Waajiri tendeni haki kwa wasichana kumbuka nawe ulizaliwa na mwanamke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waajiri tendeni haki kwa wasichana kumbuka nawe ulizaliwa na mwanamke

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mamabaraka, Jan 23, 2012.

 1. m

  mamabaraka Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna baadhi ya waajiri hasa ktk mashirika binafsi wanakwepa kuajiri wasichana, mi niliwah kusikia katika ofisi moja mkurugenzi akisema ukiajiri msichana graduate una hasara, akifanya kazi kidogo utasikia anataka kuolewa, akiolewa atapata mimba na kuanza kuumwa umwa kila mara anaomba ruhusa, akijifungua anadai matenity leave. Baada ya hapo mara mtoto anaumwa nampeleka hospitali mara clinic. Jamani waajiri na nyie mmezaliwa na wanawake tendeni haki kwa mabinti. Mnawanyanyasa kijinsia haipendezi kabisa.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hata ofısı za Serıkalı ıkıtokea wanawake wengı wakıpata mımba kwa mfuatano mabosı wa kıume mara nyıngı hawafurahıı kwa sababu kazı zınalala sana hasa wakatı wa maternıty leave. Ingawa sıyo kosa lao kwanı hakuna anayekuwa akıjua kuwa kıpındı hıcho hıcho mwenzake pıa anapewa ujauzıto.
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hawapendi wangezaliwa Kama sio Hao wanawake? Wanajitoa fahamu mbona wakezao wakiwa na mimba wanafurahi japo mimba si zao...
   
 4. korino

  korino JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 492
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  ahahahahahah umenchekesha! ni kweli kabisa me nshawah ona nafasi za kazi wamesema wanataka wanaume tu! sio haki jaman....kwa Mola mtaenda adhibiwa!
   
 5. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,345
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  jf never bouring,
  hata saa usiku wa manane nimo tu,
   
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Upande mmoja inauma ila kwa upande mngine ukizingatia sio kosa lao, wenyewe wanatafuta productivity.
  Naweza kusema ni kosa la paternalist system nzima, inayo toa value kwa kazi za watu wasio shinda nyumbani kusaidia basic needs za reproduction, feeding, shelter na mengine. wanaume au wanawake wanao taka kuonekana productive leo, lazima wacompete katika field za nje ya zile primary needs, huku ikiwa vigumu kwa mwanamke kuziacha moja kwa moja.
  Kama system inge ipa thamani kazi watu wanayo ifanya hata manyumbani kwao kama kazi za ndani, za kulea watoto, kupika na kadhalika, kwa kweli hawange lazimika kutafuta hizo kazi za ofisini ikiwa bado wanataka kua na watoto kila miaka miwili au mitatu.
  Ni swala ngumu sana kutatua.
   
 7. m

  majimbi Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa ukweli mabosi wengine hawako wazi kwa akina mama ni vema kuwajali manake nao wana wake zao na watoto nyumbani. tujue watoto ni taifa la kesho, sasa mama akienda matenity leave ndo majungu yanaanza! oooh jamaa hawafwati nyota ya kijani? tena ukute ndo umeunganisha kila mwaka mazee unalooooo!!!!:tongue:
   
 8. Maayo

  Maayo JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili kwel hata mm huwa linanishangaza sana kuna shule moja ipo Dodoma mfanyakazi yeyote wa kike (walimu, secretary na wengine) akipata ujauzito anaanza kuhesabu siku za kufanya kaz. Akijifungua tu ndo mwisho wa kazi. Mbaya sana.
   
 9. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ofisi zingine ukienda maternity, hakuna tena kwenda likizo
   
 10. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi nyie mkoje? Kama wewe ni bosi, unatoa ripoti ya kazi kwa mkubwa wako, unaweza kuweka hapo kipengele kuwa : Mapato yamepungua kwa kuwa uzalishaji mwaka huu umeshuka kwa vile wamama 17 walikuwa maternity leave?

  Kazi ya bosi ni kuangalia ufanisi wa ofisi yake na wala sio kubalance jinsia kazini. Kwanza wanawake huwa wahako serious, kwa mfano saa hizi badala ya kufanya kazi, mko mnachat, baada ya miezi miwili, una mimba. Leo mtoto anaumwa, kesho kafa bibi yako, kesho kutwa unaenda ngomani, mara unasikia kichefu chefu. All in all, tutambue kuwa muajiri anawajibika kufanikisha kazi na sio kubalance jinsia.
   
 11. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wewe peke yako hapa ndio umeongea kitu cha maana. Watu hapa wanafikiri kuwa MAKAMPUNI YAPO ILI WAO WAAJIRIWE WALIPWE MISHAHARA wkt uhalisia ni kwamba makampuni yapo ILI YAZALISHE YAPATE FAIDA NA YAENDELEE KUWEPO. Tatizo letu watanzania ni kuwa hata wanaume, tunafikiri mtu akianzisha kampuni yake anaanzisha ili sisi tupate ajira. Hakuna anayejua kuwa inaanzishwa kwa lengo la kuzalisha na hii ndio maana mara nyingi watu hawajali wala kuona vibaya kulipwa hata kama wanapafom below standad.

  Ukiangalia maneno yalioandikwa hapa, utaona dhana ya uwajibikaji haieleweki kabisa. Hona huyu anasema ujinga gani?
  Yaani mtu unakuwa haupo serious kiasi unaamini mwajiri afurahi wewe kuwa mjamzito kila mwaka! Hivi kweli jamani kama tuna akili hata kidogo, nikuajiri uwe unauza dukani kwangu, halafu miezi 4 kati ya 11 unakuwa nyumbani unanyonyesha halafu mimi biashara yangu inakuwaje?
   
