Vyuo vikuu bora Tanzania

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,983
Elimu ya Chuo Kikuu ni moja ya malengo ya wanafunzi wengi shuleni ambayo pia huhesabiwa kama moja ya kilele muhimu cha safari ya kielimu. Nchini Tanzania elimu imeganyika katika mtindo wa elimu ya awali, ya msingi, ya sekondari na ya chuo. Katika ngazi ya chuo nako kumegawanyika kwani vipi vyuo ambavyo hutoa vyeti na diploma na vipo vile ambavyo hutoa shahada (digrii). Hapa chini tumekuwekea orodha ya vyuo vikuu bora nchini Tanzania vinavyotoa shahada. Orodha hii imezingatia pamoja na mambo mengine idadi ya tafiti ambazo chuo hufanya kwa mwaka, uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi, machapisho (publications), heshima katika majukwaa ya elimu ya kimataifa pamoja na mambo mengine. Orodha hii ni kama ifuatavyo.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Hiki kiko jijini Dar Es Salaam na ndicho chuo kikongwe zaidi nchini. Kilianzishwa mwaka 1970.


2. Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)

Chuo hiki kiko mkoani Morogoro na kilianzishwa mwaka 1984. Kinatoa elimu hasa katika mambo ya tafiti za kilimo, chakula, mifugo na teknolojia katika mambo hayo.


3. Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU)

Kama ilivyo kwa SUA, hiki nacho kinapatikana mkoani Morogoro. Awali kilifahamika kama IDM-Mzumbe lakini kikapanda ngazi na kuwa chuo kikuu mwaka 2001. Kina matawi katika maeneo mbalimbali nchini.


4. Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Chuo hiki kinapatikana Jijini Dodoma na kilianzishwa mwaka 2007. Kama ilivyo kwa UDSM, SUA na MU, vyuo hivi vyote vinamilikiwa na serikali.


5. Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)

Chuo hiki nacho ni mali ya serikali, kinapatikana jijini Dar Es Salaam na kilianzishwa mwaka 1963.


6. Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU)

Chuo hiki kinapatikana jijini Dar Es Salaam. Kinamilikiwa na serikali na kilianzishwa mwaka 2007.


7. Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)

Chuo hiki kilianzishwa mwaka 2010, kiko jijini Arusha. Kinamilikiwa na serikali.


8. Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU)

Hiki kilianzishwa mwaka 1997, zamani kikiitwa Mikocheni International University. Umiliki wake ni binafsi na kinatoa hasa elimu ya tiba katika kuanzia stashahada hadi shahada ya uzamili.


9. Chuo Kikuu cha Tumaini (TU)

Hiki kinamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kilianzishwa mwaka 2007. Kinapatikana mtaa wa Ikungi Jijini Dar Es Salaam. Kina matawi katika maeneo mbalimbali nchini.

10. Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT)

Chuo hiki kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania. Kinapatikana mkoani Mwanza lakini pia kina matawi katika maeneo mbalimbali nchini. Kilianzishwa mwaka 2002.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema UDSM ndo kongwe zaidi na imeanzishwa 1970
Mbona hiyo MUHAS ni ya 1963 ipi kongwe zaidi sasa?
 
Mkuu umeanza vzur sana, ila nashindwa kuelewa kama nikweli unataka nyie tuu ( in case na wewe umo) mliosoma nje ya mipaka ndo muongee kwamba mmesoma vyuo. Ama nashindwa kuelewa kama nikweli unataka watu kutoka mataifa yote yasiyo kwenye hiyo list wahamie kusoma Misri na SA, that's too shallow.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naukitaka taarifa kamili ingia Google andika #league table

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa waandaji wa hiyo orodha tayari wameshakuambia ",,,Ranking aim to provide a non-academic League Table based on UNBIASED & VALID WEB METRIC!!

Hivi huoni hiyo orodha yako isiyo university ranking by ACADEMIC STUFF?!

Orodha ya MAGACHA hata kama inaweza isiwe sahihi kwa sababu haina data wala reference lakini amezungumzia suala la academic stuff pale aliposema "|Orodha hii imezingatia pamoja na mambo mengine idadi ya tafiti ambazo chuo hufanya kwa mwaka, uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi, machapisho (publications), heshima katika majukwaa ya elimu ya kimataifa pamoja na mambo mengine."

Orodha yake inanipa shaka kwa sababu sioni ni namna gani MUHAS inaweza kuwa chini ya Mzumbe & UDOM!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…