Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Leo nimesikitishwa sana kwa na kitendo cha aibu cha msanii Irene Uwoya kugawa rushwa ya fedha kwa wanabahari mbele ya kamera.
Uwoya amefanya hivyo mbele ya camera kitendo kinachodhalilisha sana taaluma ya habari.
Lakini pia, sijathibitisha, naambiwa aibu nyingine ya mwaka ni kuwa wapo wanahabari waliopigana vikumbo kugombania fedha hizo alizokuwa akizigawa kwa mtindo wa pedeshee wa kike.
Kama hili la pili ni kweli basi, historia leo imeandikwa, hatuna waandishi nchi hii bali tuna wasanii katika tasnia ya habari.
Hapa ndio unajiuliza watetea taaluma ya habari kama hata ile Idara ya MAELEZO, Jukwaa na wahariri na MCT wako wapi?
Hawa waandishi wakemewe na au hatua zichukuliwe dhidi yao.
Mwalimu wangu Dr Kibatala (sio huyu wakili) aliwahi kutoa neno likanukuliwa visivyo. Alipowaambia waandishi wa habari ukweli huo wakamtolea clip kuthibitisha kuwa ni kweli kasema yaliyoandikwa. Dr Kibatala akawaambia hivi: nilichokisema nyie hamna uwezo wa kukitafsiri inavyotakiwa maana wengi wenu mmekimbilia uandishi wa habari baada ya kushindwa mitihani ya sekondari. Anaebisha naomba aniruhusu nitoe matokeo yake hadharani.
Challenge hiyo aliwapa waandishi miaka ya mwanzo ya 90, hadi leo hii hakuna mwandishi aliempa hicho kibali.