 12. m

  mamabaraka Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ofisi nyingne inaeleweka kuwa matenity leave inatolewa baada ya miaka mitatu, lakin kwa wanaume mnaochangia mada pia muangalie mkeo anafukuzwa kazi kisa mjamzito. Tena ofisi nyingne washenzi kweli ukigundulika una mimba unapewa barua ya kufuzwa kazi. Kama tatizo ni productivity itaftwe another alternative kuwasaidia kina mama. Kama anapata mimba kila mwaka apewe likizo bila malipo, lakin kama mtu anafata utaratibu inakuwaje kumwachisha kazi? Na saa nyingine mama wa watu ni mchapakazi kweli kweli? Its not fair.
   
 13. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio mke wa nani, tatizo ni nini mwenye kampuni ametarget wakati anaanzisha kampuni yake. Wewe mwenyewe ni mfano wa mtu asiyejua mshahara unatoka wapi. Unaposema fulani apewe likizo bila malipo, kazi za huyo fulani anayepewa likizo bila malipo anazifanya nani? Lets be realistic, the business is about bargaining and not begging. Hakuna kitu kama kuwasaidia kina mama kwenye accounts.

  Unashauri waajiri wawe flexible kwenye attendance bila kujali mishahara inatokana na uzalishaji. Your only alternative ni kumpa likizo bila malipo, kwa hiyo aajiriwe mwingine au? Wanawake wawe na shughuli za kufanya. Hata haukuwa mpango wa Mungu kumu- engage mwanamke kwenye direct production na ndio maana tuna complications za namna hii. Unaweza ukaniona mbaya kwa ninayoyasema lkn zingatia uhalisia huu.

  Piga hesabu una genge lako la kuuza nyanya na vitunguu. Wakati una mimba, tayari una mtoto mwingine mdogo wa miaka miwili. Kwa wingi wa kazi za nyumbani unashindwa kwenda sokoni kuchukua bidhaa za gengeni, kwa hiyo biashara inaanza kusuasua na baadaye unaamua kuacha kabisa. The same inatokea kwenye makampuni tunayofanya kazi. Kinachotufanya tusione ni kwa sababu sisi hatuko responsible na hasara wala faida ya kampuni, mwisho wa mwezi unapokea mshahara kama umefanya kazi au hujafanya, hilo hujali. Na ndio maana si ajabu ukakuta wanawake wanapiga story huku teller desk za benki zimejaa foleni na hakuna anayejali. Siwalaumu lkn kubalianeni na maumbile na mipango ya Mungu.
   
 14. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kampuni ya mumeo ikifa kwa kuwa ameajiri wanawake na wako maternity utampigia makofi kwa kuwajali wanawake au utaanza kulia kuwa nyumba yenu mlioweka dhamana kupata mkopo wa kuanzishia hiyo kampuni itauzwa?

  Business ni kitu serious, hakiongozwi na hisia.
   
 15. p

  priscilla Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mmenikatisha tamaa mm nimeolewa nina mwaka ss na ndo nimepata ujauzito na nimeomba kazi kwenye kampuni fulani na wameshanifanyia interview na subiri majibu je kama wakinipa kazi na badae wakajua mm ni mjamzito watanifukuza?jamani naombeni maoni yenu am scared
   
 16. m

  mamabaraka Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mmenikatisha tamaa mm nimeolewa nina mwaka ss na ndo nimepata ujauzito na nimeomba kazi kwenye kampuni fulani na wameshanifanyia interview na subiri majibu je kama wakinipa kazi na badae wakajua mm ni mjamzito watanifukuza?jamani naombeni maoni yenu am scared. pole sana dada prisca ni kweli hilo linaweza kutokea au lisitokee inategemea bosi wako atakuwaje, du it pains. Jamani kwa wakaka mnaochangia mada jaribu kufikiri wewe binafsi ungekuwa mwanamke umesomeshwa kwa tabu na mzazi mkulima unafanya kazi zako vzr then unafukuzwa kisa tu ni mchamzito. Fikiri ingekuwa wewe.
   
 17. p

  priscilla Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante mamabaraka naimani Mungu atanihifadhi maana ndo bado changa si rahisi mtu ajue,lol kukaa tena miezi tisa bila kazi na mm nimezoea kufanya kazi sintaweza,ila maoni ni mazuri maana kila mtu ana upeo wake
   
 18. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wakati unaona kwa upande huo, hebu fikiria mfano wa huyu anayeingia kazini na mimba tayari. Sio kwamba nina chuki na wanawake, lkn umeshaona shida atakayopata muajiri ikiwa huyu Priscilla ni secretary au typist? Unaingia kazini leo, baada ya miezi mi4 unaenda maternity ambako unakaa miezi kadhaa. Nani anafanya shughuli zako? UZAZI WA MPANGO UFANYIKE KWA KUZINGATIA MAJUKUMU PIA
   
 19. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,125
  Likes Received: 3,312
  Trophy Points: 280
  Lakini kuna ukweli ndani yake.
   
 20. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kweli kazi ipo kwa akina mama.Mimi ninamfano hai wa dada mmoja tulimujiri katika idara ya IT kwa ajili ya kazi maalum lakini tumeishia kupoteza hiyo project.Alianza mara naumwa tumbo mara akapata mimba baada ya hapo akapewa bedrest ya miezi sita plus likizo ya uzazi siku 84 mwaka tayari.Yaani tumepata hasara kwa ajili ya mtu huyo.Sasa fikiria kama ungekuwa nao kama hao watano au kumi shirika kwisha kazi yake.
   
Loading...