Si haki, ila wakati mwingine mazingira yanasababisha hali hii. Maisha ni magumu kwa mwananchi wa kawaida, wengi wanatafuta kwa jasho na kujinyima sana, shida inapotokea kibaka akakupora kiulainii chochote chako ambacho bila shaka kitakupa usumbufu kukipata tena lazima hasira ziwake. Hawa vibaka nao wajifikirie sana, kuhatarisha maisha kwa simu/pochi, etc. etc. - kijana mzimaa, huna kasoro yoyote mwilini kutegemea kupora watu mtaani ndio yawe maisha yako, haifai.