Wa kulaumiwa CCM ni hawa

Wa kulaumiwa CCM ni hawa

Papa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
2,023
Reaction score
2,218
Wana CCM tusitafute mchawi wa kwanini tunendelea kupoteza. Waliotuponza ni hawa:
  • Anna Makinda - Spika aliyehakikisha bunge linalinda masilahi ya serikali kwa kuzima hija za msingi na kuwaksirisha wapiga kura wetu.
  • Wabunge wa vitu maalum wa CCM kwa kura zao za ndiyoooo kwa maamuzi yasiyona maslahi kwa taifa. zilikera sana wananchi.
  • Taasisi ya rais na rais mwenyewe kwa kupuuza maazimio ya bunge yaliyomuhitaji katika utekelezaji wake.
  • Samwel Sitta na team yake akina Lukuvi na Wasira kukanyaga maoni ya wananchi ya katiba mpya.
  • Majina ya mfukoni ya ugombea urais
 
Mkuu, kwani ndugu yenu Lowasa si kahamia UKAWA? Sasa si muende kuungana naye kuliko kujipakazia kuwa wana ccm??
 
Muendelzo wa mtindo wa Kisultani wakurithishana madaraka nao pia ulichangia.
-kikwete, Riziwani, Salma ( baba mwenyekiti, mtoto mbunge na mama mjumbe wa NEC)
- Nape = mtoto wa Moses Nnauye
- Kippi Warioba= mtoto wa Joseph Sinde Warioba
- Vita kawawa = mtoto wa Rashid Kawawa
-Maria sarungi= Mtoto wa philemon Sarungi
-Hussein Mwinyi= Mtoto wa Ali Hassan mwnyi
- Mahmoud Mgimwa= Mtoto wa mgimwa aliekuwa waziri wa fedha
-Anna malecela= mke wa Samuel malecela
-Magret Sitta= Mke wa Samuel Sitta.

hao niliowataja na wengine tele tu ni mfano halisi wa Usultani wa CCM ni Kuendeleza Ufisadi wao
 
CCM wote wajilaumu kwa madudu waliyoyafanya.

Kuanzia mjumbe wa nyumba 10 hadi rais wa jamuhuri ya muungano.
 
Iwapo fisiem watafanikiwa kushinda uchaguzi huu sijui watafanya muujiza gani kurdisha imani za watz maana Magufuli ametwishwa mzigo mzito sana utadhani ni maraika ndani ya ccm
 
The biggest mistake ever ilianzia na sitta kwenye bunge maalum la katiba, maamuzi mabaya ya akina sitta ndio yaliozaa zimwi linaloitwa ukawa. Weekend moja wakati bunge la katiba linaendelea nilipanda ndege kuelekea Zanzibar kutoka dar, mbele yangu walikuwepo aliekuwa mwanasheria wa Zanzibar na waziri wa serikali ya Zanzibar mwanasheria yule alimsimulia waziri madhara watakayopata ccm pindi wakilazimisha katiba wanayotaka wao, naapa kwa jina la Mungu yote aliyoyasema mwanasheria yule ndio yanayotokea sasa, ccm wanalipa gharama kubwa sana kwa kosa la sitta. Kwa uhasama uliokuwepo kati ya chadema na cuf isingekuwa rahisi vyama hivi kuungana na pasingekuwa na ukawa, lakini ona sasa
 
Iwapo fisiem watafanikiwa kushinda uchaguzi huu sijui watafanya muujiza gani kurdisha imani za watz maana Magufuli ametwishwa mzigo mzito sana utadhani ni maraika ndani ya ccm

Wapitie njia gani labda? Au washinde kwa kura zipi?? Ccm mwaka huu ishaishiwa pumzi inaelekea kufa tar 25
 
R.I.P fisiem,hizo push up tutakuwa tunaanda tamasha maalum la push up na kupiga tumba mgeni rasmi mh raisi Mamvi a.k.a Eddo ata padlock alcoholic analijua.
 
Wa Kulaumiwa ni Mkulu mwenyewe kwa kuleta mchakato feki wa katiba uliokuja kuzaa kirusi kinachoitwa UKAWA. Big mistake ilianzia hapa plus ESCROW saga.
 
Back
Top Bottom