Hivi Waungwana niulize tu, UDSM ilianza na wahadhiri wangapi 'wenye qualifications"na je, the other scenario, Kama isingeanzishwa UDOM, hao wanafunzi almost 18,000 wangekuwa wapi sasa hivi given the current capacaity ya public universities, na ada 'za kuruka' za vyuo vikuu binafsi?Kweli kuna mtu angetegemea, as from 2007, chuo kiwe kimeshajitosheleza kwa wahadhiri wenye qualifications, madarasa pamoja na mabweni, maktaba, vitabu vya kutosha nk?Isnt it nice to start somewhere? Ninavojua mimi, kwenye chuo kikuu kuna mchanganyiko wa wahadhiri...kuanzia tutorial assistants hadi maprofessa. Kinachoonekana sasa hivi ni kwamba maprofesa wengi wanaelekea kustaafu na hili linasababishwa na sera ya serikali (au ya WB) miaka ya 90 kufreeze ajira. Sasa wakiajiriwa wahadhiri ambao watajiendeleza wakiwa tayari kazini, at the same time kukiwa na back up ya wahadhiri kutoka nje, kuna tatizo gani?Au tunadhani kuwa vyuo vikuu "vinashuka' tu kama mana jangwani, havi-evolve over time? Unapolinganisha kwa mfano UDOM na UDSM ambayo ilianza 1964, nadhani inakuwa sio fair ....vyuo vingine duniani mfano Cambridge ni vya tangu karne!