Vyuo vya watu wenye matatizo ya akili

Vyuo vya watu wenye matatizo ya akili

SakaroMbulu

Member
Joined
May 23, 2018
Posts
12
Reaction score
3
Habari wanajamii, nina mdogo wangu anaumri wa miaka 20, akili yake haiko sawa, kila chuo tukijaribu kumpeleka anashindwa,ameshamaliza course mbali mbali kama mapishi,computer na ufundi lakini bado hajui chochote, naombeni msaada kwa yeyote mwenye kujua chuo cha watu kama hao,iwe ndani ama nje ya nchi.
asanteni sana
 
Hapo kuna vitu viwili, unaweza kufafanua ili wadau waelewe zaidi nini cha kusaidia.

Ana mtindio wa ubongo au ni vile akifundishwa havingii kichwani?
 
huyo anahitaji maombi,
hebu jaribu kutafuta msaada wa kiroho na Mungu atamsaidia
 
mfungulie biashara ama shughuli yoyote ya kufanya,shule is not for everyone...I just discovered that,lol
 
Pole sana,Kuna chuo chao maalumu kule Yombo jaribu kumpeleka au pale pale mnazi mmoja ndani ya Halmashauri ya Ilala kuna chuo cha maendeleo ya wananchi naonaga waliopo pale ni walemavu na wenye mtindio wa ubongo jaribu kumpeleka
 
Mara nyingi matatizo ya ubongo huwa yanatibika kama hajarogwa.Mtafuteni daktari wa saikolojia au ubongo.then atawapa namna bora zaidi.

Kama mna uwezo wa kumpeleka chuo hata nje ya nchi maana yake mpo vema kiuxhumi.sasa mkimtibu akawa sawa kiakili itakuwa vema na atawashukuru sana.
 
Back
Top Bottom