Kongole @ Smart911. MTU anataka kugida bia 5. Starehe!Maisha yapo kawaida tuu...
Enzi unazozungumzia nadhani ni baada au kipindi cha vita ya kagera, kama sijakosea... ndiyo nchi ilifunga mkanda na vyuma kukazika kisawa sawa...
Wanaolalamika vyuma kukaza bado hawajaona maana halisi ya vyuma kukaza, waache sasa wafanye haya maandamano wanayotaka kufanya alafu waone vyuma vitakavyokaza...
cc: mahondaw
Unajua nimekuja kuhitimisha kuwa sisi Watanzania tuko ‘soft’ sana, hususan nyakati hizi.
Unakuta mtu ana likitambi lake likubwa tu halafu eti analalamika vyuma vimekaza.
Watu wanakula bata kila kona huku wanalalamika vyuma vimekaza.
Wakati mwingine huwa nikiwaangalia naishia kucheka na kuwaambia ‘mnacheza nyie’.
Wahenga wenzangu watakubaliana nami kuwa kuna kipindi nchi hii vyuma vilikaza kweli kweli.
Enzi za miaka ya 80, hususan mwanzoni hadi katikati.
Enzi za maduka ya ugawaji. Watu mnajipanga mstari kusubiri kununua bidhaa kama sukari, unga, mafuta, mchele, miche ya sabuni, na vitu vinginevyo.
Bidhaa hizo za kila siku zilikuwa adimu. Sabuni za kuogea kama vile Imperial Lather na Palmolive zilikuwa hazipatikani kirahisi nchini. Kuzipata ilibidi mtu aende nje ya nchi kama Kenya au Ulaya huko. Watu tulikuwa tunaogea sabuni za Mbuni. Sabuni hiyo hiyo unaoshea vyombo, hiyo hiyo unaogea na hiyo hiyo unafulia nguo.
Hata dawa za mswaki zilikuwa adimu. Kunywa hata soda lilikuwa ni jambo la anasa. Watu mnaweza kupitisha hata miezi sita hamjanywa soda. Hata kula mkate wa siha ilikuwa nadra.
Kula pilau nako hivyo hivyo. Kula kuku pia.
Kunywa bia ndo kabisa! Kukaza huko kwa vyuma kulifanya pombe za kienyeji zipande chati, hususan wanzuki na kangala.
Sasa leo nikiona hivi vitoto vya miaka ya 90 vikijiliza liza eti vyuma vimekaza huku majumbani kwao kuna DSTV, maduka yamejaa kila aina ya bidhaa, vikienda baa vinakunywa Smirnoff, Savanna nini sijui, Hennessy V nini sijui, vinavaa nguo za madizaina [hata kama ni feki], yaani starehe mwanzo mwisho!
Nikiona hivyo huwa najiuliza sana...kama sasa hivi vyuma vimekaza...enzi zile vilikuwa vimefanya nini sasa!
Nani humu kaenda dukani akakosa Colgate, kwa mfano?
Nani hajanywa soda mwaka mzima? Nani hajanywa Fursana au Mo Orange kisa kashindwa kununua kwa sababu vyuma vimekaza?
Nani kaenda dukani kununua Rinju akakosa?
Tumekuwa watu walaini mno sisi. Watu wa kudekadeka tu.
Vyuma vilikaza miaka hiyo. Hakuna vyuma vilivyokaza miaka hii.
Acheni usleki mayai.
chief nakuhesabia! hili ni bandiko la kumi ndani ya siku nne seems like unatafuta attention au stress za credit card zinakupeleka mbio?
Natafuta ukuu wa wilaya.
Kweli kabisa watu walikua wanatafuta majani yakitoa povu tu wanafulia,hivi sasa wengi baba zao ndio walioangusha mashirika wanawakejeli wabongo kujidai wazalendo!
Hahahahaha na jamaa akasisitiza kwa mara ya kwanza kacomment sababu jamaa kaongea points sanaa hahahahaha, kama ndio hivi huyu hapaswi kucomment chochote tena maishani.Nayo ni hoja hiyo? aisee wamarekan walioishi maisha ya mwaka 1777 ni sawa na wa sasa?
Huu uzi braza The List ameuona lakini?Unajua nimekuja kuhitimisha kuwa sisi Watanzania tuko ‘soft’ sana, hususan nyakati hizi.
Unakuta mtu ana likitambi lake likubwa tu halafu eti analalamika vyuma vimekaza.
