Vyombo Vya Habari Vya Tanzania, Havina Uwezo wa Uchambuzi wa Habari, News Analysis-Jicho Letu

kweli sijaona substance toka kwa Moses zaidi ya misamiati ya kingereza uchumi ambayo ilikuwa diaconected na maada,binafsi nimeona huyo Moses ameharibu flow nzuri ya Mansoor.ningewaomba Star tv wairudio maada hii.ni kitu mhimi sana media wajue sis walaji tunataka zaidi ya kuhabarishwa.habari tunakuwa tumeshazipata toka kwa social media kabla ya tv na magazeti.so mostly wanafanyaga repeatition ya the same contents.

Acha kufanya Watu wajinga na labda ukidhani humu JF kuna Watu wa ' hovyo hovyo ' Mkuu. Ukweli ni kwamba unamchukia Moses Mathew kwakuwa inajulikana ni mwana CCM na anafanya katika Gazeti la Serikali la Daily News na unamkubali na kumpenda Mansur Jumanne kwakuwa inajulikana ni ' Mwanaharakati ' halafu ni mwana CHADEMA mzuri hivyo anakukosha kwakuwa unafanana nae Kiitikadi. Tanzania itapiga hatua tu pale ' Unafiki ' huu wa aina yako utapungua au kuisha kabisa.
 
Wanabodi,

Kama kawaida ya Jumamosi asubuhi, Star TV, kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, leo, kipindi kimeiponda media ya Tanzania kuwa vina uwezo duni wa kufanya news analysis, kazi kubwa media ya Tanzania inayofanya ni kuhabarisha tuu jamii kuhusu matukio, lakini hakuna media zinazofanya news analysis kupitia kitu kinachoitwa interpretative journalism, kuwaeleza wasomaji, watazamaji na wasikilizaji kufanya evaluation ya hizo habari zina maana gani kwa taifa letu.

Wakatolea mfano mabadiliko ya baraza la mawaziri, yaliyofanyika hivi karibuni, media zote zimeishia kuhabarisha tuu fulani na fulani wameteuliwa, lakini hakuna media iliyofanya any news analysis, kuwaeleza Watanzania, what does that mean.

Endelea kufuatilia.

Paskali
Mayalla, nadhani kuna mapungufu makubwa kwenye tasnia ya habari hapa Tanzania. Upungufu ambao hauhitaji kuwa mwandishi wa habari kuubaini. Na hili ni jambo ambalo linanitia hofu sana.
Magazeti yetu nayaripoti tu, lakini kibaya zaidi yanaripoti baadhi tu ya taarifa, hasa zile zinazowafurahisha baadhi ya watu.
Magazeti yetu yanaripotu tu, lakini kibaya zaidi yanaripoti kiushabiki, eg. Jana nilisoma gazeti moja limeandika " kibano kingine kwa wapinzani chaja"
Vyombo vyetu vinapopata nafasi ya kuongea na viongozi wetu vinauliza maswali ya kuwajenga tu, hawaulizi critical questions ambayo yatajibu challenges zetu.
Watu wenye mawazo tofauti hawapewi nafasi kwenye vyombo vya habari hasa tv kama inavyostahili. Nakumbuka miaka ya nyumba tulizoea kuwaona watu kama Dr Slaa kwenye tv.
Kinachonitia hofu zaidi ni kuwa vyombo vyetu vya habari vingi hapa Tz vinajaribu kuzifinyanga bongo zetu ili wote tufikirie kwa namna moja tu! Nadhani hawajui the friend to all is the friend to none
 
Mkuu Mromboo, kwenye topic hii, kichwa ni Mansoor, Moses Methew kwenye topic hii ni hakuna kitu, ni mtupu, mweupe kabisa!.

P.
Mkuu Pascal Mayalla,tafadhali mshauri rafiki yako Dotto asiwe anamualika huyo Moses Mathew,maana sisi watazamaji hakuna chochote tupatacho/tunufaikacho toka kwake. Ni mtupu wa kupindukia.
 
Mimi binafsi ninachokiona kwa kizazi cha sasa katika uandishi na utangazaji ni UVIVU katika kusoma habari na taarifa mbalimbali zenye kutanua Uwezo wa ubongo.

