachukulia hatua wanakimbilia uhuru wa vyombo vya habari ooh sijui waache waandishi waseme...ebooo kusema gani kusiko na mipaka? Na haya tuambie ni sehemu gani iliyosema habari za mtu binafsi ni uhuru wa kusema....uandishi gani huu kajisema chenkapa!

  Nasema tujirekebishi sitaki kusema mengi au kuibua na kuanza kutajana majina fulani hajaenda shule kaingizwa na shemeji yake baada ya kufundishwa ABC za uandishi na inasemekana kila akiandika habari zake lazima agezee habari ya kwenye gazeti ili asikosee kanuni...aaah tujirekebishe hata wewe hujasomea sasa si uanze kwa kujifunza heshima ya fani yenyewe badala ya kuwachafua wenye fani zao!!!!! Kuna mambo mengi ya msingi kama baa la njaa linalonukia, maslahi ya wabunge na uwiano wa kazi wanazozifanya au hata upungufu wa wataalam kutokana na vijana wengi kushindwa kulipia gharama za elimu juu huku Serikali igawa mabilioni kwa wajasiliamali ambao watagawana elfu hamsini kama mtaji...eee bwana ndio yapo hayo muyaandike na sio huo ushabiki wenu maandazi.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hawa ni mafisadi wa aina yake,watafutiwe dawa kama mafisadi wengine.
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Jambo moja liko wazi na wana taaluma ya uandishi kila kukicha wanakwepa kulikubali,nalo ni kwamba JUST AS THE MEDIA NEEDS PROTECTION AGAINST GOVERNMENT EXCESSIES SO DOES THE PUBLIC NEED PROTECTION AGAINST MEDIA EXCESSIES.
   
 4. k

  kela72 Senior Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu hali hiyo inakera sana! Lakini usisahau hata matatizo ya kuwa na uongozi mbovu ktk nchi yetu ni waandishi hahao kwa kiasi kikubwa walichangia kutuuzia mbuzi kwenye gunia mwaka 2005. Najua wapo watakaojifanya hawakuhusika, lakini ukweli uko wazi walihongwa na wanamtandao ili wampe sifa Nguchiro aliekuwa kwenye kiroba tukiaminishwa kuwa ni mbuzi!! Heshima juu kwa mwandishi kama Ngurumo (Ansbert) yeye aliwahi kuomba msamaha kwa hilo.
  Hebu angalia kichekesho kingine cha waandishi wetu, Rostam miaka nenda rudi amekuwa akiwashambulia wenzake kupitia vyombo vyake vya habari huku wao wako kiimya! wahanga wake ni kama JOHN MAGUFULI, SAMWEL SITTA, FREDRICK SUMAYE N.K Sasa kituko no hiki, baada kujibiwa na Dk M wakyembe waandishi wanatuambia 'eti hayo ni malumbano!' malumbano vipi mtu kujibu tuhuma za fisadi??
   
 5. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka unajiamini sana ila angalia wanamtandao
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
Loading...