Vyuo vikuu vya tanzania kumetokea nini? Mbona kimya?

OPORO

Member
Apr 22, 2012
59
14
Wana JF
Naomba kujua kwanini katika miaka miwili ya 2010/2011 vyuo vikuu vyote Tanzania vimekuwa kimya,hakuna mijadala ya wanafunzi kudai haki zao,hivi wote kwa sasa wanapata mikopo? wanaridhika na mfumo wa utoaji mikopo ya HESLB? Je,mfumo wa kulazimisha mtu kwenda kusoma chuo asichopenda kupitia TCU kwa njia ya CAS wameridhika nao?

Je,uonevu unaofanywa na vyombo vya dola hasa polisi kwa watanzania hawaoni? ,tulizoea kuona uezo wa kufikiri ukianza UDSM na kusambaa kwenye vyuo vingine,mbona kimya jamani?

Wadau kumetokea nini? UDSM,DUCE,UDOM,MKWAWA,AIA,TIA,IFM,DIT,DMI mmeridhika na hali iliyopo? je,mnajua maana ya kuwa msomi? jamani wanafunzi mtuangusha.

Mwenye sababu ya ukimya wote huu atujuze wadau
 
Kuna chuo kimoja hapo nasiki ni kama chekechea wanasimamiwa yani ukitaka kwenda nje lazima useme unakokwenda....mambo mengine tanzania yanastaajabisha
 
Ndudu oporo kwa kweli hitimisho lako ni batili sana. Ni nani aliyekuambia maandamano/mgomo ndio njia pekee wasomi wanayoweza itumia kudai haki zao? Ukiona kimya ujue wanaweza kuwa wanatumia njia nyinginezo ikiwemo mazungumzo/majadiliano.
 
Kuna chuo kimoja hapo nasiki ni kama chekechea wanasimamiwa yani ukitaka kwenda nje lazima useme unakokwenda....mambo mengine tanzania yanastaajabisha
Mzumbe University,
Upanga Campus kwa wasomao MBA.
Ila ni tabia binafsi ya Mwalimu Mmoja hivi, sio chuo kizima.
 
Nani kakudanganya kuwa Versity bila kunji mambo yanaenda? Soma historia ya vyuo vikuu tangu Karne ya 13 France, Egypt, kunji ndo lugha inayoeleweka kwa wale watumiao akili nyingi, nguvu nyingi na muda mrefu kutatua matatizo madogo madogo. Unapokutana na maprof & Ma dr wana-urgue na mwanafunzi ambae hana hata degree moja ni vigumu sana kufikia muafaka. Kunji halizuiliki ktk mazingira haya.
 
Back
Top Bottom