Mambo yanatisha mkuu.Tupe experience mkuu
Aiseee....mimi jaribu la kwanza tu ningeondoka......Pole sana rafiki..Mambo yanatisha mkuu.
Niliripoti kule ilikuwa siku ya ijumaa ili jumatatu nianze kazi ya kilichonipeleka. Nilipokelewa na mwenyeji wangu vizuri na kupelekwa mpaka sehemu ya makazi niliyokuwa nimetayarishiwa. Mwenyeji akanipa Dos & Donts za pale na jinsi ya kuishi na wenyeji.
Kikawaida siku za kawaida huwa nalala mapema kwa sababu huwa naamka alfajiri sana na tabia ya kufanya zoezi kidogo kabla ya kuanza siku. Nilipoamka mida ya saa kumi na nusu alfajiri nikasikia kama watu wanaongea hapo nje ya nyumba. Sikutilia maanani nikajua kumekucha pengine kuna watu wanaanza siku zao mapema pia. Nikajiandaa na kutoka nje nikakutana na giza kali sana. Sikufikiria chochote nje ya kawaida kwa hiyo nikaendelea zangu na mambo yangu. Nje sikukutana na mtu hata kidogo. Wakati narudi mazoezini huwezi amini nimerudi mpaka pale nilipofikia nikakuta hakuna jengo....mwanzoni nikajua labda nimepotea. Bahati nzuri nilitoka na kasimu kangu katochi...nikampigia mwenyeji wangu ambaye anaishi karibu na mimi. Alipofika pale na pikipiki kwa mujibu wake nilikuwa kama mtu niliyepoteza kumbukumbu. Akachukua funguo mkononi kwangu na kufungua mlango wa nyumba mpaka ndani. Siku yote hiyo jumamosi sikushinda vizuri kwa kweli.
Nikampigia simu Mzee wangu nikamuelezea hilo tukio. Akanipa maneno ya kiutu uzima...yeye ni mwenyeji na mzaliwa wa kanda ya ziwa. Akaniambia hapo kijana wangu kamatia maombi na msogeze Mungu karibu sana. Nikamuelewa....so nikaanza kufanya tafiti pole pole huku naendelea na shughuli zangu zilizonipeleka. Ndani kama ya miezi mitatu nikaanza kuzoea mazingira ya pale. Siku moja nimekaa na washkaji sehemu nikaona Mamba kwa mbali anakuja upande tuliokuwa tumekaa...cha kushangaza eneo hilo hatukuwa karibu na ziwa wala mto. Mamba alifika karibu kabisa kiasi cha futi 12 na nilipo mimi...lakini cha ajabu wale wenyeji wangu hawakuona kitu. Baadae nikajua huo ni aina ya Uchawi wanautumia sana kule kwa kuondoa uhai wa mtu. Unachukuliwa na mamba hata kama mmekaa watu 10...anakunyakua peke yako na ndio mwisho wako.
Ya mwisho kali iliyofanya nifunge virago. Ilikuwa siku ya jumamosi usiku...nilishtuka usingizini kama saa 8 usiku..nikawa naskia kelele kama watu wanafanya sherehe sebuleni kwangu. Nikavaa nguo nitoke...ile nafika sebuleni nakuta kweupee na kimya. Nikirudi chumbani kelele na party inaendelea. Nikasali zangu nikapanda kitandani nikalala. Aisee asubuhi yake ilikuwa jumapili nikakutwa nimelala kibarazani uchi wa mnyama kama nilivyozaliwa. Na walinikuta watu waliokuwa wanaenda kanisani....ndio kwenda kumuita mwenyeji wangu wakaja kuniamsha pale. Aisee nilipatwa na taharuki sana. Jumatano ya wiki iliyofuata nilikuwa Dar es salaam. Na sijawahi kurudi huko tenaaaa mpaka leo.
Haya mambo yapo...nilikuwa siamini hata chembe lakini ninakubali haya mambo yapo kwa kisa kilichonipata UKEREWE.
Asante sana rafiki. Si unajua sisi ambao hatujawahi kukumbwa na hii misukosuko huwa tunaona kila kitu kama utani. Mpaka hapo liliponifika hilo la kukutwa kibarazani mtu mzima Uchi wa Mnyama ...hapo ndipo nikasema hapana hapa kuna jambo.Aiseee....mimi jaribu la kwanza tu ningeondoka......Pole sana rafiki..
Ukerewe hawana lolote zunguka Tanzania hi ujionee nenda kuna sehemu inaitwa Nyasa karibu na Mbambabay mkoa wa Ruvuma,Ludewa ndani huko wanapima radi hadi za mia 5(ambako shoka iliungua mpini ukabaki),Tanga(pangani),Ngende(Mtwara) Makete ndanindani,Sumbawanga(kuna kijiji nimekisahau jina ambacho waliweka rekodi ya Mwewe kunyanyua ng'ombe alienona na rekodi Haijawahi vunjwa,Kigoma(Kibondo),Kyela mpakani mwa TZ na Malawi nk
duuu tuwainngize national teamhuko nyasa kuna watu huwa wanapiga football hatari sana usiku...ila juu ya maji ya ziwa Nyasa!
Acha kabisa hadi magari yanatembea juu ya majihuko nyasa kuna watu huwa wanapiga football hatari sana usiku...ila juu ya maji ya ziwa Nyasa!
Kigoma ukitembea kilometers chache tu unakutana na kichaa. Yaani huku vichaa wamefurika kuliko sehemu zote nilizotembeaMbona nasikia eti Kigoma ndio lango la mambo yetu haya nchini?
Bangi pia kama hujaizoea ina tabia ya kukufanya uone ndoto ulizoota ni uhalisia [emoji1] [emoji1] [emoji23]Mambo yanatisha mkuu.
