Wa-Tanzania Kwa Kupenda Kujichukulia sheria Mikononi Mwao hatari sana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
HIVI HII NI HAKI?




Kutokana na hasira za watu hao walioamua kujichukulia sheria mkononi,sidhani kama alipona kwani baadaye walitokea mgambo wa jiji na kumuokoa, Wakati wakielekea katika kituo cha Polisi cha Karume Kibaka huyo alianguka na kupoteza fahamu kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi kichwani.


DSC_0435.JPG



Soma Zaidi »
 
Mawe haya wanastahili wezi wa Account ya ECRO sio huyo mkwapua chain
 
Watu wanahangaika na kibaka hapo, badala ya ku_deal kisawa sawa na "waizi" wa fedha za ESCROW..Kuliko kum_terminate kibaka si bora kuwa_assassinate watu wawili katika ile list.
 
Waseme tufanye tunachotaka kuwafanya ndio watatujua sisi kina nani tulivyo na usongo nao.
 
Polisi wamekuwa hawafany lolote wanakula na vibaka, na sheria haifuati mkondo ndio maana raia wamefikia hivyo...ni kuchoshwaa...

Wengi tunaibiwa ukimkamata mtuhumiwa kesho yake unamuona nje...roho iliniuma sana sitokaa nisahau..






HIVI HII NI HAKI?




Kutokana na hasira za watu hao walioamua kujichukulia sheria mkononi,sidhani kama alipona kwani baadaye walitokea mgambo wa jiji na kumuokoa, Wakati wakielekea katika kituo cha Polisi cha Karume Kibaka huyo alianguka na kupoteza fahamu kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi kichwani.


DSC_0435.JPG



Soma Zaidi »
 
Si haki, ila wakati mwingine mazingira yanasababisha hali hii. Maisha ni magumu kwa mwananchi wa kawaida, wengi wanatafuta kwa jasho na kujinyima sana, shida inapotokea kibaka akakupora kiulainii chochote chako ambacho bila shaka kitakupa usumbufu kukipata tena lazima hasira ziwake. Hawa vibaka nao wajifikirie sana, kuhatarisha maisha kwa simu/pochi, etc. etc. - kijana mzimaa, huna kasoro yoyote mwilini kutegemea kupora watu mtaani ndio yawe maisha yako, haifai.
 
vibaka wanakera sana, wanaweza kukutoa roho hata kwa laki moja; na wao wanapaswa kufuata sheria pia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom