Waajiri wanaotaka pasipoti kwanza

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,313
kumekuwa na katabia ka waajiri walio wengi hasa wa mashirika/taasisi ya serikali kudai mwombaji aweke picha (mara nyingi picha moja au mbili) pindi wanapotangaza nafasi za kazi kwenye vyombo ivyo. mi nashindwa kuelewa hizo picha ni za nini hasa ukizingatia kuwa waombaji walio wengi huchujwa na kuachwa ktk hatua za awali tu. Hi sio ni kuchezea hela za watu tu?

Kumtaka mtu alete picha ni kumnyima haki mwombaji kwa sababu ya gharama ya pesa na muda wa upatikanaji wa picha hasa ukizingatia wanataka pia umwone mwanasheria wa kuhakiki vyeti.

Labda mnisaidie wadau hizo ndo sheria za uajili au ni utaratibu tu ambao mtu anaamka nao. Mtazamo wangu hii sio haki kabisa hasa kwa mtu aliye mtaani na anatafuta kazi.
 
picha ni kama utambulisho wako, ni muhimu sana hasa unapoomba kazi
ni utaratibu mzuri unachohofia ni nn? hata vyuo nk lazima uweke picha
kuepuka kudanganya.labda kama ww una historia mbaya ya makosa ya jinai ndio unahofia ama sivo? acha woga hiyo sera ktk sekta ya utumishi.
 
Kwa akili ya kawaida tu, picha inasaidia kufuatilia kujua huyu anayeomba kazi ndiye tunayemfanyia usaili na ndiye tutakayemwajiri. Picha muhimu hasa katika kipindi hiki mnachojitahidi kuchakachua kila kitu. Usigome...live your life!
 
Wanamaliza passport photograph zetu hawa, bora tuwetunapeleka hz pcha pale tunapoitwa kwnye interview.
 
Hakuna sheria yeyote ya kazi inayomtaka mwombaji aweke picha yake kwenye barua ya maombi. Ikiwa mwajiri anahitaji picha basi hilo hutakiwa kufanywa na wale walio short-listed au, wanaoajiriwa tayari. Na tukumbuke kwa sheria za nchi nyingine, ni makosa kuweka picha yako kwenye CV kama unaomba clerical post ambayo si yenye kuhusika na customer care. The employer should not be attracted to ones personal appearance.

Labda nachoweza kukisia ktk hili ni udhibiti wa umri. Japo sioni kama ndio njia, lkn kwa akili zetu za kupandisha bei ya mafuta ya taa kuzuia uchakachuaji lolote laweza kuwa jibu sahihi. Kwa hiyo niconclude tu kuwa huo ni ufukunyuku wa kutaka kuwaangalia watu sura. Ole wetu wenye sura kama Sikamona
 
Back
Top Bottom