Vyuo vikuu kama shule za kata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vikuu kama shule za kata

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mweongo, Aug 25, 2010.

 1. m

  mweongo Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini watanzania hawataki kuongelea mambo ya msingi kwa undani. Mfano elimu ya chuo kikuu leo inafanana na ya shule za kata. wakubwa wanatamba majukwani wameanzisha vyuo vikuu vingi kama UDOM. lakini hawaoni matatizo yaliyopo kwenye vyuo hivyo.
  Hakuna vifaa,Hakuna Maprofesa,majengo hayatoshi. Watu wenye Masters ndio walimu ambao nao wamesoma kwa kuunga unga tu. vyuo vikuu vya namna hii vitatufikisha wapi.

  Mtoto kafaulu kwa kubahatisha darasa la saba halafu kaenda shule ya kata kafaulu kwa kukairiri kaenda chuo kikuu UDOM. Hapa kweli tutasema tumezalisha msomi wa kuiomboa nchi hii katika ulimwengu huu wa utandawzi, soko la pamoja nk. Tanzania inaelekea pabaya. lakini viongozi wetu wanafurahia sifa rahisi rahisi. Wanchi nao wamelewa fikra za kipumavu za zidumu fikra za mwenyekiti. Taifa hili linahitaji mwelekeo mpya . we are in wrong boat and wrong direction.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwenye red,
  Unless kama una maana tofauti na ile ya 'Vingi' nnayoifahamu mimi.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  MKuu heko kwa post yako! heri hata hao wenye Masters wanafundisha! kuna sehemu wanafundisha undergraduate/Tutorial Assistant ni aibu sana. Naongea kutoka moyoni, we are in wrong boat! kama hatutaki kubadilika tuendelee kulia na stress baada ya miaka mitano itayo tutakuwa tumepata akili kidogo, kwani hata sie tuliosoma tumejaa woga wa kutupwa. We have been trained/educated to say Yes everything hata kama tunao kitu hakina manufaa, tunalipa sisi wenyewe kodi lakini hatutaki kufuatilia zinatumikaje.

  Leo ninapochangia hii thread yako mkuu, ninaumia kila siku, afya yangu sina uhakika baada ya miaka kumi ijayo nitaweza kukaa na kuandika haya au ndo nitakuwa tayari nishapotea kwa sababu ya mazingira magumu/hatarishi ya sehemu nilizosomea kama shule ya mzingi nimelima saana nikiwa mdogo, A-level nilikosomea unaingia ****** ukiwa umevua nguo zote na kuziweka mbali, Chuo nilichosomea watu tunabebana/kulala mzungu wa nne. Hata kama ninapata mshahara, lakini watu hatujiulizi hivi ndo hiki nachotakiwa nipewe kulingana na kazi yangu na shule yangu, hakuna kubisha mtu kwani wengi wamesoma kwa kuiba iba kitihani so how can he/she challenge someone for the right things? Ni kuendeleza wizi tu.

  Achilia mbali na mazingira, walimu hawatoshi tofauti nilivyokuwa nategemea kabla sijajiunga na chuo kikuu kuwa labda kuna unafuu katika utoaji wa elimu, Loooo! unaweza kuchanganyikiwa.
  Vifaa vya kufundishia, ni afadhali na secondary za st Mary's. Hata kama kuna vifaa lakini watu wa kufundisha hawapo, kama wapo ni wale wa miaka mingi ambao wanasubiri kustaafu wala hawana cha kujiendeleza. Kwa mtaji huu tutakuja lini kurusha satelite yetu ya mawasiliano iliyotengenezwa pale moshi au pale Tabora au pale Nyumbu. Ni ndoto kama hatutaki kutoka machozi sasa na kuondoa uoga wa kutofanya mabadiliko.

  Vyuo vikuu vimejaa siasa hata pale ambapo hakutakiwi kuwe na siasa watu wanajibu kisiasa kana kwamba hawajui umuhimu wa hivyo taasisi. We are in wrong boat, sure changes should be now!
   
