Waandishi msiwachonganishe wamachinga na Serikali

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,288
12,579
Wamachinga ni watoto wetu, wajukuu zetu, wapwa zetu, kaka, dada zetu, na jamaa zetu, wanatoka makabila yote na mikoa yote nchini Tanganyika na Zanzibar, hivyo hakuna mwenye chuki nao binafsi. Wamachinga wamejikuta pale walipo na kufanya vile wanavyofanya kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo hizi zifuatazo:

1. Wamachinga wengi wameletwa mijini na watu wenye ajira zao kuja kuwafanyia kazi hizi ndogondogo kwa lengo la kuwaongezea kipato. Watu wenye ajira mijini wamewatoa vijana vijijini na kuwapa mitaji au kuwafungulia biashara hizi sehemu zisizo rasmi. Hivyo biashara nyingi za wamachinga ni za watu wenye ajira na nafasi. Hapa tatizo ni mishahara midogo kwa watumishi.

2. Kuna wachinga waliohamia mijini kutoka vijijini kutokana na hali ya maisha vijijini kuwa mbaya: Hapa tatizo ni halmashauri za Wilaya husika na serikali za mitaa.

3. Kuna machinga ambao ni watoto wa wamachinga: Kama baba kama mtoto; wakati watoto wa wanasiasa wanarithishwa kazi kama za wazazi wao za udiwani, ubunge, uDC, uRC, ukurugenzi au Urais na wamachinga nao wanawarithisha watoto wao biashara, vizimba, meza na maeneo holela ya kufanyia biashara ya kimachinga: Hapa tatizo ni wazazi wenyewe.

4. Machinga waliofuata mkumbo: Kuna machinga waliojikuta kwenye biashara hii kwa kuona na kusikia success stories za wenzao wanaofanya biashara ya machinga, hivyo na wao kuiga aina hii ya kujiongezea kipato: Tatizo hapa ni vijana wenyewe na serikali ambayo haikulinda mipango miji yake.

5. Ukosefu wa ajira kwa vijana kutoka vyuoni: Baada ya kuhitimu masomo na kukosa ajira na mitaji ya kuanzisha shuhuli halali na rasmi kama kilimo, ufugaji, uvuvi, nk vijana wakajiingiza kwenye machinga kama sehemu ya kutafuta mtaji.

6. Wanafunzi waliokosa ada ya masomo yao: Wanafuzi wengi wa vyuo huwa wanafanya biashara za umachinga ili kupata karo na matumizi mengine wakiwa vyuoni, wanafunzi wengi mahudhurio yao vvyuoni ni hafifu sana kwasababu ya kukatishwa masomo mara kwa mara na uongozi wa vyuo kwaajili ya ada na kufanya biashara mitaani ili kupata mahitaji ambayo walipaswa kupewa na wazazi au serikali yao. Hapa tatizo ni wazazi na Serikali ambayo haitoi mikopo kamilifu kwa wanafunzi hasa kwenye vyuo vinavyopatikana mijini ambako maisha ni magumu sana.

7. Kuna machinga ambao wamepatikana kutokana na kufukuzwa kazi maofisini, kazi za nyumbani, na baa medi: Tatizo hapa ni waajiri.

8. Siasa: Kuna wamachinga ambao wamepewa mitaji wanasiasa na kuachwa wafanyanye biashara yoyote popote na wanasiasa bila bugudha ili wawe mtaji wa kura nyakati za chaguzi. Hapa tatizo ni wanasiasa.

9. Wafanyabiashara wakubwa: Kuna machinga ambao bidhaa walizonazo ni mali ya wafanyabishara wakubwa wenye lengo la kukwepa kodi au kutafuta wateja baada ya mbele ya maduka yao kuzibwa na wamachinga wenye bidhaa kama za kwao.

10: Serikali: Kuna wamachinga ambao wamekuwa pale walipo kutokana na serikali kukaa kimya tangu wakati wanaanza maandalizi ya kufanya biashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa: Hapa tatizo ni Serikali yenyewe na watendaji wenye dhamana.

