Waajiri tendeni haki kwa wasichana kumbuka nawe ulizaliwa na mwanamke

Hii ngoma nzito. kuna dada mmoja nimemwajiri kwenye internet cafe yangu bana na kajifungua nimempa miezi 3, sasa hvi nikitoka ofisini saa kumi na moja fasta naenda kufungua cafe hadi saa 4 usiku ndo nafunga mchana wote ipo closed. Nafikiria niajiri mwingine? nayule akirudi? duh .................................................
 
Kweli kazi ipo kwa akina mama.Mimi ninamfano hai wa dada mmoja tulimujiri katika idara ya IT kwa ajili ya kazi maalum lakini tumeishia kupoteza hiyo project.Alianza mara naumwa tumbo mara akapata mimba baada ya hapo akapewa bedrest ya miezi sita plus likizo ya uzazi siku 84 mwaka tayari.Yaani tumepata hasara kwa ajili ya mtu huyo.Sasa fikiria kama ungekuwa nao kama hao watano au kumi shirika kwisha kazi yake.

Shida yetu watanzania tunafikiri kazi zipo ili sisi tuajiriwe na kupewa mishahara na sio tufanye kazi ili mshahara uendelee kupatikana. Hivi kweli kuna mwekezaji anaweza kuanzisha mradi lengo likiwa ni kuajiri watu ili awalipe mishahara na sio kuwa na lengo la kupata faida? Ona sasa yaliyowakuta, huyo aliyesababisha project ife soon atawashitaki kwa kuwa hamjamlipa malimbikizo yake ya mishahara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom