Vyuo vikuu vinasaidia kuharibu nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vikuu vinasaidia kuharibu nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chifunanga, Mar 28, 2011.

 1. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Title inaweza ikawa inatisha kidogo, lakini nadhani issue ya humu ndani sio kubwa sana, ila nadhani ni ya muhimu.

  Kwa mtazamo wangu, vyuo vikuu ikiwemo UDSM inasaidia kuipeleka nchi hii pabaya kutokana na wahitimu wake kuwa chini ya kiwango.

  Wahitimu hawajui kuandika CV na lugha ya kiingereza inawapiga chenga sana inangawa masoyo yote kuanzia form 1 mpaka graduation ni ya kiingereza. Hata essays wanazoandika vyuoni humo huwa za kiingereza, lakini mchukue graduate mmoja umwambie aandike utashangaa.

  Wengi wao wanaomba kazi halafu ukiwauliza, wanasema wako tayari kujifunza kazini....sasa kama upo tayari kujifunza kazini huko shuleni/chuoni ulikuwa unafanya nini?

  Wengi wanaomaliza kwenye vyuo hivyo ukiwauliza wanataka kazi gani, utasikia mara sijui administrator, mara human resource, mara ye mwanasheria.......sasa wewe una degree moja unataka kuwa administrator....kweli jamani?

  Halafu kwa nini wanafunzi wote wanasoma course hizo hizo tu?.....kwa nini kila mtu human resource au mwanasheria?....hakuna taaluma nyingine?

  Mi sijui huko vyuoni wanafundishwa nini.....kila siku kugoma kuomba mabumu yaongezwe, ila kama employer nimekuwa disappointed kuwa hakuna wa kuwaajili, na wanaoleta C.V huwa hawafai kabisa yani...

  Kuna wengine wadogo wa marafiki zangu, lakini naogopa kuwasaidia kwa sababu nitaumia mimi mwishowe.

  Naomba wanafunzi wa vyuo ambao bado hamjamaliza muwe makini na jinsi nchi yenu unavyoenda na vipaji gani vinahitajika zaidi....sio mnasomasoma tuu, kama vile shule ya msingi.

  Naomba walimu wa vyuoni mfundishe pia kiingereza, kuandika C.V. na jinsi gani ya kutafuta na kuomba kazi. Sio kila mtu ataweza kujiajiri, kwa hiyo wafundisheni hawa watu jinsi ya kutafuta kazi. Pia wafundisheni jinsi ya kufikiria nje ya box....dunia inabadilika kwa haraka sana, walichofanya wadada na wakaka zenu sio ndio na nyie mfanye hichohicho...wenzenu walizaliwa enzi ambazo hamna computer....siku hizi kuna google...mambo yamebadilika jamani.
   
 2. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
 3. C

  Chamkoroma Senior Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi Chifunanga let me be the 1st to answer your avatar, never in your life blame the children and not the family, the family always knows what happened in few years went off, mimi kama mwana wa jamvi hili nimepiga kelele sn kusema kuwa niujinga uliokomaa kusema kuwa tuendeleze uTelezi wa kiswahili ilimtuendelee kuteleza kwenye, maisha yetu, najisikia kulia kwasababu Waziri mwenye dhamana ndiye anayeweza ibadili TZ kutoka kwenye umbumbu wa kiingereza hata kuwa nchi inayofanya vizuri ki elimu, hata hawa Haki Elimu cjui nikazi gani wanayofanya, kubadili mfumo tulionao ndiyo ufumbuzi tosha uliobakia, kuanzia watoto wadogo hawa chekechea mpaka Universit kiwe ni kiingereza, nashangaa kuona kuwa Private schools kuwa zinafanya vizuri nakutoa watoto wenye uwezo kielimu wakatibaba ni boya anatoa vipofu wa midomo japo wanaona kwa macho.
  haiingii akilini kuona Seminaries wanaweza kufundisha kiingereza toka shule ya msingi lkn Serkali inashindwa na ujinga wanamna gani huu?
  Ugandashule nzuri zote ni za serikali na zinazo fuatanyuma ni private lkn TZ ni kinyume chake.
  tusiwalaumu Graduates, kwa kushingwa kuongea kizungu lkn kuandika wanajua, ndiyo mfumo Dume la faru, kamua watoto wawakubwa kusomea good schools lkn akina kajamba nanitupo cc wakati huo huo vyuoi hawaendi wao peke yao kwani ni wachache, cc tulio wengi tunamung'unya maneno wakati wao kwa faida yao kwa fedha zetu sote wanakuwa baora kuliko cc.
  I N A U MA S A A A A A!
  USIWALAUMU ILA NDIYO MFUMO WA KIPOFU KUKATAA KUONGOZWA AKIJIFANYA ANAWEZA KWANI NJIA ANAIJUA HAJUI MVUA YA JUZI IMEHARIBU NJIA AKIPITA NATUMBUKIA, AKICHEKWA ANONEWA NA KUSEMA MLIJUA HAMKUNIAMBIA, LKN UNASEMA TUENDELEZE KISWAHILI CHETU BANA, KWENYE MTANDAO WA FACE BOOK, I TELL YOU THAT, ALL OF THOSE THINKING THAT SWAHIL IS THE WAY ARE IGNORANT OF THINK, THAT BY YOUR ROD(FIMBO) YOU CAN FACE THE FATIC GLOBALIZATION.
  LET US BE AWARE ALWAYS ON OUR IGNORANCE DUE TO OUR ILTERATE LEADERS WHO SUPPORTS TO BE STEATING WHILE OTHERS ARE RUNNING,
  POOR OF US .
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nasita kuwatupia lawama wahitimu hawa moja kwa moja, zaidi nitawapongeza angalau kwa ku-strugle kuweza kupata concepts za taaluma zao husika. Ningependa tusiangalie output tu, tuangalie ubora wa elimu tangia shule za awali. Shule za awali ndiyo misingi ya mtaaluma huyu, kwasasa sinahakia kama serikali ilishapitia tena mitaala (curriculum) ya shule za msingi na sekondari pamoja na kupima ubora wake. Kwasasa tuna shule nyingi (primary/secondary) za private zenye mitaala tofauti na serikali, na zingine zimetoa products nzuri sana mpaka wanaongoza Chuo kikuu (mfano Salome Maro aliyeweza kuongoza 2010 kwa kupata daraja la kwanza (GPA 4.7) kwenye Bsc. Computer Science-UDSM). Je serikali imeshafanya jitihada za kuchanganua hii mitaala na kukubaliana na moja ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa wahitimu bora? Pili, walimu ni muhimu wawe wenye sifa nzuri kwenye taaluma zao na pia wapewe motisha ili waweze kujituma katika kazi yao. Leo hii watu wakifaulu vizuri hawapendi kwenda uwalimu sababu ya maslahi duni. Je, serikali haijaliona hili na kuweka motisha ili kuvutia watu waliofaulu vizuri kuingia kwenye fani hii? Nafikiri tatizo hili halitaweza kutatuliwa kama hatutaweka kipaumbele cha kutosha kwenye elimu.
   
Loading...