Hivyo orodha ya sababu ni ndefu sana, lakini ni ukweli kuwa wamachinga wanatafuta riziki zao kwa kusababisha kero kwa watanzania wenzao walio wengi zaidi kuliko wao. Kero kubwa kuliko zote ni kuchafua mazingira kwa kuziba njia za maji na takataka zisizo na mfumo sahihi wa ukusanyaji.

Wanajisaidia popote hasa haja ndogo, wanaziba njia za magari na waenda kwa miguu ambao ni wengi zaidi kuliko wao, wanawasha moto kando ya njia na kuyeyusha lami ya barabara kwa joto la majiko na kuhatarisha maisha ya wengine kwa moto na mafuta ya moto ya kukaangia chips na mihogo. Wanaharibu mandhari ya mitaa, barabara na miji.

Kwa vyovyote vile watu hawa hakuna mtu anaeweza kuwapa maeneo wote wakatosha, kwakuwa idadi yao inaongezeka kila siku maadamu kuwa ajira rasmi kwa vijana hakuna, mitaji hakuna, mishahara ya watumishi ni midogo, wanafunzi hawana ada kamilfu inayotakiwa na vyuo, masoko ya mazao hakuna, wanasiasa uchwara wanaotafuta kura kwa njia hii laghai bado wapo, mikopo yenye riba ndogo hakuna na wafanyakazi wa nyumbani na baa bado wanaachishwa kazi zao.

Serikali kuwaondoa mitaani ndio njia pekee ya kimataifa ya kutatua tatizo la ukosefu wa ajira. Njia hii inaonekana kama njia katili lakini ni njia inayosababisha vijana kuhangaisha akili zao katika ubunifu. Njia hii indiyo ndio inayosababisha vijana wa Marekani na Ulaya wakiimba wanaimba kweli, wakipigana kwenye boxing wanapigana kwelikweli, wakicheza mpira wanacheza kweli, kiajiriwa mahali wanachapakazi kwelikweli kwasababu wana options chache sana.

Njia hii inachochea ubunifu kwa vijana kutumia vipaji na akili zao badala ya kutandika nyanya chini ya mchanga au kutembeza mashati mawili, njia hii ya kuwafukuza mitaani itawafanya wakafuge vizuri, wakalime vizuri na wakafanye biashara vizuri huko waendako badala ya kuwaacha wachuuze mitumba na bidhaa za wachina mitaani.

Waandishi wa habari tuisaidie serikali kuwaondoa wamachinga kwenye maeneo yasiyo sahihi badala ya kuungana na wamachinga dhidi ya serikali yao inayotaka kuwaondoa wavamizi wa maeneo yenye maslahi kwa watanzania wote. Kuna waandishi wanawaunga mkono wamachinga wabaki pale walipo kwa kuwakumbusha ahadi za Rais Magufuli, R.I.P kwao. Lazima tusonge mbele; hata Mzee Mwinyi aliyaacha baadhi ya mambo ya Nyerere, na Mkapa aliyaacha baadhi ya mambo ya Mwinyi, na Kikwete aliyaacha baadhi ya mambo ya Mkapa, na Magufuli aliyaacha baadhi ya Kikwete na Mama Samia LAZIMA ayaache mchana kweupe baadhi ya mambo ya Magufuli, sio dhambi na haijawahi kuwa dhambi hata huko nyumba kwa waliomtangulia.

Tuwaelimishe wafanyabiashara hawa juu ya uzuri na ubaya wa kuondoka kwenye njia za waenda kwa miguu na magari, njia za maji, nk. Kuwapangia maeneo lisiwe sharti la kuondoka sehemu waliyoivamia. waondoke kama walivyokuja ila wapewe muda wa kuondosha bidhaa zao kwa kupewa taarifa ya wiki moja hata mwezi ikibidi.
 