Leo umezungumzia baraza la mawaziri ni kitu kikubwa saana ktk nchi , lkn wakati mwingine utakuta mtangazaji anazungumzia jambo dogo tu lkn utamsikia akisema "hili bwana Fulani ngoja nikitoka hapa ntalitafutia jibu " sasa unajiuliza hivi mtangazaji jambo hili alilijua atakuja kuliongelea ila hakufanya maandalizi yoyote ya kujiongeza hapa na pale.

Sababu nini? Kwangu mm sababu kubwa tecnolojia imeharibu wengi watu wanapenda kusoma habari fupifupi, watu wengi hasa watangazaji na waandishi wa vyombo vya hbr hivi sasa wanapenda c&p za hbr za nje sababu ya uvivu.

Hivi baraza la mawaziri limetangazwa likiwa na nyongeza ya wizara napata swali la kuandika na kuuliza kwann wizara zimeongezeka? Wakati Mkuu alitangaza kupunguza wizara kubana matumizi ya serikali.

Ndo maana waandishi waliokuwepo siku ile waliingia baridi kuuliza swali? Kwann walisahau? Au walikosa kumbukumbu? Au jibu wanalijua je ni sawa jibu ukilijua usiulize kwa niaba ya wasikilizaji.

Paskal kwa majadiliano binafsi nakukubali saana na Uwezo huo huupati hivi hivi tu ni kwa kusoma, kuongea na watu, kusikiliza vyombo mbalimbali vya hbr na kupenda midahalo.

Mwandishi au mtangazaji usikurupuke bila maandalizi kwenye jambo lolote bila maandalizi mnaiangusha tasnia
 
Bwana Paskali, waandishi wengi hivi sasa wamekuwa waoga na wanashindwa kuwa wadadisi na kuogopa kuhoji zaidi ya kile mamlaka inachokihitaji. Bahati mbaya sana tumeshaingia katika mtego wa kupitisha sheria zenye kuzuia hulka ya kuhoji na kudadisi. Tumewaruhusu wenye mamlaka kutumia neno UCHOCHEZI ambalo linafifisha fikra mbadala na kuzuia kabisa jamii yenye uwezo wa kufikiri na kuvumbua fikra mpya.
 
Tanzania tuna wale waandihshi wa habari wengi wenye elimu ya hapa na pale so kutegemea watu wa aina hiyo wafanye uchambuzi wa kina wa habari fulani ni sawa na kusubiri chungwa chini ya mwembe. Vyombo vingi vya habari hapa nchini vimeajiri watu wa aina hiyo wengi sasa uchambuzi wa kina wanatoa wapi zaidi ya kutangaza na kutoa habari tu bila kuifanyia uchambuzi habari husika.
Na hii ndo hoja kuu na ya MSINGI.
 
Acha kufanya Watu wajinga na labda ukidhani humu JF kuna Watu wa ' hovyo hovyo ' Mkuu. Ukweli ni kwamba unamchukia Moses Mathew kwakuwa inajulikana ni mwana CCM na anafanya katika Gazeti la Serikali la Daily News na unamkubali na kumpenda Mansur Jumanne kwakuwa inajulikana ni ' Mwanaharakati ' halafu ni mwana CHADEMA mzuri hivyo anakukosha kwakuwa unafanana nae Kiitikadi. Tanzania itapiga hatua tu pale ' Unafiki ' wa aina yako hii utapungua au kuisha kabisa.
Mkuu Genta, huku sii kumtendea haki mchangiaji, kwanza nakiri kumfahamu Moses ni mfia chama, and he is good in his own way katika maeneo yake haswa kumtetea Magufuli na kuitetea CCM, lakini kwenye topic ya leo, there was nothing about CCM, issue ilikuwa ni news analysis, Moses amepwaya, na kiukweli tunapojadili namna ya kuisaidia nchi yetu, kati ya kundi la wasifuji, washangiliaji na wapiga makofi, na kundi la kritiki, wakosoaji na wachambuzi makini, wakosoaji wa serikali ya Magufuli ndio wanamsaidia zaidi na kulisaidia zaidi taifa hili kuliko wasifuji.

Mansoor amemalizia vizuri sana kwa kutoa wito, waandishi tumsaidie Magufuli kwa kumwambia ukweli.

P
 
Wamesema media zote zimeishia kutangaza tuu hao mawaziri na wizara zao, lakini hakuna analysis yoyote ya baraza hilo, rais Magufuli alipoingia, alijinasibu kuunda serikali ndogo kupunguza gharama, jee ni kweli baraza la mawaziri la Magufuli limepunguza gharama?, kuongezwa kwa mawaziri na manaibu 6, kunamaanisha nini kwa upande wa kuongezeka kwa gharama za uendeshaji?.

P.
Insanity doing same thing over and over again expecting different results!
 
Mkuu Pascal Mayalla,tafadhali mshauri rafiki yako Dotto asiwe anamualika huyo Moses Mathew,maana sisi watazamaji hakuna chochote tupatacho/tunufaikacho toka kwake. Ni mtupu wa kupindukia.
Mkuu, residentura, huku kutakuwa ni kumuingilia Dotto, ila pia kutomualika fulani kwa vile wewe humpendi sio kumtendea haki, na pia sii kweli kwamba hakuna mkipatacho kutoka kwa Moses, jamaa ni very good in his own way, tena kiukweli ni mtu muhimu sana na very strategic kuwepo/kualikwa, kwa sababu hata ganda la mua la jana, kwa chungu kwake ni kivuno, hivyo kuna siku Moses anatema madini muhimu na kubalance kipindi haswa kwa kumzingatia mmiliki na nani walioshika mpini.
P.
 
Uhuru wa Vyombo vya habari ni mdogo sana mkuu paskali ili viweze kufanya analysis openly, Mkuu wa nchi anaweza kutokuwa na Tatizo na media ila aliowapa dhama ministries wakaminya uhuru ili waonekane ni wachapa kazi
 
Mayala mi nahisi hilo linachangiwa na kutokuwa na uhuru kamili wa vyombo vya habari,unakumbuka kilichomkuta Jenerali Ulimwengu miaka ile,pamoja na kufungiwa na fine za mara kwa mara wanazopigwa zinawatia uwoga.Raisi ana dictate nini kiandikwe na nini kisiandikwe na vyombo vya habari tena live unategemea nini,mwishi wa siku waandishi nao ni watu na wana mkate wao wakuupigania ili watoto waweze kupishana msalani kwa mtiririko mzuri.
Kama vipi rudisha kile kipindi cha kiti moto(tafuta jina jipya lakini)alafu tupime upepo
 
Yawezekana ni kweli mkuu, yawezekana pia waandishi inabidi waongeze kuwa makini katika kutafuta habari, mahojiano, uchambuzi na utangazaji, kukosolewa kwa mazuri hakuna ubaya, binadamu twajifunza kipya kila siku..
Lakini nyie waandishi nawo msijisikie vibaya, maana ukipiga % ya wasomaji "Broad sheets" ni wachache, labda bado ile tabia ya kupenda kusoma habari muhimu haijapata mwamko sana kwetu, wasomaji wengi yaonekana wanashabikia zaidi habari za "Udaku" zaidi kuliko zile zinazohusu dola na mwelekeo wa nchi yao..Je vijana hawavutiwi na viongozi wao nchini? Yawezekana viongozi wanahitaji kuzidisha ukaribu wao na vijana wa sasa, kuwahusisha katika maamuzi kwa kupata maoni yao..
Safari ni ndefu, ila Mwakyembe na Ndalichako wanatakiwa kuliona hili...
 
Wanabodi,

Kama kawaida ya Jumamosi asubuhi, Star TV, kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, leo, kipindi kimeiponda media ya Tanzania kuwa vina uwezo duni wa kufanya news analysis, kazi kubwa media ya Tanzania inayofanya ni kuhabarisha tuu jamii kuhusu matukio, lakini hakuna media zinazofanya news analysis kupitia kitu kinachoitwa interpretative journalism, kuwaeleza wasomaji, watazamaji na wasikilizaji kufanya evaluation ya hizo habari zina maana gani kwa taifa letu.

Wakatolea mfano mabadiliko ya baraza la mawaziri, yaliyofanyika hivi karibuni, media zote zimeishia kuhabarisha tuu fulani na fulani wameteuliwa, lakini hakuna media iliyofanya any news analysis, kuwaeleza Watanzania, what does that mean.

Endelea kufuatilia.

Paskali

Paskali,
Bro huwa napenda sana kusikiliza kipindi cha StarV cha 'Jicho letu Ndani ya Habari' jamaa wako vizuri pamoja na kwamba mmmiliki wake ni Kada wa CCM aliyepigwa chini na kutaka kufilisiwa. Kuna huyu Dotto Bulendu yuko vizuri kwenye uchambuzi wa Habari.
Ninakubaliana na hoja hiyo ya kwamba media za Bongo zimejaa hja nyepesinyepesi na zisizo na hii kitu inaitwa Investigative Journalism..!! Yaani media wanazungumzia mambo mazito kwa habari za juujuu tu yaani kama ile tunaitwa C&P(copy n paste).
Kama walivyotolea mfano wa Baraza Jipya la Mawaziri, mtu kama Kangi Lugola(MB) Mwibara aliyekuwa na tuhuma za kuomba na kupokea Rushwa kwenye awamu hii inakuwaje leo anaonekana na malaika na kupewa Unaibu Waziri...???
Kwanini media hawakuhoji hilo???Yule binti Juliana Chonza(kicheche)alipewa Uwaziri kwa sifa zipi hasa?? Chonza alitokea CHADEMA huko nyuma leo anaonekana lulu kwa JPM....! Je, kagawa uroda kwa mkuu au ni aksante ya kuwakomoa kina Mdee na Bulaya kwa kupeleka hoja ya kuongezewa adhabu ya kukaa nje ya Bunge kwa miaka 2???
 
Paskali,
Bro huwa napenda sana Yule binti Juliana Chonza(kicheche)alipewa Uwaziri kwa sifa zipi hasa?? Chonza alitokea CHADEMA huko nyuma leo anaonekana lulu kwa JPM....! Je, kagawa uroda kwa mkuu au ni aksante ya kuwakomoa kina Mdee na Bulaya kwa kupeleka hoja ya kuongezewa adhabu ya kukaa nje ya Bunge kwa miaka 2???
Mkuu Mzalendo,
kumuulizia tuu kwa nini huyo binti sio kumtendea haki, unless kama unazo sababu zilizowafanya mawaziri wengine wote wanawake kuteuliwa.
Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi ...
P.
 
Ndugu yangu Mayalla, ni kweli lakini uchambuzi makini na huru unafanyika katika jamii iliyo huru vyombo vya habari vikiwemo. Kwa mazingira ya sasa inakuwa vigumu, iwe kwa mwandishi mwenyewe, mhariri au mmiliki wa chombo husika. Pili kuna hili la kujipendekeza, ambayo ni kansa ya Afrika. Mtu kama Moses Mathew anadhani kwa kutosema ukweli atawafurahisha wakubwa apewe cheo, sasa huyo ambaye anajua anachofanya na analenga nini, mhariri na uwezo wake wa kuchambua ni tumbo lake. Huo ni ujinga wa kujitakia, lakini kimsingi, vyombo vya habari na wanahabari wenyewe wamebanwa sana.
 
Ndugu yangu Mayalla, ni kweli lakini uchambuzi makini na huru unafanyika katika jamii iliyo huru vyombo vya habari vikiwemo. Kwa mazingira ya sasa inakuwa vigumu, iwe kwa mwandishi mwenyewe, mhariri au mmiliki wa chombo husika. Pili kuna hili la kujipendekeza, ambayo ni kansa ya Afrika. Mtu kama Moses Mathew anadhani kwa kutosema ukweli atawafurahisha wakubwa apewe cheo, sasa huyo ambaye anajua anachofanya na analenga nini, mhariri na uwezo wake wa kuchambua ni tumbo lake. Huo ni ujinga wa kujitakia, lakini kimsingi, vyombo vya habari na wanahabari wenyewe wamebanwa sana.
 
Back
Top Bottom