Vyuo kufungiwa mnatutesa maskini

Vyuo kufungiwa mnatutesa maskini

Minicooper1

New Member
Joined
Feb 5, 2021
Posts
2
Reaction score
0
Wakuu natanguliza salaam.

Kiukweli hii tabia ya serikali kufungia vyuo hasa vya ngazi ya chini tunaoteseka ni sisi maskini. Unakuta mzazi amejichanga na kuweza kulipa ada ya chuo husika ndani ya mwezi mmoja chuo unasikia kimefungwa kwamba hakijakidhi sifa za kutoa fani husika ,mengi najiuliza inakuwaje mpka chuo kinasajiliwa na kuanza kutoa elimu husika alafu mwishowe kinafungwa kwa kukosa vigezo.

Je, au na usajili ni mambo kama ya kutafutiana leseni kwa wajomba zetu au ndugu zetu ilimradi tu mtu apate leseni mfano wa driving, namaanisha mtu anatafuta connections ya kupata vibali bila wahusika kujifanyia uchunguzi wa kina? Serikali tunaumia sana maskini.

Mfano hai kwa kanda ya ziwa Karagwe chuo cha afya (Karagwe Health College) chenye usajili REG/Has/146 kimefungwa wiki iliyopita na wanafunzi kuachwa pasipo kujua nini cha kufanya wakati intake wameingia mwezi wa 11 na kipo kwa zaidi ya miaka 3 au wenye chuo ni njia ya kutapeli watu make bila pesa mtoto haingii chuoni.

Serikali tusaidieni sisi maskini
 
Pole, kinaweza kikawa vizuri lakin kikafanya kosa kubwa, kinafungiwa tu, sometimes ni km ajali.

Inauma sana make watoto wanaachwa bila kujua cha kufanya pesa washakula watoto wanarud majumban na kuambiwa watafute vyuo vingine.
 
Inauma sana make watoto wanaachwa bila kujua cha kufanya pesa washakula watoto wanarud majumban na kuambiwa watafute vyuo vingine.
Watoto wanachuo na wewe unamuAdress mwanachuo kama mtoto huu sio ukomavu.
 
Back
Top Bottom