Kuna waandishi wanawaunga mkono wamachinga wabaki pale walipo kwa kuwakumbusha ahadi za Rais Magufuli, R.I.P kwao...
Samia kuyaacha mambo ya Magufuli siyo sawa na marais wengine kuyaacha ya watangulizi wao. Huyu Samia alinadi ilani ile ile ya Magufuli. Ahadi za Magufuli ndiyo ahadi a Samia, iweje sasa anabadilika??

Vinginevyo ni unafiki na uzandiki uliopitiliza.
 
Samia kuyaacha mambo ya Magufuli siyo sawa na marais wengine kuyaacha ya watangulizi wao. Huyu Samia alinadi ilani ile ile ya Magufuli. Ahadi za Magufuli ndiyo ahadi a Samia, iweje sasa anabadilika??

Vinginevyo ni unafiki na uzandiki uliopitiliza.
Samia Sio Makamu wa Rais sasa.Samia ni Rais kamili hivyo hana haja ya kufuata ya mtangulizi wake..hilo unatakiwa uelewe.
 
Samia kuyaacha mambo ya Magufuli siyo sawa na marais wengine kuyaacha ya watangulizi wao. Huyu Samia alinadi ilani ile ile ya Magufuli. Ahadi za Magufuli ndiyo ahadi a Samia, iweje sasa anabadilika??

Vinginevyo ni unafiki na uzandiki uliopitiliza.
Samia alikuwa akiangalia na macho tu boss wake akigawa fedha barabarani, walikuwa hawapatani watoe au wasitoe pesa na watoe ngapi. Sina uhakika ilani ya CCM Ina ujenzi wa bank chato, mbuga chato
 
Samia kuyaacha mambo ya Magufuli siyo sawa na marais wengine kuyaacha ya watangulizi wao. Huyu Samia alinadi ilani ile ile ya Magufuli. Ahadi za Magufuli ndiyo ahadi a Samia, iweje sasa anabadilika??

Vinginevyo ni unafiki na uzandiki uliopitiliza.
Kwa hiyo Samia angoje 2025 anadi ilani yake ya kuwatimua machinga barabarani au sio!?
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Samia Sio Makamu wa Rais sasa.Samia ni Rais kamili hivyo hana haja ya kufuata ya mtangulizi wake..hilo unatakiwa uelewe.
Katiba inasema makamu atarithi uRais, je anayechukua huo urais anarithi ilani ipi!? Anajitungia ya kwake mwenyewe!?
 
Samia alikuwa akiangalia na macho tu boss wake akigawa fedha barabarani, walikuwa hawapatani watoe au wasitoe pesa na watoe ngapi. Sina uhakika ilani ya CCM Ina ujenzi wa bank chato, mbuga chato
Hahaha! Hapo kwenye bank Chato pamenitoa meno nje. Sawa mkuu maelezo yako yamenishibisha.
 
Katiba inasema makamu atarithi uRais, je anayechukua huo urais anarithi ilani ipi!? Anajitungia ya kwake mwenyewe!?
Anarithi sera na ilani sio matamko, hisani, wema, huruma, uonevu, Chuki, tabia na mihemko ya utashi ya anaemrithi. Mfano, sera na ilani ya CCM haisemi wamachinga waruhusiwe kufanya biashara kwenye njia za waenda kwa miguu na juu ya mitaro ya maji taka.
 
Anarithi sera na ilani sio matamko, hisani, wema, huruma, uonevu, Chuki, tabia na mihemko ya utashi ya anaemrithi. Mfano, sera na ilani ya CCM haisemi wamachinga waruhusiwe kufanya biashara kwenye njia za waenda kwa miguu na juu ya ya maji taka.
Kwani alivyokuwa ananadi mgombea urais kuwa watawezeshwa kukopa kwa kutumia vitambulisho vyao hayakuwa yanatoka kwenye ilani!? Yale ya mikutano ya vyama vya siasa mbona bado anafata msimamo wa yule aliyepita, kwa nini asifuate katiba!? Mwambieni achague kuwa moto au baridi, kujaribu kuwa vuguvugu ni utapeli huo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom