Vyombo vya habari tanzania vimelala

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
taarifa za ajali ya meli leo Zanzibar imechelewa kutufikia watanzania, muda mwingi vyombo hivi vinapiga muziki kama vile Tz ni nchi ya musician....

nimeangalia chanel tena habari,wameshidwa hata kutupa picha eti wanaongea kwa simu na mwandishi wa habari(munir zakaria),mnataka kwenda digital wakati hata analog hamuiwezi..........
 
Tunaitegemea tbc ndio iwe ya kwanza kutoa habari zilizokamilika lakini hamna chochote,mpaka jana saa 2 usiku hawakuwa na picha hata za shughuli za uokoaji au kuhoji hata walionusurika sasa tutalaumu vipi vyombo vingine ambavyo hata uwezo wake kifedha ni mdogo?lawama zote kwanza ni kwa tbc wanaohudumiwa na kodi zetu
 
MI NILIDHANI WAZANZIBAR WAMEJIENGUA KWENYE MUUNGANO.. Kumbe Bado Wanautamani hata Vyombo Vyao haviripoti wanategemea vya Tanganyika...
 
Tunaitegemea tbc ndio iwe ya kwanza kutoa habari zilizokamilika lakini hamna chochote,mpaka jana saa 2 usiku hawakuwa na picha hata za shughuli za uokoaji au kuhoji hata walionusurika sasa tutalaumu vipi vyombo vingine ambavyo hata uwezo wake kifedha ni mdogo?lawama zote kwanza ni kwa tbc wanaohudumiwa na kodi zetu

Umenikumbusha IGUNGA. ITV wanatangaza Matokeo TBC wanaonyesha Taarabu.
 
Back
Top Bottom