 4. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  nilishasema muda mrefu, UDOM NI bOMU LINALOKUJA KULIPUKA SOON, WALIMU WACHACHE AND PURELY UNQUALIFIED
   
 5. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,918
  Likes Received: 1,027
  Trophy Points: 280
  Ni mwanzo, mara nyingi mwanzo wa kitu chochote huwa mgumu, serikali kuanzisha vyuo vikuu haija kosea. Hiyo ni hatua ya kwanza kuwa na taasisi, halafu baadaye kuwa na walimu wenye sifa. Isingekuwa hekima (kwa mawazo yangu lkn) kusubiri kuwa na walimu wenye sifa, halafu ndiyo kuanzaisha taasisi. Hapa tulipo si pabaya, hayo ulioongelea hapo juu ni marekebisho tu, na si ya msingi, walimu watapatikana tu, na ndiyo maana serikali imeanza kuajiri ma-dr na ma-prof toka sehemu yoyote ya dunia.
  Ondoa shaka, Roma haikujengwa kwa siku moja, vivyo hivyo, vyuo vyetu havitaimarika kwa siku moja, ni mchakato. cha msingi ni kuwa na mipango na mikakati ambayo inazingatiwa na kufuatwa.
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  We ndo una matatizo ya kuelewa! Kufaulu si kwenda moja kwa moja mpaka PHD tu. We una mtizamo wa kizamani
   
 7. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii yote ni nchi kuto kujipanga ama watawala kutokua na uwezo wa kusoma nyakati. Nchi imejaa ubabishaji sana hii, hakuna jipya mtu anloweza kulifikiria litatokea baada ya lets say miaka ishirni ijayo, watu wanawaza kesho watakula nini tu. Unapokosa uwezo wa kujua mambo ya mbeleni kwa kuangalia yaliyopita na sasa ni ujinga mtupu. ndo maana nchi imeingia kwenye matatizo kama haya ya shule mpaka vyuo kuwa na uwezo mdogo wa kutoa quality education. Hili imetokana na serikali kushindwa kuweka mikakati endelevu toka miaka ya nyuma!! Vyuo vingi vinaibuka ka uyoga walimu hakuna unategemea nn sasa? tokea mwanzo serikali ingeboresha maslai ya Wahadhiri tusingekua hapa tulipo. :confused2:
   
 8. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,084
  Likes Received: 15,723
  Trophy Points: 280
  Mwenzangu hii habari yako imenifurahisha sana sasa naomba unisaidie. Mie nasoma TPSC DAR CAMPUS nina assignment yangu ya ku submit tarehe 30 Agosti, 2010. sasa naomba unisaidie majibu, maana umeonekana utakuwa msaada mkubwa sana kwangu ili niongeze course work japo ni nzuri

  swali ni liko hivi:

  Write SWOT analysis for higher learning institutions and suggest strategic objective that should be addressed so as to align curriculum with the economic demands in Tanzania and world at large.

  natanguliza shukurani zangu. endapo utakuwa tayari kunisaidia ndugu yangu na mwingine atakaye guswa basi naomba majibu unitumie katika e-mail addesses hizi: esther_machapo@yahoo.com, esta_venance@hotmail.com au estavenance@gmail.com simu zangu ni 0754 089 043 0789 089 043 na 0655 089 043

  Mungu awabariki wote watakaoguswa kunikomboa ili nijazie course work yangu.
   
 9. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  nimehitimu hivi karibuni unalosema ni kweli. Vyuo vimeanza kua hovyo kuliko nilivyodhani kabla sijajiunga na elimu ya juu. Hapo udsm japochou kikongwe lakini reference books ni haba usipime. Nakumbuka vitabu vinne vya uchumi tulikua tunagombania wanafunzi 800 kutoka bcom and economics degree. Vyoo havifai ni uti kila kukicha, mabweni hayatoshelezi, hela za mafunzo kwa vitendo hazitolewi kwa uwiano na kwa muda, vyumba vya mihadhara tumejazana hadi tunakaa chini, walimu wasio na teaching/delivering skills ndo wamejazana huku proferssors competent kama baregu wakiondolewa chuoni. Malazi duni, hata maeneo ya kufanyia discussion(vimbweta) vimevunjika and no replacement. Huku ndo kuboresha elimu inakojisifia serikali kweli?!!!
   
 10. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waliokimbilia huko na qualifications zao nao wamegeuka wabangaizaji na ...lickers
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa uchache nakubaliana na wewe kabisa.
  Lakini kuhusu qualificatrions najua wapo wenye qualification nzuri walioibwa kutoka UDSM, DUCE, UCLAS, MUHAS n.k. just to strengthen UDOM but weakening other Universities.
   
 12. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  mimi ni mmojawapo wa wanachuo UDOM ila ninijilaumu na kuilaumu nafsi yangu kwa kuwa UDOM kwani nilipata nafasi katika vyuo vitatu UDSM,SUA na UDOM nilishawishika kujiunga na UDOM baada ya kuelezwa na ndugu zangu na rafiki zangu kuhusu sifa za chuo hiki kumbe ni maneno ya kisiasa tu maneno matamu kumbe ubora hakuna kabisa, hii inatia uchungu kwa wapenda maendeleo, hali halisi ndani ya UDOM ukifika utalia
  1.hakuna uhuru wa kujieleza, udikteta na u ccm umeezidi, ukitoa wazo zuri wanafikiri wewe ni mwana chadema na unatafutiwa zengwe kufukuzwa, wanachuo waliofukuzwa chuo mwaka juzi wengi ni wana chadema na wasiokuwa na kadi za ccm,kwani kipindi nimewasili chuoni katibu wa ccm kitivo cha elimu alinifuata anipe kadi ya ccm kwa madai kuwa wana ccm majina yao yanapelekwa kwa mkuu wa chuo na hawawezi kufelishwa au kufukuzwa ikitokea mgomo

  2.watu wanaosoma kozi za biashara hawakuwa na semina badala yake wamefundishwa kupitia lecture na walimu ambao wanasoma masters udom hii ni aibu kwani walikuwa wakilipua mfano mtu anafundisha hesabu kwa projecta hii inasikitisha

  3.kutumiwa kisiasa na wanasiasa kama shabiby, huyu alileta mashati ya ccm pamoja na magari kubebea wanachuo wakaandamane<mimi maandamano huwa ni hiari>kumpokea kikwete pamoja na kumchangia pesa ya kuchukua fomu huku vijijini kwao watu wakifa kwa njaa na shida ya maji hii itapelekea kutengeneza wasomi wapumbavu

  4.kutokuwa na haki sawa kisiasa mfano wana ccm huweka matangazo yao na kugawa kadi bila kubugudhiwa lakini kwa chadema ni kosa

  5.kukosewa kwa matokeo mara mkwa mara mfano leo mtu ana D anaenda kulalamika anapandiswa daraja au kushushwa kama akibishana na wakubwa
  6.mkuu wa chuo bwana kikula kutukana wafanyakazi kuwa wote wako kwa ajili ya dhiki kwani wamepeleka CV ila yeye kachaguliwa na raisi,pia kuwaita wanafunzi wana haramu baada ya kudai haki yao ya kupewa field
  7.chuo hakina mtaala wake kwani kina kopi UDSM na vyuo vya nje
  8.kuchaguliwa wanafunzi wa HKL kusoma kozi kama B.COM na BBA ambapo kimsingi hawakustahili kuzisoma
   
 13. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Hivi Waungwana niulize tu, UDSM ilianza na wahadhiri wangapi 'wenye qualifications"

  na je, the other scenario, Kama isingeanzishwa UDOM, hao wanafunzi almost 18,000 wangekuwa wapi sasa hivi given the current capacaity ya public universities, na ada 'za kuruka' za vyuo vikuu binafsi?

  Kweli kuna mtu angetegemea, as from 2007, chuo kiwe kimeshajitosheleza kwa wahadhiri wenye qualifications, madarasa pamoja na mabweni, maktaba, vitabu vya kutosha nk?

