mwambunnyara
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 518
- 208
Habari za asubuhi wadau,nimetafakari sana juu ya mambo yanavyokwenda katika sekta yetu ya elimu,hususan kwa waalimu wa science.
Baada ya tafakuri yangu kwa muda mrefu,nimegundua kuwa,waalimu wa science tunapaswa kuwa na umoja wetu,nje ya CWT,kwani CWT haiwezi kutusaidia kabisa kwa changamoto zinazotukabili.
Katika ajira zilizotolewa na serikali kwa waalimu,kwa mwaka 2015 ziliambatana na ajira za wataalamu wa maabara,kwa ajili ya practicals,lakini tukumbuke kuwa kabla ya kuletwa kwa wataalamu hao wa maabara,walimu wa science ndio walikuwa wanafanya majukumu yote,practicals & theories,(hapo pana tatizo,kwani tumekuwa tunafanya kazi mbili kwa malipo yale Yale).
Kuna changamoto lukuki,ambazo sisi kama wana science tunapaswa kukaa kwa pamoja,kuzijadili,na kuziwasilisha kwa serikali yetu,ambayo inaonekana wazi kuzingatia sana utaalamu na sio siasa,(ushahidi wa hili ni pamoja na uteuzi wa waziri wa Elimu,Dr.Joyce Ndalichako).
Natoa wito kwa waalimu wenzangu wa science,tutengeze umoja huu ili kuweza kujadiliana namna bora ya kuboresha utendaji wetu wa kazi,lakini pia kutatua matatizo yetu.
NAPENDEKEZA JINA LA UMOJA HUU,LIWE TANZANIA SCIENCE TEACHERS UNION.