Niliripoti kule ilikuwa siku ya ijumaa ili jumatatu nianze kazi ya kilichonipeleka. Nilipokelewa na mwenyeji wangu vizuri na kupelekwa mpaka sehemu ya makazi niliyokuwa nimetayarishiwa. Mwenyeji akanipa Dos & Donts za pale na jinsi ya kuishi na wenyeji.
Kikawaida siku za kawaida huwa nalala mapema kwa sababu huwa naamka alfajiri sana na tabia ya kufanya zoezi kidogo kabla ya kuanza siku. Nilipoamka mida ya saa kumi na nusu alfajiri nikasikia kama watu wanaongea hapo nje ya nyumba. Sikutilia maanani nikajua kumekucha pengine kuna watu wanaanza siku zao mapema pia. Nikajiandaa na kutoka nje nikakutana na giza kali sana. Sikufikiria chochote nje ya kawaida kwa hiyo nikaendelea zangu na mambo yangu. Nje sikukutana na mtu hata kidogo. Wakati narudi mazoezini huwezi amini nimerudi mpaka pale nilipofikia nikakuta hakuna jengo....mwanzoni nikajua labda nimepotea. Bahati nzuri nilitoka na kasimu kangu katochi...nikampigia mwenyeji wangu ambaye anaishi karibu na mimi. Alipofika pale na pikipiki kwa mujibu wake nilikuwa kama mtu niliyepoteza kumbukumbu. Akachukua funguo mkononi kwangu na kufungua mlango wa nyumba mpaka ndani. Siku yote hiyo jumamosi sikushinda vizuri kwa kweli.
Nikampigia simu Mzee wangu nikamuelezea hilo tukio. Akanipa maneno ya kiutu uzima...yeye ni mwenyeji na mzaliwa wa kanda ya ziwa. Akaniambia hapo kijana wangu kamatia maombi na msogeze Mungu karibu sana. Nikamuelewa....so nikaanza kufanya tafiti pole pole huku naendelea na shughuli zangu zilizonipeleka. Ndani kama ya miezi mitatu nikaanza kuzoea mazingira ya pale. Siku moja nimekaa na washkaji sehemu nikaona Mamba kwa mbali anakuja upande tuliokuwa tumekaa...cha kushangaza eneo hilo hatukuwa karibu na ziwa wala mto. Mamba alifika karibu kabisa kiasi cha futi 12 na nilipo mimi...lakini cha ajabu wale wenyeji wangu hawakuona kitu. Baadae nikajua huo ni aina ya Uchawi wanautumia sana kule kwa kuondoa uhai wa mtu. Unachukuliwa na mamba hata kama mmekaa watu 10...anakunyakua peke yako na ndio mwisho wako.
Ya mwisho kali iliyofanya nifunge virago. Ilikuwa siku ya jumamosi usiku...nilishtuka usingizini kama saa 8 usiku..nikawa naskia kelele kama watu wanafanya sherehe sebuleni kwangu. Nikavaa nguo nitoke...ile nafika sebuleni nakuta kweupee na kimya. Nikirudi chumbani kelele na party inaendelea. Nikasali zangu nikapanda kitandani nikalala. Aisee asubuhi yake ilikuwa jumapili nikakutwa nimelala kibarazani uchi wa mnyama kama nilivyozaliwa. Na walinikuta watu waliokuwa wanaenda kanisani....ndio kwenda kumuita mwenyeji wangu wakaja kuniamsha pale. Aisee nilipatwa na taharuki sana. Jumatano ya wiki iliyofuata nilikuwa Dar es salaam. Na sijawahi kurudi huko tenaaaa mpaka leo.
Haya mambo yapo...nilikuwa siamini hata chembe lakini ninakubali haya mambo yapo kwa kisa kilichonipata UKEREWE.
Kumbe ilifanyika tamasha la mashindano ya kichawi inaweza kuwa burudani sanaUkerewe hawana lolote zunguka Tanzania hi ujionee nenda kuna sehemu inaitwa Nyasa karibu na Mbambabay mkoa wa Ruvuma,Ludewa ndani huko wanapima radi hadi za mia 5(ambako shoka iliungua mpini ukabaki),Tanga(pangani),Ngende(Mtwara) Makete ndanindani,Sumbawanga(kuna kijiji nimekisahau jina ambacho waliweka rekodi ya Mwewe kunyanyua ng'ombe alienona na rekodi Haijawahi vunjwa,Kigoma(Kibondo),Kyela mpakani mwa TZ na Malawi nk
Lifanyike kwenye msitu wa mabwepande. Na wadhamini wawe wale jamaa wauza majeneza pale Muhimbili.Kumbe ilifanyika tamasha la mashindano ya kichawi inaweza kuwa burudani sana
huko sitakwenda tena aisee mauzauza hadi mchana ukiwa mgeni tu unafanyiwa mambo ya ajabu sanaUmesahau sehemu inaitwa UKEREWE...sidhani kama kuna sehemu ulizotaja hapo zinaingia. Nilienda kikazi hata sikumaliza muda wangu nikafunga virago.
Kumbe unapajua kwa mauzauza mkuu? Yaani ni hatari sana. Nashangaa kuna watu wanabisha na kupafananisha na sehemu dhaifu kichawi.huko sitakwenda tena aisee mauzauza hadi mchana ukiwa mgeni tu unafanyiwa mambo ya ajabu sana
Nafikiri kati ya Mzizi Mkavu au Mshana lazima mmoja awe Dean wa chuo piga ua galagaza.Huu ndo wakati wetu Wana jf wanaotoa mada za uchawi kupata ajira ya kufundisha, SIPATI PICHA INTERVIEWS ZA KUWAPATA LECTURE NA PROFESSOR WACHAWI zitakuwaje.