Waamuzi waliochezesha yanfa vs simba waondolewa ligi kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waamuzi waliochezesha yanfa vs simba waondolewa ligi kuu

Discussion in 'Sports' started by WABHEJASANA, Oct 6, 2012.

 1. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wanajamvini siku moja baada ya mechi kati ya Yanga na Simba kulitokea mabishano mengi kati ya mashabiki wa pande zote mbili,huku kila mmoja akiwalaumu waamuzi kwamba ndio waliosababisha timu yao ishindwe kuibuka na ushindi.

  Binafsi nishuhudia mechi hiyo LIVE na haya hapa niliyoyasema.
  1:Mshika Kibenderea namba mbili Ephrony Ndissa yule aliyekuwa akinyoosha mara kwa mara kibendera kuashiria wachezaji wa Yanga wameotea ni lazima amsababishie Mwamuzi wa kati Methew Akrama kutoka mwanza matatizo,
  2:Mwamuzi Akrama kutompatia kadi nyekundu 'BOBAN'kadi nyekundu kwa rafu mbaya aliyomcheea kelvine Yondani lazima Imcost.
  3:Mwamuzi Akrama kutomwadhibu Mbuyu Twite wa yanga kwa kumuangusha Christopher kwenye eneo la hatari,na kuipatia simba penati,na kadi ambayo ingemsababishia Twite kadi ya pili na hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu lazima imsababishie matatizo tena makubwa.

  Sasa hebu angali taarifa hii iliyotolewa na Msemaji wa TFF Boniphace Wambura halafu ujihoji
  Kamati ya Ligi imewaondoa waamuzi watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom(VPL) kwa kushindwa kumudu michezo waliyopangiwa. Waamuzi hao ni Mathew Akramawa Mwanza aliyechezesha mechi namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati yaYanga na Simba iliyochezwa Oktoba 3 mwaka huu.
  Wengine ni Paul Soleji wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Simbana Tanzania Prisons, na mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo MwarabuMumbi wa Morogoro. Pia mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi ya Yanga na Simba,Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam amepewa onyo.
  Kamishna wa mechi namba 28 kati ya Yanga na African Lyon, PiusMashera ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi hiyo kwa kuchelewakufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (Pre match meeting) na uwanjani.
  Vilevile Mashera kwenye ripoti yake aliwasilisha malalamiko dhidiya msimamizi wa kituo cha Dar es Salaam, na kwa vile suala hilo ni la kinidhamuametakiwa alipeleke kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
  Nayo Simba imepigwa faini ya jumla ya sh. 600,000 kwa kuchelewakufika kwenye pre match meeting ya mchezo wao dhidi Tanzania Prisons (sh.100,000) na kwa washabiki wake kuwatupia chupa za maji waamuzi wa mechi hiyo(500,000).
  Pia Kamati ya Ligi imeagiza kuwa kwa vile suala la kipa ShabaniKado wa Mtibwa Sugar kudaiwa kumpiga kiongozi mmoja wa Ruvu Shooting mara baadaya mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ni la kinidhamulipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikishola Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
   
 2. Ngalangala

  Ngalangala JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Peleka kule kwenye michezo sheikhe ili tuweze kuchangia vizuri
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mchezo ulikuwa fair na wachezji walimpa mwamuzi mkono wa Hongera
  Sasa sijui mechi nzuri ya watani wa jadi mpaka mtu afungwe?
   
 4. p

  pilau JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ...... unafahamu kuwa wachezaji wa Simba Kazimoto, Christopher na Mkude wote walitoka nje kwa kuchapwa buti na wale wa Yanga, Faulo ni faulo tu kuizungumzia faulo ya Boban pekeyake sijaridhika... zungumzieni, na mfanye tathimini ya matukio yote uwanjani bila ushabiki.....
   
 5. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Si bure katumwa na gabachori kuja kujisafisha, sijui vibaraka wa Yanga watauambia nini umma huu wa Watanzania ambao ulishuhudia mpira ule "LIVE" ili wawaelewe! Ripoti hii ya TFF ndiyo iwafungue macho Wa-TZ na wapenzi wa Simba SC kuwa jiji la Mwanza ni ngome kuu ya Yanga na hilo nimekuwa nikilisema mara kwa mara lakini TFF wanafunga visikilizio vyao.
   
 6. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  grafani11 unatumia kilevi gani? Usije kukuta ni kati ya wale wanao'nusa petrol? mana'ke naona unaandika sana hlf full of nonsense,mfano hapa Jiji la Mwanza na report ya TFF ya kuwafungia wale wachezaji wenu wa ziada vinauhusiano gani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo mtu yeyote anayekupa ukweli unafikiri anatumia kilevi kama wewe? Ama kweli kilevi kimekuzidia mpaka umeshindwa kusoma vizuri ripoti ya TFF na asilimia kubwa ya marefa waliofungiwa wanatoka mkoa gani.. Poor anselm...
   
Loading...