Regnatus Cletus
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,114
- 959
Waalimu ni waamini wazuri sana wa adhabu ya viboko! Wanapenda sana matumizi ya fimbo wakiamini ni nyenzo ya kufundisha.
Imani hii ya viboko imewafanya waone kwamba bila fimbo maisha yao yatakosa raha. Kimsingi wanapenda sana kuchapa, tena kuchapa mpaka mwanafunzi atoke uhai basi roho zao zinasuuzika.
Waraka wa elimu pamoja na sheria ya elimu na kanuni ya elimu, inaelekeza kwamba, adhabu ya viboko visivyozidi vinne inapaswa kutolewa na mwalimu mkuu husika wa shule kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi.
Baada ya adhabu, mwalimu mkuu atahakikisha anarekodi jina la mwanafunzi husika, sababu ya kutoa adhabu, na jina husika la mwalimu husika.
Utaratibu huu umelenga kuepusha ukatili mashuleni, mauaji ya wanafunzi, na adhabu zilizozidi kipimo. Kwa kuzingatia hilo, utaratibu wa utoaji wa adhabu ya viboko umetengenezewa mfumo stahiki.
Lakini walimu wote wanalia. Wanataka kuchapa.
Nashauri walimu wote watakaokiuka utaratibu huu wa utoaji adhabu, baada ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama kufukuzwa kazi na kusimamishwa, wapewe adhabu kali ya viboko. Ndio, wachapwe haswa maana hilo ndilo wanaloliamini na kulipenda sana.
Punda bila mjeledi haendi. Walimu wanaokiuka maaagizo wawajibishwe kikamilifu bila kusahau kuwasulubu kwa mboko toshelezi.
Nimesema waalimu wanaokiuka maagizo.Mkuu umetembelea walimu wote nchini Tanzania ukawakuta wanalia kuchapa viboko?
Ni kweli. Lakini adhabu isiyozidi viboko vinne itatolewa na mwalimu mkuu husika wa shule.Hapa fimbo tuu. Dawa ya mwanafunzi ni viboko. Watu hawajui kiasi gani wanafunzi hasa walio kwenye balehe walivyo watukutu na dharau. Hawaendi bila fimbo.
Nazani ungetoa ushauri nini wafanye walimu katika malezi hasa kizazi Cha sasa cha watoto tulio nao,na si kuwapigilia walimu msumari wa moto kwenye kidonda hasa wanaovunja sheria,nini njia mbadala ya kuwalea watoto wetu hasa kwenye kizazi tulichonacho?Nimesema waalimu wanaokiuka maagizo.
Hilo ni jambo ambalo haliwezekani.Ni kweli. Lakini adhabu isiyozidi viboko vinne itatolewa na mwalimu mkuu husika wa shule.
Adhabu isiyozidi viboko vinne itatolewa na mwalimu mkuu husika wa shule kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi. Baada ya adhabu, mwalimu husika atarekodi jina lake, jina la mwanafunzi, na sababu ya viboko.Nazani ungetoa ushauri nini wafanye walimu katika malezi hasa kizazi Cha sasa cha watoto tulio nao,na si kuwapigilia walimu msumari wa moto kwenye kidonda hasa wanaovunja sheria,nini njia mbadala ya kuwalea watoto wetu hasa kwenye kizazi tulichonacho?
Acha kazi.Hilo ni jambo ambalo haliwezekani.
Kwanza litawapa wanafunzi kiburi zaidi. Enzi zetu tulichapwa fimbo hadi unashindwa kukaa na hatukufa.
Mkuu umetembelea walimu wote nchini Tanzania ukawakuta wanalia kuchapa viboko?
Kuna dhambi mimi kuwa Mwalimu?Bila shaka utakuwa wewe ni mwalimu
Kuna dhambi mimi kuwa Mwalimu?
Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu.Huenda wamesikia shauri lako.
Acha kazi.