Vyuo na programu zilivyozuiliwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18

Nipo nacheka hapa... ligi ya vyuo bana ni hatari sana... sasaivi UDOM, SAUT, MZUMBE n.k ni vyuo vya kata... kweli UDSM Mungu anawaona asee... hamtaki competition kabisa eti...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu anataka kuapply kaniuliza sa sijaelewa ni tawi lake la mkoa ndo limefungiwa au ni chuo chenyewe. Nimepagawa
 
Hakitapokea wanafunzi mwaka huu, atafute kwingine. tembea wavuti ya TCU ujionee mwenyewe
 
Ndugu zangu Hivi Ni kweli kwamba Wale Wanaosoma comb ya CBG hawataruhusiwa Kusoma Course za Sayansi Chuo Kikuu ama hizi taarifa siyo za kweli!?
[HASHTAG]#Ufafanuzi[/HASHTAG] Jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Course za sayansi? Rekebisha swali lako, hiyo ni combination ya sayansi sasa kusema aliesoma hawezi kusoma course za sayansi ni swala ambalo haliwezi kutokea labda hadi hiyo combination ifutwe kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kusoma CBG hapo moja kwa moja utasoma course ambazo ni sayansi yani hata ukienda ualimu basi utakuwa mwalimu wa masomo ya sayansi.


Labda ulikuwa una maana ya kuwa ukisoma CBG huwezi kusoma sayansi ya udaktari(Medicine).
Embu eleza kwa kina maana hujaeleweka mkuu
 
Mkuu kusoma CBG hapo moja kwa moja utasoma course ambazo ni sayansi yani hata ukienda ualimu basi utakuwa mwalimu wa masomo ya sayansi.


Labda ulikuwa una maana ya kuwa ukisoma CBG huwezi kusoma sayansi ya udaktari(Medicine).
Embu eleza kwa kina maana hujaeleweka mkuu
Inasemekana kwamba kuna tamko limetoka kwamba mtu aliyesoma CBG hawezi kusoma Nursing, pharmacy, Doctor wa mifugo yani kama akisoma ni ENVIRONMENT HEALTH TU ndo itahusika kwahiyo inabidi hasome Education ama vitu vingine lkn kwa Pharmacy, Nursing haruhusiwi kusoma ndo sijajua hapo kama kuna huo ukweli ama laaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kusoma CBG hapo moja kwa moja utasoma course ambazo ni sayansi yani hata ukienda ualimu basi utakuwa mwalimu wa masomo ya sayansi.


Labda ulikuwa una maana ya kuwa ukisoma CBG huwezi kusoma sayansi ya udaktari(Medicine).
Embu eleza kwa kina maana hujaeleweka mkuu
Ndio inavyosemekana hata kusoma Pharmacy, nursing pia haruhusiwi yani course ambayo anaweza kusoma ni ENVIRONMENT HEALTH TU tofauti na hapo akasome Education sasa ndo sijajua Hiyo inshu ni kweli ama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kuulizana kwa muda sasa TCU wamefunguka na kutoa ufafanuzi. Tafadhali tuzingatie.

VYUO NA PROGRAMU ZILIVYOZUILIWA KUDAHILI WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18

1.0 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kuwa, mwezi Septemba na Oktoba mwaka 2016 ilifanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni. Ripoti ya uhakiki ilionesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo. Kwa sababu hiyo, Tume imesitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo vifuatavyo:

  1. Eckenforde Tanga University
  2. Jomo Kenyatta University, Arusha
  3. Kenyatta University, Arusha
  4. United African University of Tanzania
  5. International Medical and Technological University (IMTU)
  6. University of Bagamoyo
  7. Francis University College of Health and Allied Sciences
  8. Archibishop James University College
  9. Archibishop Mihayo University College
  10. Cardinal Rugambwa Memorial University College
  11. Kampala International University Dsm College
  12. Marian University College
  13. Johns University of Tanzania Msalato Centre
  14. Johns University of Tanzania, Marks Centre
  15. Joseph University College of Engineering and Technology
  16. Teofilo Kisanji University
  17. Teofilo Kisanji University Tabora Centre
  18. Tumaini University, Mbeya Centre
  19. Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)
2.0 Aidha, kutokana na mapungufu katika vyuo mbalimbali imeamriwa kwamba jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18. Kuona Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/18 tafadhali bonyeza hapa.

3.0 Aidha Tume inapenda kusisitiza kwamba, uamuzi huu hautawahusu wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika.

Imetolewa na:

Prof. Eleuther Mwageni

Kaimu Katibu Mtendaji

24 Julai 2017
View attachment 549527View attachment 549528
 
Nami naomba nisaidieni, hii Bsc molecular and biolechnology inahusika na nini? Vipi kuhusu ajira zake?
 
Nami naomba nisaidieni, hii Bsc molecular and biolechnology inahusika na nini? Vipi kuhusu ajira zake?


Mkuu swali gumu nitajaribu wengine wanaweza kuongezea au kukosoa. Hii ni molecular biology and biotechnology=maisha ya binadamu, wadudu (bacteria, virus, na vidudu vidogo zaidi), mimea, wanyama au chochote kinachoishi huwa yanakuwa yameandikwa (coded) ndani ya vinasaba vya DNA au RNA ambayo hupatikana ndani ya cells (chembe chembe za uhai) na vidudu ambavyo viko level ya cells au chini.

Hizi code husomwa na kutengeneza protein (kama enzymes) ambazo kwa mpangilio ambao uko kwenye hivyo vinasaba huwezesha cells kuizalia na kuwa cells aina tofauti na kufanya kazi tofauti mwilini. Hivyo hivyo kwa vidudu. Molecular biology ndo somo la kuelewa mahusiano ya hivi vinasaba na protein, vimeundwa vipi na vinafanya kazi gani na vinafanje kazi ndani ya mwili au cell au wadudu.

Hapa hukutana masomo ya cell biology, biochemistry, genetics, microbiology , immunology etc. Biotechnology ni kutumia elimu hiyo ya molecular biology kutengenza, kubadilisha,etc structure na kazi ya hivyo vinasaba na protein ili kuzalisha technology mpya kwa manufaa ya binadamu.

Technology kama za kutambua magonjwa, kutibu magonjwa, kutibu magonjwa, kuzalisha mazao ya aina fulani ambayo tunasema yako genetically modified (kama viazi vyenye carotene nyingi etc). Hawa ni wana science wa maabara. Ajira zaidi itakuwa kwenye utafiti (afya, kilimo, mifugo, wanyama pori, vyuo vikuu, ualimu)
 
Back
Top Bottom