  Isnt it nice to start somewhere? Ninavojua mimi, kwenye chuo kikuu kuna mchanganyiko wa wahadhiri...kuanzia tutorial assistants hadi maprofessa. Kinachoonekana sasa hivi ni kwamba maprofesa wengi wanaelekea kustaafu na hili linasababishwa na sera ya serikali (au ya WB) miaka ya 90 kufreeze ajira. Sasa wakiajiriwa wahadhiri ambao watajiendeleza wakiwa tayari kazini, at the same time kukiwa na back up ya wahadhiri kutoka nje, kuna tatizo gani?

  Au tunadhani kuwa vyuo vikuu "vinashuka' tu kama mana jangwani, havi-evolve over time? Unapolinganisha kwa mfano UDOM na UDSM ambayo ilianza 1964, nadhani inakuwa sio fair ....vyuo vingine duniani mfano Cambridge ni vya tangu karne!
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kaizer,
  Ningependa kukujibu kuwa UDSM ilianza ikiwa na waalimu wengi tu wa kutosha kutoka Uingereza, Jamaica, na kwingineko waliokuwa well qualified. Wakati huo serikali ilijitahidi sana kuajiri the best minds there was in the academic world. Sizo hizi porojo za sasa za kujenga UDOM bila kufanya maandalizi stahiki na juzi namsikia mkulu wa CCM akijidai kuwa mwaka huu waalimu elfu 15 wanafuzu masomo. UDSM ya 60-70 ilikuwa an intellectual oasis.
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, lakini walau kwa mazingira ya wakati ule na UCHACHE wa wanafunzi, hilo liliwezekana.

  sasa hivi mazingira yamebadilika mno,wanafunzi wengi na mahitaji ni makubwa, sidhani kama serikali inaweza au inakuwa na ile willingness ya kuajiri hao walimu wa hivyo kutoka vyuo vya nje....hukawii kuambiwa kuwa wakulima wanahitaji pembejeo and the like.
   
 16. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe mwanafunzi unahitaji kusoma na kupata exposure kidogo. Maana nyingi ya tuhuma hazina msingi. Otherwise utakuwa miongoni mwa wale wanaopenda kulalamika bila sababu. Nikianza na
  8. Nani kakueleza kuwa HKL hawastahili kusoma Bcom na BBA. Kwani Bcom na BBA zipo kwa ajili ya akina nani? Kuna kitu gani huko mpaka wastahili watu fulani? Mbona Bcom ni kozi ya kawaida inayosomwa na mtu yeyote provided anaqualification na anaipenda.
  7. Umesema chuo hakina mtaala mara wanacopy kutoka vyuo vya nje na UDSM. Huo ndio mtaala wenyewe, na km wanaongezea na wa nje inakuwa inapendeza maana huenda walimu wenu wanaangalia mahitaji ya soko na ushindani baina ya vyuo.
  6. Wewe umesema Mkuu wa Chuo anatukana wafanyakazi woote. Huu ni uzushi hivi unadhani wafanyakazi wote hapo UDOM wanatukanika? Na pia mbona zipo mamlaka zinahusika kushughulikia hilo? Ameanza UDOM wakati yupo ardhi alikuwaje?
  5. Kuna process za appeal bwana mdogo na swala la kukosewa matokea si kigezo cha kusema chuo hakifai ingekuwa wanafake matokeo then tungesema vingine.
  4 na 3. Ni mambo ya kisiasa. Kuna haja ya kuyaaddress. Kuna mswada ulipiga marufuku mambo ya kisiasa. Hilo ni tatizo lakini kumbuka pia wewe hapo ni mtu mzima, ushiriki wa siasa ni hiari.
  2. Hoja ya kufundisha hesabu kwa projector inafanyika sehem nyingi duniani km hujamuelewa mwl uliza atakueleza. Hoja ya seminar ni uhaba wa walim, changanya akili fanya discussion.
  1. Upo kisiasa zaidi kuliko uhalisia
   
