vyuo vyetu vya elimu ya juu, digrii zake ni sawa?

Jahom

JF-Expert Member
Aug 26, 2008
351
32
Kwa sasa vyuo vilivyokuwa vinatoa advanced diploma (kiswahili chake kinanichanganya) sasa vinatoa digrii. Kwa kutaja vichache ni km vile Mipango Dom, IFM, CBE, DSA(TIA), n.k. Hofu yangu ni pale tutapoanza kuzibagua digrii hizi kwa vigezo vilivyotumika na Msemakweli. Hizi ni digrii za kweli? Mbona vyuo vyenyewe havijaitwa Universities? Tuelimishane
 
hiii kali, tusijejuta huko baade. lakini hata kuwa 'deemed university' bado! na sijui 'sirikali' inamipango gani
 
kwa sasa vyuo vilivyokuwa vinatoa advanced diploma (kiswahili chake kinanichanganya) sasa vinatoa digrii. Kwa kutaja vichache ni km vile mipango dom, ifm, cbe, dsa(tia), n.k. Hofu yangu ni pale tutapoanza kuzibagua digrii hizi kwa vigezo vilivyotumika na msemakweli. Hizi ni digrii za kweli? Mbona vyuo vyenyewe havijaitwa universities? Tuelimishane

tofautisha kati ya

vyuo na universities jibu unalipata rahisi
 
Diploma=stashahada
Advance Diploma= stashahada ya juu
Degree=Shahada
Post Graduate Diploma=stashahada ya Uzamili.
Masters degree= shahada ya uzamili
Phd=shadada ya uzamivu
kwani wewe mkuu degree unazipimaje?
 
chuokikuu ==university
vyuo vikuu==universities

Ans...................

Diploma=stashahada
Advance Diploma= stashahada ya juu
Degree=Shahada
Post Graduate Diploma=stashahada ya Uzamili.
Masters degree= shahada ya uzamili
Phd=shadada ya uzamivu
kwani wewe mkuu degree unazipimaje?
 
Diploma=stashahada
Advance Diploma= stashahada ya juu
Degree=Shahada
Post Graduate Diploma=stashahada ya Uzamili.
Masters degree= shahada ya uzamili
Phd=shadada ya uzamivu
kwani wewe mkuu degree unazipimaje?

Tatizo ni kutoa degree kwenye chuo ambacho si chuo kikuu baadae hata ajira zitazingatia ni wapi ulimaliza, badala ya fani gani ulisomea. Kwa taariifa kidogo nilinazo Staff hawajabadilika, ni walewale waliokuwa wanafyatua adv. diploma
 
Hizi digrii hatazitambuliki nje ya nchi (I mean if you are applying for job, or studies outside tz it might be difficulty for you to get a chance) because they are not accredited by TCU. Therefore they are just for home consumption. Do it at your own risk!!
 
mpangwa1,

kuna utafiti umefanya kwa hilo au walonga tu?

Mie nina jamaa yangu alisoma mzumbe ya zamani akapata advanced diploma...akaenda majuu akachukua masta yake moja kwa moja.

Mimi nadhani ukitaka kujua kama digrii ni ya ukweli ama la, kaa na wahitimu wa vyuo hivyo kisha uwatathmini kwa uelewa wao kitaaluma na kijamii.

kuna watu wamemaliza pale mlimani, lakini du... upeo wao ni haba sana.
 
Kwa sasa vyuo vilivyokuwa vinatoa advanced diploma (kiswahili chake kinanichanganya) sasa vinatoa digrii. Kwa kutaja vichache ni km vile Mipango Dom, IFM, CBE, DSA(TIA), n.k. Hofu yangu ni pale tutapoanza kuzibagua digrii hizi kwa vigezo vilivyotumika na Msemakweli. Hizi ni digrii za kweli? Mbona vyuo vyenyewe havijaitwa Universities? Tuelimishane

Nchi nyingi duniani kama si zote zina taasisi ambazo kazi yake ni kuratibu ubora wa elimu. Tanzania kuna Tanzania Commission for Universities - TCU. Moja ya kazi yake ni kulinda na kusimamia ubora wa elimu ya vyuo vikuu. Kabla ya Taasisi kuanza kutoa degree ni lazima itume maombi na kukubaliwa na TCU. Kabla ya kutoa kibali TCU ni lazima ijiridhishe na uwezo wa Taasisi husika katika kutoa degree. Mambo ambayo huangaliwa na TCU ni pamoja na mitaala, walimu idadi na sifa walizonazo, miundombinu eg madarasa, mabweni, maktaba, computer labs, science labs, health facilities, scheme of service, organizational structure, academic units etc.

Kimsingi degree zote zinapaswa kuwa sana lakini tatizo ni utekelezaji. Kuna baadhi ya Taasisi hasa za binafsi elimu ni biashara. Kila mwanafunzi anayeingia hapo ni lazima atoke na degree tena festi klasi. Utakuta darasa zima wana festi klasi na apa sekand. Hapo ndipo maswali ya ubora yanapojitokeza.
 
Back
Top Bottom