Je, ni sahihi kwa Mtangazaji wa TBC Taifa kutamka haya Hewani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
"Tafadhali ewe Mtanzania fanya kila uwezalo na kama una Babu yako Mganga wa Kienyeji mwambie asaidie kwa Ndumba ili Taifa Stars iifunge Zambia na hata tulicheza na Congo DR tushinde pia"

Kuna Mtu miaka ya nyuma aliwahi kuniambia kuwa kama kuna Media ambayo Watumishi wake Wanarogana / Wanapigana mno Misumari ni TBC nikambishia Ila baada ya Kumsikia Mtangazaji yule kila mara akihimiza Ulozi na Uganga sasa GENTAMYCINE nimeamini rasmi.

Kwa ninavyowajua Wakongo leo labda tu Turoge tupunguze Magoli, ila tusipoteze muda kabisa Kuwaroga ili tuwafunge kwani kama ni Ndumba (Kikongo wanaita KINDOKI) wao ndiyo Walimu na Congo DR ndiyo Makao Makuu yake.

Tuendeleeni tu na Hesabu za Vidole.
 
Yupo sahihi ndo maisha ya waswahili waliowengi, Ukiona jamii inaamini sana katika nguvu za kiroho basi ujue si Mungu tu bali hata za shetani zinatumika.

Me naomba sana tupigwe Mkono mtungi.
 
Ni sahihi kabisa kwa mtangazaji kutamka hayo maneno, na huyo mtangazaji anajitambua kuliko unavyofikiri au wengine wasiotambua ukweli wanavyofikiri.

Amini nawaambia leo Taifa Stars tutashinda.
 
Back
Top Bottom