martial jb
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 864
- 1,464
Baada ya siku chache kupita toka bunge la TANZANIA chini ya spika Mh.Tulia Ackson Mwansasu liagize vijana kupokelewa vyuoni na kuanza masomo huku mchakato wa mikopo yao ukiendelea, limeonekama kupingwa na vyuo mbalimbali nchini na kuonekana kama limepotezewa.
Agizo hilo lililotolewa na spika wa bunge, ni kama limepotezewa na vyuo mbalimbali pamoja na taasisi za kielimu nchini. Ambapo vijana hao wameshindwa kupokelewa vyuoni pasipo kuwa na viwango vya fedha vinavyotakiwa na vyuo hivyo.
Vijana hao hasa wa mwaka wa kwanza wameonekana kulalamika na kuudhunika kutokana na hali halisi inayoendelea mpaka sasa, huku masomo yakiendelea vyuoni kwa wale waliolipia viasi hivyo vya pesa.
Baadhi ya vyuo Dar Es Salaam kama UDSM na Ifm wamekataa kabisa kusajili wanafunzi hao wapya huku wakilazisha kulipwa pesa ya awali ambayo si chini ya laki sita ili wanafunzi hao wapate kusajiliwa. Hivyo kuzua sintofahamu Kwa baadhi ya wanafunzi.
Ombi langu kubwa kwa serikali ni kuangalia upande huo wa vijana kwanza, kwani wanateseka ukizingatia masomo yanazidi kusonga mavyuoni. Serikali ifanye mchakato juu ya vijana hao kwanza na mambo mengine ndio yaendelee.