 17. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  sSi kweli kama ulivyosema kua vyuo vikuu ni kama shule za kata. unapaswa kujua kuwa Tanzania iko ynyuma kiasi katika kutoa elimu ya chuo kikuu ukilinganisha na nchi nyingi. Hivo ni jitihada za serikali kuongeza idadi ya wanafunzi katika ngazi hii. Katika kufanya hivo yapo matatizo yaliyojitokeza na hii si ajabu. Jambo la muhimu ni kujaribu kubainisha kasoro hizo na kushauri nini kifanywe sio kulaumu tu kila kitu. Ukumbuke kuwa wapo wanafunzi wengi wanaomba kusoma na wamekuwa tayari kuzikabili changamotoi wanazopata vyuoni. Popole na kwa mipango mizuri tutfika. Watu wanafanya utafiti katika eneo hili hawajalala. Basi Na tupaze sauti Zetu kwa watunga sera pia tuwape sauti wale wanotufaa ili mambo yaende vizuri. Asante
   
 18. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kaizer, we do not have to re-invent the wheel! Unataka Tanzania tuanze na First Generation Computer kwa sababu tu tulichelewa! La hasha, na usisahau jambo la msingi-- maadili ya kulewa yamedorora sana, kwa maana hakuna uangalizi wowote unafanywa kuona wale ambao bado hawajapata ujuzi wanafanya kazi yao na kuongoza jinsi ya kuiboresha!

  Nasema haya nikiwa na uchungu, maana kwa ajili ya siasa vyuo vikuu vimefurika, VCs vyuo vya uma ni wanasiasa (wengine wanajiita wenyewe ni wana-usalama) hawajui na wala hawataki kujua kinachoenedelea....TAs wanafundisha (oh TA hana Masters bado, ukiwa na Masters nzuri unapewa hadhi kufundisha Chuo Kikuu, inakubalika), hawa ni fresh kabisa tena wengine (kina mama nisameheni tu) wanapewa nafasi za uTAs kwa upendeleo lakini bado sio wajuzi walau kwa yale waliyoyasoma kwenye Bachelor.....

  Nahofu kama kweli vijana wetu wanaweza kuchuana na wenzao kwingine....zamani A-LEVEL WA TZ akiingia Urusi licha ya shida ya lugha alikuwa anatisha, siku hiziii mmhjhhhhh na Adv Dipl za Mzumbe, Ardhi wakati ule wakifika ngambo, walitisha sasa siku hizzzzz z sijujiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #19
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kwakuwa nyuma katika elimu ya chuo kikuu,je inahalalisha sub-standard?
  Tatizo: Uanzishwaji wa vyuo umefanywa kwa kisiasa, hivyo wataalamu hawashirikishwi. Mfano uanzishwaji wa chuo kikuu musoma cha kilimo,tujiulize kwanini SUA isiimarishwe kwa huduma ili kuchukua wanafunzi wengi zaidi! kwa vile ime jie establish. Hiki cha musoma kitatoa wapi walimu. SUA inaweza kwa vile tayari ni known worldwide.
  : Wasomi wetu i.e Don etc wamepoteza ''intellectual capacity''. Inakuwaje Prof. aamriwe kufundisha darasa la wanafunzi 2000 wanao ning'inia madirashani na asihoji ubora wa kile anachotarajia kukipata.!!! Yeye anajali mshiko na sabbatical basi.
  : Lakini ninyi mnaolalamika si ndio wale wale mnaojiita '' ccm tawi la vyuo vikuu''? mnapobeba mabango ya ccm imetimiza ilani, si pamoja na elimu bora?. Kwanini msitumie nguvu hizo kudai hali bora ya elimu, badala ya kuvaa magwanda na kutembeza fomu za mzazi mmoja anayejengea watoto wake future!
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Acheni watu wasome, hayo ndo maendeleo yenyewe. Nyie mnataka mwe na chuo kimoja kama cha enzi zile??

  Acheni hizo, na uhakika mtu aliyefika chuo kikuu hata kama kipo chini ya mwembe ana uelewa mkubwa wa kupambanua mambo kuliko yule wa LY.
   
Loading...