Waalimu tunadharauliwa sana hivi kwanini?

Ualimu sio kazi ya kufanya kwenye huu ulimwengu wa tatu basi tu umaskini watu hawawezi kuchomoka huko na hii ndio fimbo kubwa ya kuwachapia.

Ualimu ni umaskini, unyonge na kukosa uthubutu
Nani akafundishe sasa mkuu? Dah,nimecheka. Sio kazi yakufanya???
 
UYUI kuna shida pale, ukienda Masijala ya elimu utakutana na walimu kibao wanafatilia barua zao za madai. Eti mwalimu hakulipwa mshahara miezi miwili ya mwanzo wakati anaajiliwa, hapo ameanza kufatilia mwaka 2019 had leo hajalipwa. Sidhani kama kuna watumishi nchi hii wanatia huruma kama walimu asee.
 
Achana nawatu usihangaike nao ishi utakavyoo
 
Hiyo kada yenu,
ni watetezi wakubwa wa dhulma.
Msitegemee heshima kwenye hili
 

 
yaaani kuna dharau mpk basi nilikifika pale yaani hii hamashauri daaahhh we acha. maisha uvumilivu
 
Ualimu sio kazi ya kufanya kwenye huu ulimwengu wa tatu basi tu umaskini watu hawawezi kuchomoka huko na hii ndio fimbo kubwa ya kuwachapia.

Ualimu ni umaskini, unyonge na kukosa uthubutu
Mama Naa naomba namba yako PM.. Wewe ni mtu na nusu. Una pointi, nataka nikusikilize
 
Kada ya ualimu ilianza kudharauliwa wakati wa UPE badala ya Universal Primary Education ikaitwa Ualimu Pasipo Elimu. Hapo darasa la saba wakawa walimu shule walizosoma. Dharau ilianzia hapo.
Wenye ufaulu mzuri au wastani wakawa wanaenda taaluma nyingine zote kasoro ualimu na waliofeli Div 4 ndiyo walienda ualimu.
Hili donda limeimeza heshima ya ualimu. Ufumbuzi wake ni mgumu sana. Kumfanya mwenye div 1 aende ualimu. Inawezekana lakini yahitaji mabadiliko makubwa sana. Mishahara mizuri ba mazingira bora ya kufanyia kazi.
Nchi iamue !
 
Tatizo la hii nchi ni kubwa sana, failures ndio wanaokwenda katika kada nyeti zinazoweza kuleta mabadiliko mabaya/mazuri katika Taifa
Na tusipo badilika hali itakua mbaya zaidi,
Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…