Watu wanakula bata kila kona huku wanalalamika vyuma vimekaza.
Wakati mwingine huwa nikiwaangalia naishia kucheka na kuwaambia ‘mnacheza nyie’.
Wahenga wenzangu watakubaliana nami kuwa kuna kipindi nchi hii vyuma vilikaza kweli kweli.
Enzi za miaka ya 80, hususan mwanzoni hadi katikati.
Enzi za maduka ya ugawaji. Watu mnajipanga mstari kusubiri kununua bidhaa kama sukari, unga, mafuta, mchele, miche ya sabuni, na vitu vinginevyo.
Bidhaa hizo za kila siku zilikuwa adimu. Sabuni za kuogea kama vile Imperial Lather na Palmolive zilikuwa hazipatikani kirahisi nchini. Kuzipata ilibidi mtu aende nje ya nchi kama Kenya au Ulaya huko. Watu tulikuwa tunaogea sabuni za Mbuni. Sabuni hiyo hiyo unaoshea vyombo, hiyo hiyo unaogea na hiyo hiyo unafulia nguo.
Hata dawa za mswaki zilikuwa adimu. Kunywa hata soda lilikuwa ni jambo la anasa. Watu mnaweza kupitisha hata miezi sita hamjanywa soda. Hata kula mkate wa siha ilikuwa nadra.
Kula pilau nako hivyo hivyo. Kula kuku pia.
Kunywa bia ndo kabisa! Kukaza huko kwa vyuma kulifanya pombe za kienyeji zipande chati, hususan wanzuki na kangala.
Sasa leo nikiona hivi vitoto vya miaka ya 90 vikijiliza liza eti vyuma vimekaza huku majumbani kwao kuna DSTV, maduka yamejaa kila aina ya bidhaa, vikienda baa vinakunywa Smirnoff, Savanna nini sijui, Hennessy V nini sijui, vinavaa nguo za madizaina [hata kama ni feki], yaani starehe mwanzo mwisho!
Nikiona hivyo huwa najiuliza sana...kama sasa hivi vyuma vimekaza...enzi zile vilikuwa vimefanya nini sasa!
Nani humu kaenda dukani akakosa Colgate, kwa mfano?
Nani hajanywa soda mwaka mzima? Nani hajanywa Fursana au Mo Orange kisa kashindwa kununua kwa sababu vyuma vimekaza?
Nani kaenda dukani kununua Rinju akakosa?
Tumekuwa watu walaini mno sisi. Watu wa kudekadeka tu.
Vyuma vilikaza miaka hiyo. Hakuna vyuma vilivyokaza miaka hii.
Acheni usleki mayai.
We ulikuwepo?Mwaka 1986 hakukuwa na vita na ugawaji ulikuwepo.
Kama ulikuwepo unasubir nini kufa?We ulikuwepo?
guilty are afraidMaisha yapo kawaida tuu...
Enzi unazozungumzia nadhani ni baada au kipindi cha vita ya kagera, kama sijakosea... ndiyo nchi ilifunga mkanda na vyuma kukazika kisawa sawa...
Wanaolalamika vyuma kukaza bado hawajaona maana halisi ya vyuma kukaza, waache sasa wafanye haya maandamano wanayotaka kufanya alafu waone vyuma vitakavyokaza...
cc: mahondaw
mkuu hii mijitu n bogus kbsmkuu naona mabandiko yako, unajitahidi kutumia nguvu kubwa sana kudhihirisha serikali ya ccm chini ya raisi JPM mambo yako poa tu ajira zipo, maisha hayana gharama, uhuru wa maoni upo, demokrasia ipo, yaani kila kitu kipo, sera za ccm zinatimizwa zote tena kwa wakati n.k.
inahitaji kujitoa akili ili mtu usome na kuelewa unachokipigania hivi karibuni kupitia sredi zako uchwara zenye ukakasi mwingi... kama wewe unapata milo mitatu kwa siku na ukakula hizo unazoziita bata sio wote wako hivo...
Sahihi kabisa mkuu! Eti jitu linakuja kulinganisha enzi hizo na sasa!Kipindi hicho viuma vilikuwa na full greese shida ilikuwa bidhaa maduka hayakuwepo kila bidhaa kwenye maduka ya ujamaa soda unapanga mstari kupata sasa bidhaa zipo madukani shida ni pesa ya kufanyia manunuzi